Introduction-to-Computers/C2/Google-Drive-Options/Swahili
From Script | Spoken-Tutorial
| Time | Narration |
| 00:01 | Habari na karibu kwenye Mafunzo Simulizi, kuhusu Uunganishaji wa Printa |
| 00:06 | Katika mafunzo haya, tutajifunza kuunganisha printa kwenye computer. |
| 00:11 | Kwa mafunzo haya, ninatumia |
| 00:13 | Ubuntu Linux 12.10 OS |
| 00:17 | na Cannon Printa |
| 00:20 | Wacha nikutambulishe haraka, kwa sehemu mbali-mbali za kompyuta. |
| 00:25 | Hii ni CPU, |
| 00:27 | Monitor, |
| 00:29 | Keyboard, Mouse |
| 00:32 | na Printa |
| 00:34 | Hebu, tutizame kwenye CPU. |
| 00:41 | Katika CPU nyingi, kuna baadhi ya milango ya USB upande wa mbele. |
| 00:46 | na nyingine nyuma. |
| 00:49 | Sasa, tuangalie printa yetu. |
| 00:53 | Kawaida, kuna swichi ya umeme upande wa mbele au sehemu ya juu ya printa. |
| 01:00 | Na kuna nafasi ya umeme na mlango wa USB, upande wa nyuma wa printa. |
| 01:11 | Kuunganisha printa kwenye kompyuta, tunahitaji kutumia waya wa USB. |
| 01:16 | Tuchomeke waya wa USB kwenye Printa |
| 01:22 | Sasa, hebu tuunganishe ncha nyingine ya waya, kwenye mlango wa USB wa CPU. |
| 01:30 | printa yetu sasa imeunganishwa kwenye kompyuta. |
| 01:33 | Washa kitufe cha umeme kwenye printa. |
| 01:37 | Sasa, hebu tusanidi printa kwa kutumia kompyuta yetu. |
| 01:43 | Twende kwenye Desktop. |
| 01:46 | Bofya ikoni ya Dash Home, upande wa juu kushoto wa upau wa kizindua |
| 01:53 | Katika Search bar, andika Printing. |
| 01:58 | Ikoni ya printa itaonekana. |
| 02:02 | Bofya juu yake. |
| 02:04 | Katika matoleo ya zamani ya Ubuntu, bofya |
| 02:07 | System, Administration, |
| 02:09 | na Printing. |
| 02:12 | Sasa kisanduku cha mazungumzo cha Printing kitaonekana. |
| 02:16 | Kinasema - There are no printers configured yet. |
| 02:21 | Kwenye kona ya juu kushoto, kuna kitufe kinachoitwa Ongeza chenye alama ya Jumlisha ya kijani juu yake. Bofya hicho |
| 02:30 | Itafungua kisanduku cha mazungumzo cha New Printa |
| 02:34 | Upande wa kushoto, orodha ya vifaa vya printa vilivyounganishwa na kompyuta itaonekana. |
| 02:42 | Hapa, tuchague printa yetu, yaani Cannon printa na tubofye Forward. |
| 02:51 | Kisha, itaendelea kutafuta drivers moja kwa moja. Nitabofya Cancel. |
| 02:59 | Sasa kisanduku cha mazungumzo kitabadilika kwenda kwenye chaguo la Choose Driver. |
| 03:04 | Chaguo la Msingi litafanya kazi katika hali nyingi. |
| 03:08 | Kwa kuwa nina Canon printa, hapa kwenye orodha, imechaguliwa moja kwa moja. |
| 03:16 | Sasa bofya Forward. |
| 03:19 | Kwenye ukurasa wa Mfumo, mfumo wa printa yangu umetambuliwa moja kwa moja. |
| 03:26 | Imeonyeshwa kama Imependekezwa, ndani ya mabano. |
| 03:31 | Pia, katika Programu Endeshaji, inaonyesha programu endeshaji inayofaa kwa printa yangu |
| 03:38 | Sasa, bofya Forward tena. |
| 03:42 | Sasa, tunahimizwa kuelezea printer yetu - jina la printa na eneo lake. |
| 03:49 | Nitakiacha kama msingi, na kubofya Apply. |
| 03:53 | printa yetu imejumuishwa vema, kwenye kompyuta yetu. |
| 04:00 | Ujumbe unaonekana: “Would you like to print a test page?” |
| 04:04 | Hebu tubofye chaguo la Print Test Page. |
| 04:08 | Dirisha dogo litaonekana na ujumbe: |
| 04:12 | “Submitted – Test Page submitted as job ...” na nambari yake. |
| 04:18 | Bofya OK. |
| 04:20 | Kisha tena bofya OK, kwenye kisanduku cha mazungumzo cha Sifa za printa. |
| 04:24 | Hapa kuna karatasi yetu ya majaribio iliyochapishwa kutoka kwenye printa yetu. |
| 04:29 | Sasa printa yetu iko tayari kuchapisha hati zetu. |
| 04:34 | Tufunge kisanduku cha mazungumzo cha Printa |
| 04:37 | Hebu nionyeshe haraka jinsi ya kuchapisha hati. |
| 04:42 | Tufungue hati. |
| 04:45 | Kisha, bonyeza vitufe vya Ctrl na P kwa pamoja. |
| 04:49 | Kisanduku cha mazungumzo cha Print, kitaonekana. |
| 04:53 | Angalia kuwa printa iliyounganishwa imechaguliwa moja kwa moja. |
| 04:58 | Katika kisanduku hiki, tuna chaguzi kadhaa. |
| 05:03 | Range inaturuhusu kuchagua anuwai ya kurasa tunazotaka kuchapisha. |
| 05:08 | Kuna chaguzi kadhaa chini ya Range: |
| 05:12 | Chaguo la All pages linachapisha kurasa zote kwenye hati. |
| 05:16 | Chaguo la Current page linachapisha ukurasa wa sasa pekee. |
| 05:22 | Chaguo la Pages linachapisha kurasa kulingana na tulivyoainisha, kwa mfano, 3-4. |
| 05:31 | Sasa, tuangalie chaguzi zinazopatikana chini ya Copies. |
| 05:36 | Chaguo la Copies ndilo tunachagua idadi ya nakala tunazotaka kuchapisha. |
| 05:42 | Tukibadilisha Copies kuwa 2, basi nakala 2 za kurasa zilizochaguliwa zitachapishwa. |
| 05:49 | Kisha bofya kitufe cha Print. |
| 05:52 | Ikiwa umeisanidi printa yako vizuri, hati yako itaanza kuchapishwa. |
| 05:58 | Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. Katika mafunzo haya, tulijifunza: |
| 06:05 | Kuunganisha printa kwenye kompyuta, |
| 06:07 | Kusanidi mipangilio ya printa, na |
| 06:10 | Kuchapisha hati. |
| 06:12 | Pia tulijifunza kuhusu chaguzi mbalimbali za uchapishaji. |
| 06:17 | Tunatumaini taarifa hii ilikuwa ya msaada. |
| 06:20 | Tazama video inayopatikana katika kiungo kifuatacho. |
| 06:24 | Inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial. |
| 06:27 | Ikiwa huna mtandao wenye kasi nzuri, unaweza kupakua na kuitazama. |
| 06:32 | Timu ya Mradi wa Spoken Tutorial: Huendesha warsha kwa kutumia spoken tutorials. Hutoa vyeti kwa wale wanaofaulu mtihani wa mtandaoni. Kwa maelezo zaidi, tafadhali andika kwa: contact at spoken hyphen tutorial dot org. |
| 06:49 | Mradi wa Spoken Tutorial ni sehemu ya mradi wa Talk to a Teacher. Una-dhaminiwa na National Mission on Education through ICT, MHRD, Serikali ya India. |
| 07:10 | Maelezo zaidi kuhusu Mission hii yanapatikana kwenye: spoken hyphen tutorial dot org slash NMEICT hyphen Intro. |
| 07:12 | Asante kwa kutazama. |
| 07:16 | Script ya mafunzo haya iliandikwa na Praveen. |