Introduction-to-Computers/C2/Introduction-to-Gmail/Swahili
From Script | Spoken-Tutorial
| Time | Narration |
| 00:01 | Karibu kwenye Mafunzo Simulizi, kuhusu Chaguzi za Kuandika Baruapepe. |
| 00:07 | Katika somo hili, tutajifunza: |
| 00:10 | kuhusu wapokeaji wa barua pepe, yaani- To, Cc, Bcc. |
| 00:16 | Kupanga maandishi ya barua pepe |
| 00:19 | Kuambatanisha faili kwenye barua pepe |
| 00:22 | Kushiriki faili kupitia Google Drive |
| 00:25 | Kuingiza picha au kiunganishi ndani ya barua pepe |
| 00:29 | na kuhusu chaguzi za Dirisha la Kuandika |
| 00:33 | Kwa somo hili, utahitaji muunganisho wa intaneti unaofanya kazi |
| 00:38 | na kivinjari cha wavuti. |
| 00:40 | Kwa onyesho hili, nitakuwa natumia kivinjari cha wavuti cha Firefox. |
| 00:45 | Tuanze. Fungua kivinjari chako cha wavuti na andika: http://gmail.com |
| 00:55 | Ukurasa wa Login page unafunguka. |
| 00:58 | Weka jina la mtumiaji na nywila kwenye masanduku ya maandishi husika |
| 01:04 | Kama ukurasa wa kuingia ukifunguka na kuonyesha jina la mtumiaji, hii inamaanisha kuwa tayari umeshafikia akaunti hii kutoka kwenye kompyuta yako |
| 01:12 | Weka Nywila |
| 01:15 | na ubofye kitufe cha Sign in. |
| 01:18 | Tupo kwenye ukurasa wetu wa Gmail page. |
| 01:21 | Sasa, hebu tuangalie chaguzi zilizopo kwa kuandika barua pepe. |
| 01:26 | Kwanza, hebu tubofye kitufe cha Compose. |
| 01:31 | Dirisha la Compose linafunguka. |
| 01:34 | Sehemu ya To ni mahali ainisha wapokeaji. |
| 01:38 | Ina chaguzi tatu, To, Cc na Bcc. |
| 01:44 | Cc inamaanisha "Carbon Copy " na "Bcc" inamaanisha "Blind Carbon Copy". |
| 01:51 | Tunahitaji kuweka anwani ya barua pepe ya yule tunayemtumia kwenye sehemu ya To. |
| 01:58 | Hii ni picha ya skrini. |
| 02:01 | Tukitaka kutuma barua pepe hiyo kwa watu zaidi ya mmoja, ongeza tu email-ids kwenye sehemu ya To. |
| 02:09 | Hii ni picha ya skrini. |
| 02:12 | Tumia chaguo la Cc kupeleka nakala ya barua pepe kwa wengine. |
| 02:18 | Wapokeaji wote waliowekwa kwenye To na Cc wanaweza kuona wapokeaji wengine wote. |
| 02:25 | Hii ni picha ya skrini. |
| 02:28 | Tunaweza pia kutumia chaguo la Bcc kutuma nakala fiche kwa wengine. |
| 02:34 | Katika chaguo hili, wapokeaji wa To na Cc hawawezi kuona walioko kwenye Bcc. |
| 02:42 | Mpokeaji aliye kwenye Bcc anaweza kuona walioko To na Cc |
| 02:47 | lakini hawezi kuona wapokeaji wengine wa Bcc. |
| 02:51 | Mtumaji wa barua anaweza kuona orodha kamili ya wapokeaji. |
| 02:55 | Hii ni picha ya skrini. |
| 02:58 | Jambo la Kuzingatia: |
| 03:00 | Tunaweza kuongeza idadi yoyote ya email-ids kwenye sehemu ya wapokeaji - To, Cc na Bcc. |
| 03:08 | Lakini kikomo cha juu ni wapokeaji 500 kwa siku. |
| 03:13 | Kila barua pepe lazima itenganishwe kwa nafasi, koma au kolon. |
| 03:20 | Hebu sasa turudi kwenye dirisha letu la Gmail Compose window. |
| 03:25 | Kwa kawaida, cursor ipo kwenye sehemu ya To. |
| 03:29 | Tutaingiza anwani za wapokeaji kama ifuatavyo- |
| 03:33 | Katika sehemu ya To, tutaweka barua pepe: "ray.becky.0808@gmail.com". |
| 03:46 | Katika sehemu ya Cc, "0808iambecky@gmail.com". |
| 03:55 | Katika sehemu ya Bcc, "stlibreoffice@gmail.com" na "info@spoken-tutorial.org". |
| 04:10 | Bofya kwenye mstari wa Subject na andika maelezo mafupi ya barua pepe yako. |
| 04:15 | Nitaandika: "Partner with us". |
| 04:19 | Katika eneo la maandishi, hebu tuandike ujumbe: |
| 04:24 | Spoken Tutorial Project is helping to bridge the digital divide. |
| 04:29 | Gmail hutuwezesha kufanya mpangilio wa msingi wa maandishi katika sehemu Kuu ya barua pepe yetu |
| 04:35 | Huonyeshwa, kwa chaguo-msingi, chini ya dirisha la Kuandika |
| 04:41 | Kama haionekani, ili kufikia formatting toolbar, bofya kitufe cha Formatting options. |
| 04:47 | Hapa, tuna chaguzi kama vile aina tofauti za Font, Size, Bold, Italic, Underline, Text color, Align, Numbered na Bulleted Lists na Indentation. |
| 05:03 | Chaguzi hizi zinafanana kabisa na programu yoyote ya Word Processor application. |
| 05:08 | Unaweza kuchunguza chaguzi hizi mwenyewe. |
| 05:12 | Hivi ndivyo nilivyopanga maandishi yangu. |
| 05:16 | Ili kuficha formatting toolbar, bofya kitufe cha Formatting options. |
| 05:22 | Katika Compose window, kuna chaguzi za kuambatanisha files, photos, links na emoticons. |
| 05:32 | Ili kushiri files au documents na wengine, |
| 05:35 | tunaweza kutumia chaguzi za Attach files au Insert files using Drive. |
| 05:41 | Watoa huduma wote wa Mail huruhusu kutuma faili kama attachment. |
| 05:46 | Unaweza kuambatisha faili hadi ukubwa wa megabaiti 25 (MB). |
| 05:51 | Ili kutuma faili kubwa zaidi ya hiyo, unaweza kutumia chaguo la Insert files using Drive. |
| 05:59 | Hebu kwanza tuambatanishe faili la 'pdf' lenye ukubwa wa chini ya 1Mb. |
| 06:04 | Bofya kwenye Attach file icon inayofanana na klipu ya karatasi. |
| 06:09 | Hii itafungua file browser. |
| 06:12 | Tafuta na uchague faili unayotaka kutuma kupitia barua pepe. |
| 06:16 | Kutoka kwenye Desktop, nitachagua "myscript.pdf" na kubofya Open. |
| 06:23 | Tunaweza kuona faili yetu inaambatanishwa kwenye barua pepe yetu. |
| 06:27 | Faili nyingi pia zinaweza kuambatanishwa kwenye barua pepe moja kwa kutumia chaguo la Attach files. |
| 06:34 | Ili kuondoa faili ulilolambatanisha kwenye ujumbe, bofya alama ya 'x' upande wa kulia wa jina la faili. |
| 06:41 | Sasa, hebu tuambatanishe faili lenye ukubwa wa karibu 30Mb. |
| 06:46 | Nina zip file kwenye Desktop yangu yenye ukubwa wa takriban 30Mb. |
| 06:52 | Bofya tena ikoni ya Attach files. |
| 06:56 | Tafuta na uchague faili ya zip yenye ukubwa wa 30Mb na ubofye Open. |
| 07:02 | Tutapata ujumbe wa popup: |
| 07:04 | "The file you are trying to send exceeds the 25mb attachment limit". |
| 07:09 | Na unatupatia chaguo la Send using Google drive. |
| 07:14 | Bofya kitufe cha Send using google drive. |
| 07:18 | Hebu nikalifunge hili kwa sasa. |
| 07:21 | Kubofya chaguo la Insert files using Drive pia kunatufikisha kwenye window ile ile kama awali. |
| 07:28 | Hapa, tunaweza kuona tabs tatu: |
| 07:31 | My Drive, Shared with me na Upload. |
| 07:36 | Kwa chaguo-msingi, faili ambazo tayari zimepakiwa zitapatikana chini ya My Drive tab. |
| 07:43 | Hapa unaweza kuona faili moja. |
| 07:46 | Hili lilishirikishwa na Timu ya Google wakati wa kuunda akaunti. |
| 07:51 | Hebu tubofye kwenye tab ya Shared with me. |
| 07:55 | Hapa tunaona ujumbe: "No one's shared any files with you yet!" |
| 08:00 | Ikiwa mtu yeyote atakushirikisha faili, litapatikana chini ya tab ya Shared with Me. |
| 08:06 | Sasa, bofya kwenye tab ya Upload ili kupakia faili jipya. |
| 08:12 | Bofya kitufe cha Select files from your computer. |
| 08:16 | Tafuta na uchague faili kutoka kwenye mashine yako, unayotaka kupakia, na ubofye Open. |
| 08:23 | Bofya kitufe cha Add more files ikiwa unataka kuongeza faili zaidi. |
| 08:27 | Nitaachana na hii kwa sasa na kuendelea na upakiaji wa faili moja tu |
| 08:33 | Baada ya faili kuongezwa, tunapaswa kutaja jinsi inavyopaswa kuingizwa kwenye barua pepe yetu. |
| 08:40 | Angalia vitufe viwili upande wa kulia chini vinavyosema- |
| 08:44 | Insert as Drive link na |
| 08:46 | Attachment. |
| 08:48 | Kwa chaguo-msingi, Insert as Drive link limechaguliwa. |
| 08:52 | Ikiwa tutachagua Attachment, basi faili itaingizwa kama attachment. |
| 08:57 | Tutaacha kama ilivyo. |
| 09:00 | Bofya kitufe cha Upload kilicho upande wa kushoto chini ya skrini. |
| 09:05 | Utaratibu wa kupakia utaanza lakini inaweza kuchukua muda kulingana na kasi ya intaneti yako. |
| 09:11 | Baada ya kukamilika, hapa katika eneo la maudhui, tunaweza kuona link ya faili iliyopakiwa. |
| 09:17 | Sasa hebu tubofye kwenye chaguo la Insert Photo ili kuingiza Picha kwenye barua pepe. |
| 09:24 | Dirisha la Upload Photos linafunguka. |
| 09:27 | Tunaweza kupakia picha kutoka kwenye kompyuta yetu au kwa kutoa anwani ya tovuti ya picha. |
| 09:34 | Kwa sasa, sitaki upload picha yoyote. |
| 09:38 | Kwa hiyo, nitabofya kitufe cha Cancel. |
| 09:41 | Unaweza kuchunguza chaguo hili mwenyewe. |
| 09:44 | Chaguo linalofuata ni Insert Link. Hebu tubofye hapo. |
| 09:49 | Dirisha la mazungumzo la Edit Link linafunguka. |
| 09:53 | Katika sehemu ya Text to display, andika maandishi unayotaka yawe kiungo. |
| 09:58 | Nitaandika Spoken Tutorial. |
| 10:02 | Katika sehemu ya Link to, kwa chaguo-msingi, chaguo la Web address, limechaguliwa. |
| 10:08 | Katika sehemu ya maandishi, andika: url kama http://spoken-tutorial.org |
| 10:20 | kisha bofya kitufe cha OK. |
| 10:23 | Sasa, katika eneo la maudhui, unaweza kuona maandishi Spoken Tutorial na yamewekwa kiungo. |
| 10:29 | Hebu nibofye maandishi yenye kiungo. |
| 10:32 | Dirisha dogo la pop window linafunguka chini ya maandishi. |
| 10:35 | Inaonyesha- Go to link:. |
| 10:38 | Kubofya kwenye URL inayoonyeshwa, kutakupeleka kwenye Homepage ya tovuti ya Spoken Tutorial. |
| 10:45 | Ili kubadilisha URL au kuondoa link, tunaweza kubofya chaguo la Change au Remove. |
| 10:53 | Tunaweza pia kuingiza vielelezo mbalimbali kwa msaada wa ikoni ya emoticon. |
| 10:59 | Tumia kipengele hiki katika mawasiliano yako ya barua pepe pale inapohitajika. |
| 11:04 | Angalia maandishi Saved kabla ya ikoni ya Trash. |
| 11:08 | Kila tunapoongeza au kuondoa maudhui, barua pepe yetu itaifadhiwa moja kwa moja kwenye Drafts folder. |
| 11:16 | Hii ni msaada mkubwa kwa kupata ujumbe wetu wa kuandikwa, iwapo kutatokea kukatika kwa umeme au mtandao. |
| 11:24 | Ikiwa tunataka kufuta ujumbe huu, bofya kwenye ikoni ya Trash. |
| 11:28 | Kitendo hiki kitaifuta barua pepe kutoka kwenye Drafts folder pia. |
| 11:34 | Bofya kwenye kitufe cha More options kilicho karibu na ikoni ya Trash. |
| 11:39 | Chaguo la Default to full-screen litafanya Compose window kuwa kubwa. |
| 11:44 | Label – Tutajifunza kuhusu kipengele hiki katika mafunzo yajayo. |
| 11:49 | Chaguo la Plain text mode litaondoa mipangilio yote ya maandishi na kubadilisha barua pepe kuwa maandishi rahisi tu. |
| 11:57 | Chaguo la Print litatuma barua pepe iliyoandikwa kwenye printer iliyosanidiwa. |
| 12:03 | Check Spelling itafanya ukaguzi wa tahajia ya maudhui yaliyoandikwa. |
| 12:07 | Sasa tuko tayari kutuma barua pepe yetu. |
| 12:09 | Bofya kitufe cha Send. |
| 12:12 | Tunapata ujumbe ufuatao kwenye skrini– |
| 12:15 | "This Drive file isn't shared with all recipients." |
| 12:19 | Hii ni kwa sababu hatukushiriki faili na watu waliotajwa kwenye barua pepe hii. |
| 12:25 | Bofya kitufe cha Share & Send. |
| 12:29 | Kwenye skrini, tutaona mojawapo ya ujumbe ufuatao: |
| 12:32 | Ujumbe wako unaendelea "sending" |
| 12:34 | au "Your message has been sent". |
| 12:38 | Ili kuona barua pepe iliyotumwa, bofya kiungo cha View Message. |
| 12:43 | Tunaweza kuona maudhui ya barua pepe tuliyotuma hapa. |
| 12:47 | Hebu tuthibitishe moja baada ya nyingine. |
| 12:50 | Hapa kuna attachments |
| 12:52 | na hapa kuna URL link. |
| 12:55 | Chini ya anwani ya barua pepe, kuna pembetatu iliyogeuzwa inayonyesha maelezo ya kichwa. |
| 13:00 | Hebu nibofye hapo. |
| 13:03 | Tunaweza kuona email-ids za wapokeaji wote kwenye sehemu za To, Cc na Bcc fields. |
| 13:11 | Hebu tuone barua pepe itaonekanaje kwa wapokeaji. |
| 13:16 | Hii ni mail-id ya mpokeaji aliyemwekwa kwenye Cc. |
| 13:21 | Unaweza kuona ujumbe uliotumwa sasa. Hebu nifungue na kusoma. |
| 13:27 | Bofya kwenye Show Details. |
| 13:29 | Inaonyesha To na Cc lakini sio wapokeaji wa Bcc. |
| 13:35 | Hii ni mail-id ya mmoja wa wapokeaji waliowekwa kwenye Bcc. |
| 13:41 | Unaweza kuona ujumbe uliotumwa sasa. |
| 13:43 | Hebu nifungue na kusoma. |
| 13:46 | Bofya kwenye Show Details. |
| 13:49 | Unaweza kuona maelezo ya wapokeaji wa To, Cc na Bcc. |
| 13:55 | Hebu nirudi kwenye akaunti ya Gmail ya mtumaji. |
| 13:59 | Tazama hapa, tuliweka wapokeaji wawili kwenye Bcc. |
| 14:04 | Lakini hapa tunaweza kuona tu email id moja. Ile nyingine haionekani. |
| 14:10 | Hivi ndivyo kipengele cha Bcc kinavyofanya kazi. |
| 14:13 | Natumaini umeweza kuelewa tofauti hizi kwa uwazi. |
| 14:17 | Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. |
| 14:20 | Hebu tufanye muhtasari. |
| 14:22 | Katika mafunzo haya, tumejifunza kuhusu: |
| 14:25 | Wapokeaji wa barua pepe, yaani, To, Cc, Bcc |
| 14:30 | Kufanya formatting ya maandishi kwenye barua pepe |
| 14:33 | Kushikiza faili kwenye barua pepe |
| 14:36 | Kushiriki faili kupitia Google Drive |
| 14:39 | Kuingiza picha au kiungo kwenye barua pepe, ...na kuhusu |
| 14:43 | chaguzi katika Compose window. |
| 14:47 | Video iliyoko kwenye kiungo kilichotolewa inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial |
| 14:52 | Tafadhali pakua na uitazame. |
| 14:55 | Tunafanya warsha na tunatoa vyeti kwa wale wanaofaulu mitihani yetu ya mtandaoni. |
| 15:01 | Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie. |
| 15:04 | Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na NMEICT, MHRD, Serikali ya India. |
| 15:11 | Maelezo zaidi kuhusu dhamira hii yanapatikana kwenye kiungo hiki. |
| 15:16 | Mafunzo haya yameandaliwa na Timu ya Spoken Tutorial, IIT Bombay. |
| 15:21 | Huyu alikuwa Hokins Moshi, nikikamilisha. Asante kwa kutazama. |