Introduction-to-Computers/C2/Introduction-to-Gmail/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Revision as of 17:35, 9 May 2025 by Ketkinaina (Talk | contribs)

(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye Mafunzo Simulizi, kuhusu Chaguzi za Kuandika Baruapepe.
00:07 Katika somo hili, tutajifunza:
00:10 kuhusu wapokeaji wa barua pepe, yaani- To, Cc, Bcc.
00:16 Kupanga maandishi ya barua pepe
00:19 Kuambatanisha faili kwenye barua pepe
00:22 Kushiriki faili kupitia Google Drive
00:25 Kuingiza picha au kiunganishi ndani ya barua pepe
00:29 na kuhusu chaguzi za Dirisha la Kuandika
00:33 Kwa somo hili, utahitaji muunganisho wa intaneti unaofanya kazi
00:38 na kivinjari cha wavuti.
00:40 Kwa onyesho hili, nitakuwa natumia kivinjari cha wavuti cha Firefox.
00:45 Tuanze. Fungua kivinjari chako cha wavuti na andika: http://gmail.com
00:55 Ukurasa wa Login page unafunguka.
00:58 Weka jina la mtumiaji na nywila kwenye masanduku ya maandishi husika
01:04 Kama ukurasa wa kuingia ukifunguka na kuonyesha jina la mtumiaji, hii inamaanisha kuwa tayari umeshafikia akaunti hii kutoka kwenye kompyuta yako
01:12 Weka Nywila
01:15 na ubofye kitufe cha Sign in.
01:18 Tupo kwenye ukurasa wetu wa Gmail page.
01:21 Sasa, hebu tuangalie chaguzi zilizopo kwa kuandika barua pepe.
01:26 Kwanza, hebu tubofye kitufe cha Compose.
01:31 Dirisha la Compose linafunguka.
01:34 Sehemu ya To ni mahali ainisha wapokeaji.
01:38 Ina chaguzi tatu, To, Cc na Bcc.
01:44 Cc inamaanisha "Carbon Copy " na "Bcc" inamaanisha "Blind Carbon Copy".
01:51 Tunahitaji kuweka anwani ya barua pepe ya yule tunayemtumia kwenye sehemu ya To.
01:58 Hii ni picha ya skrini.
02:01 Tukitaka kutuma barua pepe hiyo kwa watu zaidi ya mmoja, ongeza tu email-ids kwenye sehemu ya To.
02:09 Hii ni picha ya skrini.
02:12 Tumia chaguo la Cc kupeleka nakala ya barua pepe kwa wengine.
02:18 Wapokeaji wote waliowekwa kwenye To na Cc wanaweza kuona wapokeaji wengine wote.
02:25 Hii ni picha ya skrini.
02:28 Tunaweza pia kutumia chaguo la Bcc kutuma nakala fiche kwa wengine.
02:34 Katika chaguo hili, wapokeaji wa To na Cc hawawezi kuona walioko kwenye Bcc.
02:42 Mpokeaji aliye kwenye Bcc anaweza kuona walioko To na Cc
02:47 lakini hawezi kuona wapokeaji wengine wa Bcc.
02:51 Mtumaji wa barua anaweza kuona orodha kamili ya wapokeaji.
02:55 Hii ni picha ya skrini.
02:58 Jambo la Kuzingatia:
03:00 Tunaweza kuongeza idadi yoyote ya email-ids kwenye sehemu ya wapokeaji - To, Cc na Bcc.
03:08 Lakini kikomo cha juu ni wapokeaji 500 kwa siku.
03:13 Kila barua pepe lazima itenganishwe kwa nafasi, koma au kolon.
03:20 Hebu sasa turudi kwenye dirisha letu la Gmail Compose window.
03:25 Kwa kawaida, cursor ipo kwenye sehemu ya To.
03:29 Tutaingiza anwani za wapokeaji kama ifuatavyo-
03:33 Katika sehemu ya To, tutaweka barua pepe: "ray.becky.0808@gmail.com".
03:46 Katika sehemu ya Cc, "0808iambecky@gmail.com".
03:55 Katika sehemu ya Bcc, "stlibreoffice@gmail.com" na "info@spoken-tutorial.org".
04:10 Bofya kwenye mstari wa Subject na andika maelezo mafupi ya barua pepe yako.
04:15 Nitaandika: "Partner with us".
04:19 Katika eneo la maandishi, hebu tuandike ujumbe:
04:24 Spoken Tutorial Project is helping to bridge the digital divide.
04:29 Gmail hutuwezesha kufanya mpangilio wa msingi wa maandishi katika sehemu Kuu ya barua pepe yetu
04:35 Huonyeshwa, kwa chaguo-msingi, chini ya dirisha la Kuandika
04:41 Kama haionekani, ili kufikia formatting toolbar, bofya kitufe cha Formatting options.
04:47 Hapa, tuna chaguzi kama vile aina tofauti za Font, Size, Bold, Italic, Underline, Text color, Align, Numbered na Bulleted Lists na Indentation.
05:03 Chaguzi hizi zinafanana kabisa na programu yoyote ya Word Processor application.
05:08 Unaweza kuchunguza chaguzi hizi mwenyewe.
05:12 Hivi ndivyo nilivyopanga maandishi yangu.
05:16 Ili kuficha formatting toolbar, bofya kitufe cha Formatting options.
05:22 Katika Compose window, kuna chaguzi za kuambatanisha files, photos, links na emoticons.
05:32 Ili kushiri files au documents na wengine,
05:35 tunaweza kutumia chaguzi za Attach files au Insert files using Drive.
05:41 Watoa huduma wote wa Mail huruhusu kutuma faili kama attachment.
05:46 Unaweza kuambatisha faili hadi ukubwa wa megabaiti 25 (MB).
05:51 Ili kutuma faili kubwa zaidi ya hiyo, unaweza kutumia chaguo la Insert files using Drive.
05:59 Hebu kwanza tuambatanishe faili la 'pdf' lenye ukubwa wa chini ya 1Mb.
06:04 Bofya kwenye Attach file icon inayofanana na klipu ya karatasi.
06:09 Hii itafungua file browser.
06:12 Tafuta na uchague faili unayotaka kutuma kupitia barua pepe.
06:16 Kutoka kwenye Desktop, nitachagua "myscript.pdf" na kubofya Open.
06:23 Tunaweza kuona faili yetu inaambatanishwa kwenye barua pepe yetu.
06:27 Faili nyingi pia zinaweza kuambatanishwa kwenye barua pepe moja kwa kutumia chaguo la Attach files.
06:34 Ili kuondoa faili ulilolambatanisha kwenye ujumbe, bofya alama ya 'x' upande wa kulia wa jina la faili.
06:41 Sasa, hebu tuambatanishe faili lenye ukubwa wa karibu 30Mb.
06:46 Nina zip file kwenye Desktop yangu yenye ukubwa wa takriban 30Mb.
06:52 Bofya tena ikoni ya Attach files.
06:56 Tafuta na uchague faili ya zip yenye ukubwa wa 30Mb na ubofye Open.
07:02 Tutapata ujumbe wa popup:
07:04 "The file you are trying to send exceeds the 25mb attachment limit".
07:09 Na unatupatia chaguo la Send using Google drive.
07:14 Bofya kitufe cha Send using google drive.
07:18 Hebu nikalifunge hili kwa sasa.
07:21 Kubofya chaguo la Insert files using Drive pia kunatufikisha kwenye window ile ile kama awali.
07:28 Hapa, tunaweza kuona tabs tatu:
07:31 My Drive, Shared with me na Upload.
07:36 Kwa chaguo-msingi, faili ambazo tayari zimepakiwa zitapatikana chini ya My Drive tab.
07:43 Hapa unaweza kuona faili moja.
07:46 Hili lilishirikishwa na Timu ya Google wakati wa kuunda akaunti.
07:51 Hebu tubofye kwenye tab ya Shared with me.
07:55 Hapa tunaona ujumbe: "No one's shared any files with you yet!"
08:00 Ikiwa mtu yeyote atakushirikisha faili, litapatikana chini ya tab ya Shared with Me.
08:06 Sasa, bofya kwenye tab ya Upload ili kupakia faili jipya.
08:12 Bofya kitufe cha Select files from your computer.
08:16 Tafuta na uchague faili kutoka kwenye mashine yako, unayotaka kupakia, na ubofye Open.
08:23 Bofya kitufe cha Add more files ikiwa unataka kuongeza faili zaidi.
08:27 Nitaachana na hii kwa sasa na kuendelea na upakiaji wa faili moja tu
08:33 Baada ya faili kuongezwa, tunapaswa kutaja jinsi inavyopaswa kuingizwa kwenye barua pepe yetu.
08:40 Angalia vitufe viwili upande wa kulia chini vinavyosema-
08:44 Insert as Drive link na
08:46 Attachment.
08:48 Kwa chaguo-msingi, Insert as Drive link limechaguliwa.
08:52 Ikiwa tutachagua Attachment, basi faili itaingizwa kama attachment.
08:57 Tutaacha kama ilivyo.
09:00 Bofya kitufe cha Upload kilicho upande wa kushoto chini ya skrini.
09:05 Utaratibu wa kupakia utaanza lakini inaweza kuchukua muda kulingana na kasi ya intaneti yako.
09:11 Baada ya kukamilika, hapa katika eneo la maudhui, tunaweza kuona link ya faili iliyopakiwa.
09:17 Sasa hebu tubofye kwenye chaguo la Insert Photo ili kuingiza Picha kwenye barua pepe.
09:24 Dirisha la Upload Photos linafunguka.
09:27 Tunaweza kupakia picha kutoka kwenye kompyuta yetu au kwa kutoa anwani ya tovuti ya picha.
09:34 Kwa sasa, sitaki upload picha yoyote.
09:38 Kwa hiyo, nitabofya kitufe cha Cancel.
09:41 Unaweza kuchunguza chaguo hili mwenyewe.
09:44 Chaguo linalofuata ni Insert Link. Hebu tubofye hapo.
09:49 Dirisha la mazungumzo la Edit Link linafunguka.
09:53 Katika sehemu ya Text to display, andika maandishi unayotaka yawe kiungo.
09:58 Nitaandika Spoken Tutorial.
10:02 Katika sehemu ya Link to, kwa chaguo-msingi, chaguo la Web address, limechaguliwa.
10:08 Katika sehemu ya maandishi, andika: url kama http://spoken-tutorial.org
10:20 kisha bofya kitufe cha OK.
10:23 Sasa, katika eneo la maudhui, unaweza kuona maandishi Spoken Tutorial na yamewekwa kiungo.
10:29 Hebu nibofye maandishi yenye kiungo.
10:32 Dirisha dogo la pop window linafunguka chini ya maandishi.
10:35 Inaonyesha- Go to link:.
10:38 Kubofya kwenye URL inayoonyeshwa, kutakupeleka kwenye Homepage ya tovuti ya Spoken Tutorial.
10:45 Ili kubadilisha URL au kuondoa link, tunaweza kubofya chaguo la Change au Remove.
10:53 Tunaweza pia kuingiza vielelezo mbalimbali kwa msaada wa ikoni ya emoticon.
10:59 Tumia kipengele hiki katika mawasiliano yako ya barua pepe pale inapohitajika.
11:04 Angalia maandishi Saved kabla ya ikoni ya Trash.
11:08 Kila tunapoongeza au kuondoa maudhui, barua pepe yetu itaifadhiwa moja kwa moja kwenye Drafts folder.
11:16 Hii ni msaada mkubwa kwa kupata ujumbe wetu wa kuandikwa, iwapo kutatokea kukatika kwa umeme au mtandao.
11:24 Ikiwa tunataka kufuta ujumbe huu, bofya kwenye ikoni ya Trash.
11:28 Kitendo hiki kitaifuta barua pepe kutoka kwenye Drafts folder pia.
11:34 Bofya kwenye kitufe cha More options kilicho karibu na ikoni ya Trash.
11:39 Chaguo la Default to full-screen litafanya Compose window kuwa kubwa.
11:44 Label – Tutajifunza kuhusu kipengele hiki katika mafunzo yajayo.
11:49 Chaguo la Plain text mode litaondoa mipangilio yote ya maandishi na kubadilisha barua pepe kuwa maandishi rahisi tu.
11:57 Chaguo la Print litatuma barua pepe iliyoandikwa kwenye printer iliyosanidiwa.
12:03 Check Spelling itafanya ukaguzi wa tahajia ya maudhui yaliyoandikwa.
12:07 Sasa tuko tayari kutuma barua pepe yetu.
12:09 Bofya kitufe cha Send.
12:12 Tunapata ujumbe ufuatao kwenye skrini–
12:15 "This Drive file isn't shared with all recipients."
12:19 Hii ni kwa sababu hatukushiriki faili na watu waliotajwa kwenye barua pepe hii.
12:25 Bofya kitufe cha Share & Send.
12:29 Kwenye skrini, tutaona mojawapo ya ujumbe ufuatao:
12:32 Ujumbe wako unaendelea "sending"
12:34 au "Your message has been sent".
12:38 Ili kuona barua pepe iliyotumwa, bofya kiungo cha View Message.
12:43 Tunaweza kuona maudhui ya barua pepe tuliyotuma hapa.
12:47 Hebu tuthibitishe moja baada ya nyingine.
12:50 Hapa kuna attachments
12:52 na hapa kuna URL link.
12:55 Chini ya anwani ya barua pepe, kuna pembetatu iliyogeuzwa inayonyesha maelezo ya kichwa.
13:00 Hebu nibofye hapo.
13:03 Tunaweza kuona email-ids za wapokeaji wote kwenye sehemu za To, Cc na Bcc fields.
13:11 Hebu tuone barua pepe itaonekanaje kwa wapokeaji.
13:16 Hii ni mail-id ya mpokeaji aliyemwekwa kwenye Cc.
13:21 Unaweza kuona ujumbe uliotumwa sasa. Hebu nifungue na kusoma.
13:27 Bofya kwenye Show Details.
13:29 Inaonyesha To na Cc lakini sio wapokeaji wa Bcc.
13:35 Hii ni mail-id ya mmoja wa wapokeaji waliowekwa kwenye Bcc.
13:41 Unaweza kuona ujumbe uliotumwa sasa.
13:43 Hebu nifungue na kusoma.
13:46 Bofya kwenye Show Details.
13:49 Unaweza kuona maelezo ya wapokeaji wa To, Cc na Bcc.
13:55 Hebu nirudi kwenye akaunti ya Gmail ya mtumaji.
13:59 Tazama hapa, tuliweka wapokeaji wawili kwenye Bcc.
14:04 Lakini hapa tunaweza kuona tu email id moja. Ile nyingine haionekani.
14:10 Hivi ndivyo kipengele cha Bcc kinavyofanya kazi.
14:13 Natumaini umeweza kuelewa tofauti hizi kwa uwazi.
14:17 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya.
14:20 Hebu tufanye muhtasari.
14:22 Katika mafunzo haya, tumejifunza kuhusu:
14:25 Wapokeaji wa barua pepe, yaani, To, Cc, Bcc
14:30 Kufanya formatting ya maandishi kwenye barua pepe
14:33 Kushikiza faili kwenye barua pepe
14:36 Kushiriki faili kupitia Google Drive
14:39 Kuingiza picha au kiungo kwenye barua pepe, ...na kuhusu
14:43 chaguzi katika Compose window.
14:47 Video iliyoko kwenye kiungo kilichotolewa inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial
14:52 Tafadhali pakua na uitazame.
14:55 Tunafanya warsha na tunatoa vyeti kwa wale wanaofaulu mitihani yetu ya mtandaoni.
15:01 Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie.
15:04 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na NMEICT, MHRD, Serikali ya India.
15:11 Maelezo zaidi kuhusu dhamira hii yanapatikana kwenye kiungo hiki.
15:16 Mafunzo haya yameandaliwa na Timu ya Spoken Tutorial, IIT Bombay.
15:21 Huyu alikuwa Hokins Moshi, nikikamilisha. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina