LibreOffice-Suite-Writer-6.3/C2/Typing-text-and-basic-formatting-in-Writer/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye Spoken tutorial kuhusu Typing text and basic formatting.
00:07 Katika mafunzo haya, tutajifunza jinsi ya:
00:10 Ku-Align maandishi
00:12 - Kutumia Bullets na Numbering
00:15 - Kutumia Cut, Copy
00:19 - Kutumia chaguzi za Bold, Underline na Italic
00:24 - Kutumia Font name, Font size, na Font color kwenye Writer
00:30 Vipengele vya kupanga muundo: Kutumia vipengele hivi kunafanya document zetu kuvutia zaidi.
00:37 Zitakuwa rahisi zaidi kusoma ukilinganisha na documenti ambazo ni maandishi tupu.
00:43 Mafunzo haya yameandikwa kwa kutumia:
00:46 - Ubuntu Linux OS toleo la 18.04

- LibreOffice Suite toleo la 6.3.5

00:55 Fungua faili Resume.odt tuliloliunda awali.
01:01 Faili hili limewekwa kwako katika kiungo cha Code files kwenye ukurasa wa mafunzo haya.
01:07 Tafadhali pakua na utoe faili kutoka kwenye zipu.
01:11 Fanya nakala ya faili, kisha uitumie kwa mazoezi.
01:16 Kwanza tutajifunza jinsi ya kupangilia maandishi katika Writer.
01:20 Hapo awali tuliandika neno RESUME na kulipanga katikati ya ukurasa.
01:26 Hebu tuchague tena neno RESUME.
01:31 Ikiwa umebadilisha ukubwa wa dirisha la LibreOffice, baadhi ya aikoni huenda zisionekane.
01:37 Katika hali hiyo, bonyeza aikoni ya mishale miwili mwishoni mwa toolbar ili kuona icons zilizofichwa.
01:44 Sasa bonyeza aikoni ya Align Left kwenye Formatting toolbar.
01:49 Neno RESUME sasa limepangiliwa upande wa kushoto wa ukurasa.
01:54 Bonyeza aikoni ya Align Right. Neno RESUME limepangiliwa upande wa kulia.
02:01 Sasa bonyeza aikoni ya Justify.
02:05 Neno RESUME limewekwa kwa usawa kati ya mpaka wa kulia na kushoto.
02:11 Kipengele hiki kitaonekana zaidi tunapokuwa na mstari au aya ya maandishi.
02:17 Hebu turejeshe maandishi hadi RESUME lipangiliwe katikati.
02:23 Katika Writer, bonyeza Ctrl + Z kwenye kibodi ili kutengua tendo. Kisha ondoa uteuzi wa neno

RESUME.

02:32 Sasa bonyeza kitufe cha Enter ili kwenda kwenye mstari unaofuata.
02:37 Bonyeza Enter tena ili kuunda mstari mwingine.
02:42 Bonyeza aikoni ya Align Left kwenye toolbar.
02:46 Kisha bonyeza aikoni ya Bold kutoka kwenye toolbar ili kuondoa chaguo la bold.
02:52 Sasa hebu tujifunze kuhusu Bullets na Numbering.
02:57 Bullets na Numbering hutumika wakati tunahitaji kuandika hoja huru kwenye document.
03:03 Kila hoja huanza ama kwa bullet au number.
03:07 Bullets hutumika kwa orodha zisizo na mpangilio.
03:10 Numbering hutumika kwa orodha zenye mpangilio.
03:14 Katika Formatting toolbar, tunaweza kuona aikoni tofauti kwa ajili ya Bullets na Numbering.
03:20 Hebu bonyeza aikoni ya Bullets.
03:23 Mara moja, dot au alama ya bullet inaonekana kwenye document.
03:28 Andika herufi a na bonyeza Enter.
03:32 Andika b na bonyeza Enter.
03:36 Bonyeza aikoni ya Numbering.
03:40 Bullet inabadilika kuwa namba 1.
03:45 Andika c na bonyeza Enter.
03:49 Andika d na bonyeza Enter.
03:53 Hii inakupa picha wazi ya tofauti kati ya bullets na numbering.
03:59 Chagua maandishi yote kwa kubonyeza na kuburuta kitufe cha mausi cha kushoto.
04:04 Tutajifunza njia nyingine ya kufikia Bullets and Numbering.
04:09 Bonyeza menyu ya Format kisha chagua Bullets and Numbering.
04:16 Kisanduku cha mazungumzo cha Bullets and Numbering kinafunguka.
04:20 Kinatoa mitindo mbalimbali chini ya tab tofauti.
04:27 Chagua tab ya Bullets kama haijachaguliwa tayari.
04:31 Mitindo mingi ya bullets inaonekana.
04:34 Chagua bullets za mraba mkubwa.
04:37 Bonyeza kitufe cha OK kilicho chini kulia mwa kisanduku.
04:43 Angalia mabadiliko kwenye alama za bullet.
04:47 Fungua tena kisanduku cha Bullets and Numbering, bonyeza tab ya Numbering.
04:53 Mitindo ya numbering mingi inaonekana hapa.
04:57 Chagua mtindo wa namba za Kirumi (Roman numerals).
05:01 Bonyeza kitufe cha OK.
05:07 Angalia mabadiliko — sasa numbering inaonekana kama namba za Kirumi.
05:13 Unaweza kutumia aina yoyote ya bullets au numbering unayopenda.
05:18 Bonyeza kitufe cha Delete kwenye kibodi.
05:22 Bonyeza kitufe cha Backspace ili kuondoa numbering iliyobaki.
05:28 Fungua tena kisanduku cha Bullets and Numbering, bonyeza tab ya Numbering.
05:34 Bonyeza mtindo wa pili, kisha OK.
05:40 Tuko tayari kuandika hoja yetu ya kwanza.
05:44 Andika: NAME: RAMESH, kisha bonyeza Enter.
05:51 Bonyeza Enter baada ya kila hoja inayofuata.
05:56 Bullet inayofuata inaonyesha namba mpya.
06:00 Andika hoja ya pili: FATHER’S NAME: MAHESH.
06:06 Andika hoja ya tatu: MOTHER’S NAME: SHWETA.
06:10 Andika hoja nyingine mbili kama zinavyoonyeshwa.
06:15 Kumbuka kuhifadhi faili: bonyeza Ctrl + S.
06:20 Ni tabia nzuri kuhifadhi faili mara kwa mara.
06:25 Kunaweza kuwa na viwango vingi vya bullets au numbering.
06:30 Inategemea muundo tunaouchagua.
06:33 Hebu tuone mfano.
06:36 Nenda kwenye hoja ya namba 4 – FATHER’S OCCUPATION.
06:40 Weka mshale baada ya kolon, bonyeza Enter.
06:45 Bonyeza kitufe cha Tab mara moja.
06:48 Namba 5 inageuka kuwa bullet mpya chini ya namba 4.
06:55 Hamisha mshale hadi mwisho wa bullet point, bonyeza Enter.
07:00 Andika SELF EMPLOYED, bonyeza Enter.
07:05 Bonyeza Shift + Tab ili kupunguza uingilizi.
07:10 Bonyeza Delete hadi hoja inayofuata ije mstari mmoja juu.
07:15 Hamisha mshale mwisho wa hoja ya namba 5, bonyeza Enter. Namba 6 inaonekana.
07:23 Ili kuzima Bullets and Numbering, fungua kisanduku cha Bullets and Numbering.
07:28 Bonyeza kitufe cha Remove kilicho chini.
07:32 Mtindo wa bullets na numbering hauonekani tena.
07:38 Chunguza mwenyewe Bullets and Numbering kwenye Formatting toolbar.
07:45 Angalia — tumeandika neno NAME mara tatu kwenye document.
07:50 Badala ya kurudia, tutumie Copy na Paste.
07:57 Hebu tujifunze jinsi ya kufanya hivyo.
08:00 Futa neno NAME kutoka MOTHER’S NAME.
08:05 Chagua neno NAME katika FATHER’S NAME.
08:09 Bonyeza kitufe cha kulia cha mouse, chagua Copy.
08:13 Weka mshale kati ya MOTHER’S na kolon.
08:18 Bonyeza kitufe cha kulia cha mouse, chagua Paste.
08:22 Neno NAME limebandikwa automatikali.
08:27 Vitufe vya njia ya mkato: Ctrl+C kwa Copy, Ctrl+V kwa Paste.
08:35 Hii ni muhimu sana kwa maandishi yanayojirudia.
08:40 Hivyo hatuhitaji kuandika tena — tunaweza kunakili na kubandika.
08:47 Writer pia ina kipengele cha Cut kama Copy.
08:52 Hebu tuone mfano.
08:55 Futa neno NAME kutoka MOTHER’S NAME.
09:00 Chagua neno NAME katika FATHER’S NAME.
09:04 Bonyeza kitufe cha kulia, chagua Cut.
09:07 Angalia — neno NAME halipo tena karibu na FATHER’S.
09:13 Hii ina maana limekatwa.
09:17 Weka mshale kati ya MOTHER’S na kolon.
09:21 Bonyeza kitufe cha kulia cha mouse, chagua Paste.
09:26 Neno NAME limebandikwa karibu na MOTHER’S.
09:32 Njia ya mkato ya cut ni Ctrl+X.
09:36 Vivyo hivyo, bandika neno hilo baada ya FATHER’S pia.
09:41 Kipengele cha Cut na Paste ni muhimu kwa kuhamisha maandishi kutoka sehemu moja ya document

hadi nyingine.

09:48 Tofauti pekee kati ya Copy na Cut ni kwamba chaguo la Copy huacha neno la awali mahali pake

lilipochukuliwa, wakati Cut huondoa kabisa kutoka mahali pa awali.

10:03 Hamisha mshale hadi mwisho wa document. Bonyeza Enter mara mbili.
10:09 Sasa hebu tuandike kichwa kipya EDUCATION DETAILS.
10:14 Sasa tutajifunza jinsi ya kubadilisha au kutumia Font name na Font size ya maandishi yoyote.
10:20 Hapo awali, tulichagua UnDotum kama font name.
10:25 Kwa hivyo tunaona UnDotum katika sehemu ya Font name.
10:29 Hebu tutumie Font na Size tofauti kwa kichwa cha EDUCATION DETAILS.
10:34 Basi, kwanza chagua maandishi EDUCATION DETAILS Kisha bonyeza menyu ya Font Name.
10:43 Tafuta Liberation Sans na ubofye juu yake.
10:47 Sehemu ya Font Size inaonyesha 14 kwa sasa.
10:51 Hebu tubadilishe kuwa 11.
10:54 Tunaona kuwa Font size ya maandishi imepungua.
10:58 Sasa tuhamie kwenye Font Color.
11:01 Hakikisha maandishi bado yamechaguliwa.
11:05 Sasa, bonyeza menyu ya Font Color na uchague rangi ya green.
11:11 Kwa hivyo tunaona kuwa heading sasa ina rangi ya green.
11:16 Sasa tutabonyeza kwenye aikoni za Bold, Italic na Underline.
11:22 Tunaweza kutumia mchanganyiko wowote wa mitindo hii ya maandishi kulingana na mahitaji yetu.
11:29 Hifadhi faili yetu kwa kubonyeza Ctrl + S Kisha ifunge kwa kubonyeza aikoni ya X kwenye kona ya juu kulia.
11:36 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. Hebu tueleze kwa kifupi.
11:42 Katika mafunzo haya tulijifunza:
11:45 Kuweka Align maandishi
11:47 Kutumia Bullets na Numbering Kutumia chaguo za Cut, Copy na Paste
11:53 Kutumia chaguo za Bold, Underline na Italic
11:57 Kutumia Font name, Font size, Font color ndani ya Writer
12:02 Kama kazi ya nyumbani: Fungua faili practice.odt
12:07 Washa kipengele cha Bullets and Numbering
12:10 Chagua style yoyote na andika mistari michache ya maandishi
12:14 Chagua baadhi ya maandishi na badilisha Font name kuwa Free Sans
12:18 Weka Font size kuwa 16
12:22 Fanya maandishi kuwa Italic
12:25 Badilisha Font color kuwa red
12:28 Hifadhi na funga faili
12:31 Video katika kiungo kifuatacho inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial Tafadhali pakua na uitazame.
12:38 Tunaendesha workshop tukitumia Spoken Tutorials na tunatoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi.
12:47 Tafadhali tuma maswali yako yenye muda maalum katika jukwaa hili.
12:51 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD Serikali ya India
12:56 Mafunzo haya yalichangiwa awali na DesiCrew Solutions Pvt. Ltd. mnamo 2011
13:02 Mimi ni Maira Magoma pamoja na timu ya Spoken Tutorial kutoka IIT Bombay kwaheri.. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina