LibreOffice-Suite-Calc-6.3/C2/Working-with-Sheets-in-Calc/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye Mafunzo Simulizi ya “Working with Sheets.
00:05 Katika mafunzo haya, tutajifunza:
00:08 Kuingiza na kufuta Rows, Columns, Sheets
00:13 Kubadilisha jina la Sheets na
00:15 Kusogeza Sheets
00:18 Mafunzo haya yameandikwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS toleo 18.04 na LibreOffice Suite toleo 6.3.5
00:32 Hebu tufungue faili letu la Personal Finance Tracker dot ods.
00:37 Faili hili limewekwa kwenye kiungo cha Code files kwenye ukurasa wa mafunzo haya. Tafadhali pakua na lichambue faili hilo.
00:48 Tengeneza nakala, halafu litumie kwa mazoezi.
00:52 Safu wima na mistari vinaweza kuongezwa moja-moja au kwa wingi.
00:58 Kwanza tutajifunza jinsi ya kuongeza row mpya au column mpya kwenye spreadsheet.
01:05 Katika faili letu la Personal Finance Tracker dot ods, bofya kwenye cell C1.
01:12 Cell hii ina maandishi ya “Cost” ndani yake.
01:16 Sasa bofya ikoni ya Row kwenye Standard toolbar.
01:21 Chaguzi nyingi zinazohusiana na mistari zinaonyeshwa kwenye context menu.
01:27 Angalia chaguzi mbili maalum: Insert Rows Above na Insert Rows Below.
01:35 Nitabofya chaguo la Insert Rows Above.
01:40 Mstari mpya umeongezwa juu ya cell C1.
01:45 Sasa bofya ikoni ya Column kwenye Standard toolbar.
01:50 Chaguzi nyingi zinazohusiana na safu wima zinaonyeshwa kwenye context menu.
01:56 Angalia chaguzi mbili maalum: Insert Columns before na Insert Columns after.
02:04 Nitabofya chaguo la Insert Columns Before.
02:09 Safu mpya imeongezwa upande wa kushoto wa cell C1.
02:14 Hebu turudishe mabadiliko haya.
02:17 Mistari na safu zinaweza kuongezwa pia kwa kubofya Sheet menu kwenye menu bar.
02:25 Njia nyingine ya haraka ya kuongeza mstari au safu ni kubofya kulia kwenye cell yoyote.
02:32 Bofya kulia kwenye cell C1 na kisha bofya chaguo la Insert.
02:38 Kisanduku cha mazungumzo cha Insert Cells kinafunguka.
02:42 Hapa chagua kulingana na mahitaji yako kisha bofya kitufe cha Ok.
02:48 Chunguza chaguzi hizi wewe mwenyewe kwa uelewa zaidi.
02:53 Nitaacha hili, na kubofya kitufe cha Cancel kufunga kisanduku cha mazungumzo.
02:58 Sasa, tutajifunza jinsi ya kuongeza rows na columns nyingi kwa wakati mmoja.
03:04 Tuseme tunataka kuongeza columns 4 kabla ya SN ambayo ni cell A1.
03:11 Hivyo, chagua cells A1 hadi D1 kwa kubofya na kuvuta kitufe cha kushoto cha kipanya. cells-4 zote zinachaguliwa.
03:21 Bofya kulia popote kwenye sehemu iliyochaguliwa kisha chagua Insert.
03:26 Kwenye kisanduku cha mazungumzo cha Insert Cells, bofya chaguo la Entire Column.
03:32 Kisha bofya kitufe cha OK kilichopo chini.
03:36 Angalia kuwa columns 4 mpya zimeongezwa kabla ya Serial Number.
03:42 Sasa bofya cell yoyote ya kawaida ili kuondoa uteuzi.
03:46 Kwa njia kama hiyo, tunaweza kuongeza rows nyingi pia. Chunguza hili wewe mwenyewe.
03:54 Sasa tutajifunza jinsi ya kufuta columns moja-moja na (kwa pamoja).
04:00 Chagua column yoyote kwa kubofya herufi ya column juu, kama inavyoonyeshwa.
04:07 Sasa bofya ikoni ya Column kwenye Standard toolbar halafu chagua, chaguo la Delete Columns. Column iliyochaguliwa inafutwa.
04:18 Tuseme tunataka kufuta columns zaidi ya moja kwa wakati mmoja.
04:23 Kwa upande wangu, nataka kufuta hizi columns 3 tulizoongeza sasa hivi.
04:30 Hivyo, chagua columns hizo 3 kwa kubofya herufi za columns juu, kama inavyoonyeshwa.
04:38 Columns zote 3 zinachaguliwa.
04:41 Sasa bofya ikoni ya Column kwenye Standard toolbar halafu chagua…. chaguo la Delete Columns.
04:49 Columns zilizochaguliwa zinafutwa.
04:53 Kwa njia kama hiyo, tunaweza kufuta rows nyingi pia. Chunguza hili wewe mwenyewe.
05:01 Sasa tutajifunza jinsi ya kuongeza na kufuta sheets kwenye Calc.
05:07 Kuna njia kadhaa za kuongeza sheet mpya kwenye Calc.
05:12 Tutajifunza kila moja kwa mfuatano.
05:17 Kule chini kushoto, tunaona kichupo chenye jina Sheet 1.
05:22 Kuna baadhi ya ikoni zilizopo kabla ya kichupo hicho.
05:26 Tukibofya ikoni ya Plus, sheet mpya yenye jina Sheet2 inaongezwa.
05:33 Sheet hii mpya inaongezwa upande wa kulia wa ile iliyopo sasa.
05:38 Tunaweza pia kuongeza sheets kwa kubofya sehemu tupu karibu na vichupo vya Sheet.
05:46 Tukifanya hivyo, kisanduku cha mazungumzo cha Insert Sheet kinafunguka.
05:52 Kwa kutumia kisanduku hiki, tunaweza kuongeza sheet kabla au baada ya ile ya sasa.
05:59 Tunaweza pia kuongeza idadi yoyote ya sheets kwa wakati mmoja.
06:03 Chini ya Position, nitachagua Before the current sheet. Na kwenye Number of sheets, nitaandika 2.
06:12 Kisha bofya kitufe cha OK kilichopo chini.
06:17 Angalia kuwa Sheet 3 na Sheet 4 zimeongezwa kabla ya Sheet 2.
06:24 Njia nyingine ya kuongeza sheets ni kubofya Sheet menu kwenye menu bar. Kisha bofya Insert Sheet.
06:33 Ukifanya hivyo, kisanduku cha mazungumzo cha Insert Sheet kinafunguka.
06:39 Nitaacha hili, na kubofya kitufe cha Cancel kilicho chini.
06:44 Sasa hebu tujifunze jinsi ya kufuta sheets.
06:48 Sheets zinaweza kufutwa moja- moja au kwa makundi.
06:53 Ili kufuta sheet moja, bofya kulia kwenye kichupo cha sheet unayotaka kufuta.
06:59 Halafu chagua chaguo la Delete Sheet.
07:03 Kisanduku cha mazungumzo cha confirmation kinaonekana. Bofya kitufe cha Yes.
07:10 Sheet iliyochaguliwa inafutwa.
07:14 Tunawezaje kufuta sheets zaidi ya moja kwa wakati mmoja?
07:18 Kwa mfano, tuseme tunataka kufuta Sheet 2 na Sheet 3.
07:24 Kwanza bofya kwenye kichupo cha Sheet 2.
07:27 Kisha, ukiwa unashikilia kitufe cha Shift kwenye kibodi, bofya kichupo cha Sheet 3.
07:33 Sasa bofya kulia kwenye mojawapo ya vichupo hivyo na chagua Delete Sheet.
07:40 Kisanduku cha mazungumzo cha confirmation kinaonekana.
07:44 Bofya kitufe cha Yes ili kufuta sheet. Sheets zote mbili zinafutwa.
07:51 Hebu turudishe mabadiliko haya kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl + Z.
07:57 Kwa kawaida, sheets hupewa majina kama Sheet 1, Sheet 2, Sheet 3 na kadhalika.
08:04 Calc ina kipengele cha kubadilisha majina ya sheets kulingana na mahitaji yetu.
08:09 Kwa mfano, hebu tubadilishe jina la Sheet 2 kuwa “Dump.”
08:14 Fanya hivi kwa kubofya mara mbili kwenye kichupo cha Sheet 2.
08:19 Kisanduku cha mazungumzo cha Rename Sheet kinafunguka.
08:23 Kuna kisanduku cha maandishi kilichoandikwa Sheet 2.
08:27 Futa maandishi haya na andika “Dump” kama jina jipya.
08:31 Bofya kitufe cha OK.
08:35 Kichupo cha Sheet 2 sasa kimebadilishwa jina kuwa “Dump.”
08:40 Hebu turudishe mabadiliko haya kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl + Z.
08:46 Tunaweza kupanga upya sheets kwa kubofya kwenye sheet na kuivuta hadi mahali tunapotaka.
08:54 Hifadhi faili kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl+S kwenye kibodi.
09:01 Sasa funga faili kwa kubofya ikoni ya X kwenye kona ya juu kulia.
09:08 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. Hebu tutekeleze muhtasari.
09:13 Katika mafunzo haya, tulijifunza:
09:15 Kuingiza na kufuta Rows, Columns, Sheets
09:21 Kubadilisha majina ya Sheets na kuhamisha Sheets
09:26 Kama kazi ya ziada Fungua faili Spreadsheet hyphen Practice dot ods.
09:32 Chagua na futa safu iliyo na kichwa cha SN.
09:37 Weka data husika katika safu za Name, Department na Salary
09:43 Tazama kiungo cha Code files kwa maelezo zaidi.
09:46 Badilisha jina la sheet kuwa Department-Sheet.
09:51 Hifadhi na funga faili hilo.
09:54 Video katika kiungo kifuatacho inatoa muhtasari wa mradi wa spoken tutorial. Tafadhali ipakue na kuitazama.
10:02 Timu ya Mradi wa Spoken Tutorial huendesha warsha na kutoa vyeti.
10:08 Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie.
10:12 Tafadhali tuma maswali yako ya muda kwenye jukwaa hili.
10:16 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India.
10:23 Mafunzo haya yalitolewa awali na DesiCrew Solutions Pvt. Ltd. mwaka 2011 Mimi ni Hokins Moshi pamoja na timu ya Spoken Tutorial kutoka IIT Bombay, tunahitimisha kwa sasa. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina