Introduction-to-Computers/C2/Google-Drive-Options/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Revision as of 17:45, 9 May 2025 by Ketkinaina (Talk | contribs)

(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Habari na karibu kwenye Mafunzo Simulizi, kuhusu Uunganishaji wa Printa
00:06 Katika mafunzo haya, tutajifunza kuunganisha printa kwenye computer.
00:11 Kwa mafunzo haya, ninatumia
00:13 Ubuntu Linux 12.10 OS
00:17 na Cannon Printa
00:20 Wacha nikutambulishe haraka, kwa sehemu mbali-mbali za kompyuta.
00:25 Hii ni CPU,
00:27 Monitor,
00:29 Keyboard, Mouse
00:32 na Printa
00:34 Hebu, tutizame kwenye CPU.
00:41 Katika CPU nyingi, kuna baadhi ya milango ya USB upande wa mbele.
00:46 na nyingine nyuma.
00:49 Sasa, tuangalie printa yetu.
00:53 Kawaida, kuna swichi ya umeme upande wa mbele au sehemu ya juu ya printa.
01:00 Na kuna nafasi ya umeme na mlango wa USB, upande wa nyuma wa printa.
01:11 Kuunganisha printa kwenye kompyuta, tunahitaji kutumia waya wa USB.
01:16 Tuchomeke waya wa USB kwenye Printa
01:22 Sasa, hebu tuunganishe ncha nyingine ya waya, kwenye mlango wa USB wa CPU.
01:30 printa yetu sasa imeunganishwa kwenye kompyuta.
01:33 Washa kitufe cha umeme kwenye printa.
01:37 Sasa, hebu tusanidi printa kwa kutumia kompyuta yetu.
01:43 Twende kwenye Desktop.
01:46 Bofya ikoni ya Dash Home, upande wa juu kushoto wa upau wa kizindua
01:53 Katika Search bar, andika Printing.
01:58 Ikoni ya printa itaonekana.
02:02 Bofya juu yake.
02:04 Katika matoleo ya zamani ya Ubuntu, bofya
02:07 System, Administration,
02:09 na Printing.
02:12 Sasa kisanduku cha mazungumzo cha Printing kitaonekana.
02:16 Kinasema - There are no printers configured yet.
02:21 Kwenye kona ya juu kushoto, kuna kitufe kinachoitwa Ongeza chenye alama ya Jumlisha ya kijani juu yake. Bofya hicho
02:30 Itafungua kisanduku cha mazungumzo cha New Printa
02:34 Upande wa kushoto, orodha ya vifaa vya printa vilivyounganishwa na kompyuta itaonekana.
02:42 Hapa, tuchague printa yetu, yaani Cannon printa na tubofye Forward.
02:51 Kisha, itaendelea kutafuta drivers moja kwa moja. Nitabofya Cancel.
02:59 Sasa kisanduku cha mazungumzo kitabadilika kwenda kwenye chaguo la Choose Driver.
03:04 Chaguo la Msingi litafanya kazi katika hali nyingi.
03:08 Kwa kuwa nina Canon printa, hapa kwenye orodha, imechaguliwa moja kwa moja.
03:16 Sasa bofya Forward.
03:19 Kwenye ukurasa wa Mfumo, mfumo wa printa yangu umetambuliwa moja kwa moja.
03:26 Imeonyeshwa kama Imependekezwa, ndani ya mabano.
03:31 Pia, katika Programu Endeshaji, inaonyesha programu endeshaji inayofaa kwa printa yangu
03:38 Sasa, bofya Forward tena.
03:42 Sasa, tunahimizwa kuelezea printer yetu - jina la printa na eneo lake.
03:49 Nitakiacha kama msingi, na kubofya Apply.
03:53 printa yetu imejumuishwa vema, kwenye kompyuta yetu.
04:00 Ujumbe unaonekana: “Would you like to print a test page?”
04:04 Hebu tubofye chaguo la Print Test Page.
04:08 Dirisha dogo litaonekana na ujumbe:
04:12 “Submitted – Test Page submitted as job ...” na nambari yake.
04:18 Bofya OK.
04:20 Kisha tena bofya OK, kwenye kisanduku cha mazungumzo cha Sifa za printa.
04:24 Hapa kuna karatasi yetu ya majaribio iliyochapishwa kutoka kwenye printa yetu.
04:29 Sasa printa yetu iko tayari kuchapisha hati zetu.
04:34 Tufunge kisanduku cha mazungumzo cha Printa
04:37 Hebu nionyeshe haraka jinsi ya kuchapisha hati.
04:42 Tufungue hati.
04:45 Kisha, bonyeza vitufe vya Ctrl na P kwa pamoja.
04:49 Kisanduku cha mazungumzo cha Print, kitaonekana.
04:53 Angalia kuwa printa iliyounganishwa imechaguliwa moja kwa moja.
04:58 Katika kisanduku hiki, tuna chaguzi kadhaa.
05:03 Range inaturuhusu kuchagua anuwai ya kurasa tunazotaka kuchapisha.
05:08 Kuna chaguzi kadhaa chini ya Range:
05:12 Chaguo la All pages linachapisha kurasa zote kwenye hati.
05:16 Chaguo la Current page linachapisha ukurasa wa sasa pekee.
05:22 Chaguo la Pages linachapisha kurasa kulingana na tulivyoainisha, kwa mfano, 3-4.
05:31 Sasa, tuangalie chaguzi zinazopatikana chini ya Copies.
05:36 Chaguo la Copies ndilo tunachagua idadi ya nakala tunazotaka kuchapisha.
05:42 Tukibadilisha Copies kuwa 2, basi nakala 2 za kurasa zilizochaguliwa zitachapishwa.
05:49 Kisha bofya kitufe cha Print.
05:52 Ikiwa umeisanidi printa yako vizuri, hati yako itaanza kuchapishwa.
05:58 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. Katika mafunzo haya, tulijifunza:
06:05 Kuunganisha printa kwenye kompyuta,
06:07 Kusanidi mipangilio ya printa, na
06:10 Kuchapisha hati.
06:12 Pia tulijifunza kuhusu chaguzi mbalimbali za uchapishaji.
06:17 Tunatumaini taarifa hii ilikuwa ya msaada.
06:20 Tazama video inayopatikana katika kiungo kifuatacho.
06:24 Inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial.
06:27 Ikiwa huna mtandao wenye kasi nzuri, unaweza kupakua na kuitazama.
06:32 Timu ya Mradi wa Spoken Tutorial: Huendesha warsha kwa kutumia spoken tutorials. Hutoa vyeti kwa wale wanaofaulu mtihani wa mtandaoni. Kwa maelezo zaidi, tafadhali andika kwa: contact at spoken hyphen tutorial dot org.
06:49 Mradi wa Spoken Tutorial ni sehemu ya mradi wa Talk to a Teacher. Una-dhaminiwa na National Mission on Education through ICT, MHRD, Serikali ya India.
07:10 Maelezo zaidi kuhusu Mission hii yanapatikana kwenye: spoken hyphen tutorial dot org slash NMEICT hyphen Intro.
07:12 Asante kwa kutazama.
07:16 Script ya mafunzo haya iliandikwa na Praveen.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina