LibreOffice-Suite-Writer-6.3/C2/Introduction-to-LibreOffice-Writer/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye spoken tutorial kuhusu Introduction to LibreOffice Writer.
00:07 Katika mafunzo haya, tutajifunza:
00:10 Kuhusu LibreOffice Writer
00:13 Vifaa mbalimbali vya toolbars katika Writer
00:16 Jinsi ya kufungua document mpya na iliyopo
00:20 Kuhifadhi na kufunga document katika Writer
00:24 Kuhifadhi kama document ya MS Word
00:27 Kusafirisha kama document ya PDF
00:30 LibreOffice Writer ni sehemu ya word processor katika LibreOffice Suite.
00:36 Ni sawa na Microsoft Word katika Microsoft Office Suite.
00:41 Ni programu huru na ya chanzo huria.
00:45 Inaweza kuwashared, kubadilishwa na kusambazwa bila vikwazo vyovyote.
00:51 LibreOffice Writer inaweza kufanya kazi kwenye mifumo ya uendeshaji ifuatayo:
00:57 Microsoft Windows 8 au matoleo mapya zaidi
01:01 GNU/Linux OS na
01:04 Mac OSX
01:07 Mafunzo haya yamerekodiwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS toleo la 18.04 na LibreOffice Suite toleo la 6.3.5
01:19 Kwa kawaida, Ubuntu Linux OS ya hivi karibuni huja na LibreOffice Suite tayari imewekwa
01:26 Ili kusakinisha toleo fulani, rejea mfululizo wa LibreOffice Installation kwenye tovuti hii.
01:33 Hebu tujifunze jinsi ya kufungua LibreOffice Writer.
01:37 Katika Ubuntu Linux OS, bonyeza aikoni ya Show applications iliyoko kona ya chini kushoto.
01:45 Katika search bar, andika Writer.
01:49 Kutoka kwenye orodha iliyoonekana, bonyeza aikoni ya Libreoffice Writer.
01:55 Katika Windows OS, bonyeza aikoni ya Start Menu iliyoko kona ya chini kushoto.
02:02 Katika search bar, andika Writer.
02:06 Kutoka kwenye orodha iliyoonekana, bonyeza aikoni ya Libreoffice Writer.
02:11 Hii itafungua document tupu kwenye dirisha kuu la Writer.
02:16 Sasa hebu tujifunze kuhusu sehemu kuu za dirisha la Writer.
02:21 Dirisha la Writer lina toolbars mbalimbali juu yake.
02:25 Nazo ni Title bar, Menu bar, Standard toolbar na Formatting bar.
02:32 Chini yake, tunaona Search bar, Drawing toolbar na Status bar.
02:39 Tunaweza kuruhusu au kutoruhusu toolbars hizi kutoka kwenye menyu.
02:44 Ili kufanya hivyo, nenda kwenye View menu na uchague Toolbars.
02:49 Kutoka kwenye sub menyu, weka au ondoa tiki kwenye toolbars kulingana na upendeleo wako.
02:56 Upande wa kulia, tunaona scroll bar ya wima na sidebar.
03:01 Vyote hivi vina chaguzi zinazotumika mara nyingi.
03:05 Tutajifunza kuhusu hizi kadri mfululizo unavyoendelea.
03:09 Sasa hebu tujifunze jinsi ya kufungua document mpya kwenye Writer.
03:14 Tunaweza kufungua document mpya kwa kubonyeza aikoni ya New kwenye Standard toolbar.
03:20 Vinginevyo, nenda kwenye File menu katika menu bar.
03:25 Kisha bonyeza New kwenye sub menu na uchague chaguo Text Document.
03:32 Document mpya ya Writer inayoitwa Untitled 2 itafunguka.
03:37 Funga document mpya ya Untitled 2 kwa kubonyeza aikoni ya X upande wa juu kulia.
03:44 Sasa, tutaandika maandishi fulani kwenye document ya Untitled 1.
03:49 Andika neno “RESUME”.
03:53 Baada ya kuandika, tunapaswa kuhifadhi document yetu kwa matumizi ya baadaye.
03:58 Ili kuhifadhi faili, bonyeza aikoni ya Save kwenye Standard toolbar.
04:03 Kisanduku cha mazungumzo kitaonekana kwenye skrini.
04:06 Kitatutaka tuingize jina la faili letu kwenye sehemu ya Name.
04:11 Nitaandika jina la faili kama “Resume”.
04:15 Upande wa kushoto, nitachagua Desktop kama eneo la kuhifadhi faili langu.
04:21 Angalia, kuna File type dropdown chini kulia. Bonyeza kwenye hiyo dropdown.
04:29 Inaonyesha orodha ya file types au file extensions tunazoweza kutumia kuhifadhi faili.
04:35 File type ya chaguo msingi kwenye LibreOffice Writer ni ODF Text Document (.odt).
04:42 ODF inamaanisha Open Document Format ambayo ni kiwango huria.
04:48 Pia imekubaliwa na sera ya Serikali ya India kuhusu open standards in e-Governance.
04:55 Nitabonyeza chaguo ODF Text Document ili kuhifadhi faili langu.
05:00 Fanya hivyo kwenye kompyuta yako.
05:02 Bonyeza kitufe cha Save kilicho juu kulia kwenye kisanduku cha mazungumzo.
05:07 Tutarejeshwa nyuma kabisa kwenye dirisha la Writer.
05:12 Angalia mabadiliko kwenye title bar sasa. Imebadilika kuwa Resume.odt
05:18 Mbali na kuhifadhi kwa dot odt, tunaweza pia kuhifadhi kwa dot doc na dot docx.
05:28 Faili zilizo na fomati hizi zinaweza kufunguliwa baadaye kwenye programu ya MS Word.
05:34 Sasa, tutahifadhi faili hili hili kama docx.
05:39 Nenda kwenye File menu kwenye menu bar kisha bonyeza chaguo Save As.
05:45 Kwenye kisanduku cha Save As, bonyeza File type dropdown chini kulia.
05:51 Scroll chini na uchague Word 2007 hyphen 365 (.docx)
05:59 Chagua tena eneo lile lile la kuhifadhi.
06:03 Kisha bonyeza kitufe cha Save kilicho juu kulia kwenye kisanduku.
06:08 Ikiwa tukihifadhi kwa fomati tofauti, kisanduku cha Confirm File Format kitaonekana.
06:15 Weka tiki kwenye chaguo “Ask when not saving in ODF or default format”
06:21 Kisha bonyeza kitufe cha Use Word 2007 hyphen 365 Format
06:28 Tutarudishwa kwenye dirisha la Writer.
06:32 Angalia mabadiliko kwenye title bar. Imebadilika kuwa Resume.docx
06:38 Faili pia inaweza kusafirishwa kama fomati ya PDF.
06:42 Bonyeza aikoni ya Export Directly as PDF kwenye Standard toolbar.
06:47 Andika filename, chagua eneo, na bonyeza kitufe cha Save kilicho juu kulia.
06:53 Nitabonyeza Cancel na kuonyesha njia nyingine ya kuhifadhi document kama PDF.
07:00 Bonyeza File menu kwenye menu bar na uchague sub-menyu ya Export As Kisha bonyeza chaguo la Export as PDF
07:11 Kisanduku cha mazungumzo cha PDF options kitaonekana.
07:15 Katika kisanduku hiki, tutaona mipangilio mbalimbali ya kurekebisha chaguo la PDF.
07:21 Acha mipangilio ya chaguo-msingi kama ilivyo, kisha bonyeza kitufe cha Export cha chini.
07:27 Andika filename, chagua eneo, na bonyeza kitufe cha Save kilichopo juu kulia.
07:34 Faili ya pdf itaundwa katika eneo ulilolichagua.
07:38 Kiendelezi kingine maarufu kinachofunguka katika programu nyingi ni dot rtf, the Rich Text Format.
07:45 Tunaweza pia kuhifadhi faili katika fomati ya dot html, ambayo ni web page format.
07:53 Hii hufanyika kwa njia ile ile tuliyoeleza awali.
07:57 Katika File type dropdown, scroll chini na uchague HTML Document (Writer)(.html).
08:05 Chaguo hili linaipa document kiendelezi cha dot html
08:10 Chagua tena eneo la faili kisha bonyeza aikoni ya Save iliyoko juu kulia ya kisanduku.
08:19 Kisanduku cha Confirm File Format kitaonekana.
08:23 Weka tiki kwenye “Ask when not saving in ODF or default format” option.
08:29 Kisha bonyeza kitufe cha Use HTML Document (Writer) Format.
08:35 Tunaona ya kuwa faili limehifadhiwa na kiendelezi cha dot html.
08:40 Fomati hii hutumika tunapotaka kuonyesha document yetu kama web page.
08:45 Inaweza kufunguliwa katika web browser yoyote.
08:48 Tufunge document hii kwa kubonyeza File menu kisha Close.
08:53 Sasa, tutajifunza jinsi ya kufungua document iliyopo kwenye LibreOffice Writer. Fungua document Resume.odt
09:03 Bonyeza Open File menu upande wa kushoto wa interface wa LibreOffice.
09:09 Kisanduku cha kivinjari cha faili kinafunguka. Nenda mahali ambapo faili limehifadhiwa.
09:16 Sasa kwenye orodha ya majina ya faili, chagua Resume.odt
09:22 Kisha bonyeza kitufe cha Open kilicho juu kulia.
09:27 Faili Resume.odt linafunguka kwenye dirisha la Writer.
09:32 Vivyo hivyo, tunaweza pia kufungua faili zilizo na viendelezi dot doc na dot docx kwenye Writer.
09:39 Sasa tutaona jinsi ya kubadilisha faili na kulihifadhi kwa jina lile lile.
09:45 Kwanza kabisa, tuchague neno RESUME.
09:49 Ili kufanya hivyo, bonyeza mouse button ya kushoto kisha buruta kwenye maandishi. Hii itachagua na kuangazia maandishi.
09:59 Sasa achia mouse button ya kushoto. Maandishi yatabaki yameangaziwa.
10:05 Bonyeza aikoni ya Bold kwenye Formatting bar. Maandishi sasa yamekuwa bold.
10:12 Sasa, tuweke neno RESUME katikati ya ukurasa.
10:17 Ukibadilisha ukubwa wa dirisha la LibreOffice, baadhi ya icons huenda zisionekane.
10:23 Katika hali hiyo, bonyeza aikoni ya mishale miwili mwisho wa toolbars
10:29 Bonyeza aikoni ya Align Center kwenye Formatting bar.
10:34 Tunaona kuwa maandishi yamewekwa katikati ya ukurasa.
10:38 Sasa tuongeze font size ya maandishi.
10:42 Bonyeza mshale chini kwenye sehemu ya Font Size ndani ya Formatting bar.
10:47 Kwenye menyu ya kushuka, tuchague 14. Font size ya maandishi imeongezeka hadi 14.
10:56 Sasa tubadilishe Font ambayo tunatumia.
11:00 Bonyeza mshale chini kwenye sehemu ya Font Name ndani ya Formatting bar.
11:05 Tuchague Undotum kwenye menyu. Font name ya maandishi imebadilika kuwa Undotum.
11:13 Sasa tuhifadhi mabadiliko tuliyoyafanya. kufanya hivyo bonyeza kwa pamoja Ctrl + S.
11:22 Faili limehifadhiwa kwa jina lile lile hata baada ya marekebisho.
11:27 Tufunge document sasa.
11:29 Bonyeza File kwenye menu bar kisha bonyeza chaguo la Close.
11:35 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya ya spoken tutorial. Hebu tufanye muhtasari.
11:41 Katika mafunzo haya, tulijifunza:
11:44 Kuhusu LibreOffice Writer
11:47 Toolbars mbalimbali
11:49 Jinsi ya kufungua document mpya na iliyohifadhiwa
11:53 Kuhifadhi na kufunga document katika Writer
11:57 Kuhifadhi kama document ya MS Word
12:00 Kusafirisha kama document ya PDF
12:03 Kama kazi ya nyumbani: Fungua document mpya kwenye Writer
12:07 Ihifadhi kwa jina practice.odt
12:11 Andika maandishi “This is my first assignment”
12:15 Piga mstari chini ya maandishi hayo.
12:17 Ongeza Font size hadi 16. Hifadhi na funga faili.
12:23 Video inayofuata inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial. Tafadhali ipakue na uitazame.
12:30 Tunaendesha mafunzo tukitumia spoken tutorials na kutoa vyeti.
12:34 Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie.
12:39 Una maswali kwenye Spoken Tutorial hii? Tafadhali tembelea tovuti hii
12:44 Chagua dakika na sekunde ambapo una swali Elezea swali lako kwa kifupi
12:51 Timu ya mradi wa Spoken Tutorial itahakikisha jibu linatolewa
12:55 Utahitajika kujisajili kwenye tovuti hii ili kuuliza maswali.
12:59 Jukwaa la Spoken Tutorial ni kwa maswali maalum ya mafunzo haya.
13:04 Tafadhali usichapishe maswali yasiyohusiana. Hii itasaidia kupunguza mkanganyiko.
13:11 Kwa kuwa na utulivu, tunaweza kutumia mijadala hii kama nyenzo ya kufundishia.
13:16 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India.
13:21 Mafunzo haya yalitolewa awali na DesiCrew Solutions Pvt. Ltd. mwaka 2011.
13:28 Mimi ni Maira Magoma pamoja na timu ya Spoken Tutorial kutoka IIT Bombay kwaheri. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina