LibreOffice-Suite-Calc-6.3/C2/Working-with-Cells-in-Calc/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye Mafunzo Simulizi kuhusu “Working with Cells.”
00:06 Katika mafunzo haya, tutajifunza jinsi ya:
00:09 Kuingiza numbers, text, date na time kwenye spreadsheet
00:15 Kutumia kisanduku cha mazungumzo cha Format Cells
00:19 Vinjari kati ya cells na
00:22 Kuchagua vitu vilivyomo kwenye rows na columns
00:27 Mafunzo haya yameandikwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS toleo 18.04 na LibreOffice Suite toleo 6.3.5
00:41 Kwanza, tutajifunza jinsi ya kuingiza data kwenye cells.
00:46 Tufungue faili letu la Personal Finance Tracker dot ods
00:52 Faili hili limewekwa kwenye kiungo cha Code files kwenye ukurasa huu wa mafunzo.
00:59 Tafadhali pakua na kisha lifungue.
01:03 Tengeneza nakala na uitumie kwa kufanya mazoezi.
01:08 Sasa andika maandishi kwenye cell yoyote iliyo wazi kwa kubofya cell hiyo na kuandika kwa kutumia kibodi. Bonyeza Enter.
01:18 Maandishi huwekwa upande wa kushoto kwa chaguo-msingi.
01:22 Mtu anaweza kubadilisha mpangilio wa maandishi kwa kubofya mojawapo ya ikoni za Alignment kwenye Formatting Bar.
01:30 Hebu turudishe nyuma tulichokiandika.
01:33 Bonyeza vitufe vya: Ctrl+Z kwenye kibodi ili kurudisha nyuma.
01:39 Katika spreadsheet hii, tayari tulikuwa tumeandika vichwa vya column hapo awali.
01:45 Katika Calc, tunaweza kutofautisha vichwa vya habari na data nyingine kwa kuongeza style.
01:53 Ili kufanya hivyo, bofya cell A1. Kisha shikilia kitufe cha kushoto cha kipanya na buruza, kishale hadi cell G1.
02:04 Sasa achilia kitufe cha kipanya.
02:07 Tunaweza kuona kuwa vichwa vyote vya habari vime-angaziwa.
02:16 Tunaweza kuona heading styles mbalimbali. Nitachagua Accent 2.
02:24 Sasa bofya kwenye cell yoyote kwa nasibu ili kuondoa uteuzi wa vichwa vya habari.
02:30 Angalia kuwa sasa vichwa vya habari vina-angaziwa kwa rangi ya kijivu, kama msingi.
02:36 Katika Items column, tutaandika majina ya baadhi ya vitu, moja chini ya jingine. Andika maandishi kama inavyoonyeshwa hapa.
02:47 Ili kuingiza namba kwenye cell, bofya kwenye cell na andika namba. Kisha bonyeza Enter.
02:57 Kumbuka kubonyeza kifungo cha Enter kila baada ya kuingiza data-entry.
03:03 Ili kuingiza namba hasi, andika minus sign kabla yake au iweke ndani ya parentheses.
03:13 Kwa chaguo-msingi, namba hupangwa upande wa kulia na namba hasi huwa na Alama ya Hasi mbele.
03:20 Hebu tufute maandishi haya.
03:23 Chagua cells zote za kufutwa kwa kushikilia kitufe cha Shift na kubonyeza kila cell. Sasa bonyeza kifungo cha Delete kwenye kibodi.
03:36 Katika SN column, tunataka nambari za mfuatano wa kila kipengee kimoja chini ya kingine.
03:43 Kwa hivyo bofya kwenye cell A2 na uandike nambari kama 1, 2, 3 moja chini ya jingine.
03:53 Kumbuka kubonyeza kifungo cha Enter baada ya kuandika kila nambari.
03:58 Ili kujaza nambari za mfuatano ki-otomatiki kwenye cells zinazofuata, bofya kwenye cell A4. Rudia Kusoma hii
04:06 Bofya kwenye black box ndogo inayonekana kwenye kona ya chini kulia ya cell.
04:13 Buruza hadi cell A7 na uachilie kitufe cha kipanya.
04:19 Tunaona kuwa cells A5, A6 na A7 zimejazwa ki-otomatiki na nambari za mfuatano zinazofuata.
04:28 Sasa tutaingiza gharama ya kila kipengee chini ya kichwa cha Cost.
04:35 Bofya kwenye cell C3 na uandike matumizi ya House rent kama Rupees 6,000 point 00
04:45 Sasa, je tunafanyaje ikiwa tunataka namba hiyo iwe na alama ya Rupee?
04:51 Futa thamani iliyoandikwa kwenye cell C3 kwa kubonyeza pamoja vitufe vya: Ctrl na Z.
04:59 Bonyeza kitufe cha kulia kwenye cell C3 na uchague chaguo la Format Cells.
04:59 Bonyeza kitufe cha kulia kwenye cell C3 na uchague chaguo la Format Cells.
05:05 Hii itafungua kisanduku cha mazungumzo cha Format Cells.
05:09 Kichupo cha kwanza ni Numbers. Bofya juu yake ikiwa haijachaguliwa tayari.
05:16 Hapa tunaweza kuona chaguo mbali-mbali chini ya Category.
05:21 Number, Percent, Currency, Date, Time na vingine vingi.
05:29 Tutachagua Currency.
05:31 Currency symbols mbalimbali kutoka kote duniani zinaonyeshwa kwenye orodha ya Format.
05:39 Kwa chaguo-msingi, INR Rupee English (India) imechaguliwa kwenye menyu kunjuzi ya Format.
05:46 Ikiwa sivyo, bofya kwenye menyu kunjuzi na ichague kutoka kwenye orodha iliyoonyeshwa.
05:51 Chini ya Format, menyu kunjuzi , tunaweza kuona sampuli za thamani kulingana na chaguo letu.
05:58 Tunaona: minus Rupee 1,234 decimal zero zero imeshachaguliwa kwa INR Rupees English (India).
06:10 Tunaweza kuona format tuliyochagua kwenye eneo dogo la onyesho upande wa kulia.
06:16 Chini ya sehemu ya Category, kuna sehemu nyingine inayoitwa Options.
06:22 Kupitia hii, tunaweza kuongeza au kupunguza idadi ya Decimal places na Leading zeroes.
06:30 Tunapofanya hivyo, tunaona mabadiliko katika thamani ya sampuli na eneo la onyesho.
06:37 Tutahifadhi thamani za chaguo-msingi.
06:41 Ili kuongeza koma kati ya thamani, weka tiki kwenye kisanduku cha Thousands separator.
06:48 Mtu pia anaweza kubadilisha font style kwa kubonyeza kichupo cha Font.
06:54 Ina chaguzi mbali-mbali kwa: Family, Style na Size.
06:59 Chunguza Font Effects na vichupo vingine ili kujifunza zaidi kwa kujitegemea.
07:07 Tutajifunza kuhusu chaguo kwenye kichupo cha Alignment katika somo lijalo.
07:13 Hebu tubonyeze kitufe cha OK kilicho kona ya chini kulia.
07:18 Sasa andika 6,000 kwenye cell C3 na bonyeza Enter.
07:24 Angalia kuwa namba 6000 inaonyeshwa kama Rupees 6,000 ikiwa na 2 decimal places.
07:34 Sasa, tuchague cells C4 hadi C7 kwa kushikilia kitufe cha Shift na kubofya cells.
07:43 Shikilia kitufe cha CTRL na uchague pia cell G2.
07:48 Angalia kuwa cells zote zilizochaguliwa zime-angaziwa.
07:52 Bofya kulia, kwenye mojawapo ya cells zilizo-angaziwa na uchague Format Cells.
07:59 Chagua chaguo zile- zile kama hapo awali.
08:03 Bofya kitufe cha OK kilicho chini kulia.
08:07 Bofya cell yoyote kwenye spreadsheet ili kuondoa uteuzi wa cells.
08:13 Kisha, andika kiasi cha kila kipengee kimoja chini ya kingine, kama inavyoonyeshwa hapa.
08:22 Chini ya kichwa cha safu “Account”, tutaandika mshahara wa mwezi kama 30,000.
08:29 Tuendelee kwenye safu ya Date. Bofya kwenye cell F2.
08:36 Ili kuingiza tarehe kwenye Calc, chagua cell na uandike date kama inavyoonyeshwa.
08:42 Hapa nimetumia forward slash kati ya vipengele vya tarehe.
08:47 Tunaweza pia kutenganisha vipengele vya tarehe kwa kutumia hyphen.
08:52 Au tumia maandishi kama: 05 June 2020.
08:59 Calc, hutambua aina mbalimbali za fomati za tarehe.
09:02 Pia tunaweza kubadilisha fomati ya tarehe kulingana na mahitaji yetu.
09:09 Ili kufanya hivyo, bofya kulia kwenye cell na uchague chaguo la Format Cells.
09:16 Bofya kwenye kichupo cha Numbers. Katika sehemu ya Category, chagua Date.
09:22 Chini ya sehemu ya Format, chagua fomati ya tarehe kulingana na mahitaji yako. Nitachagua 31 slash 12 slash 1999.
09:36 Angalia maonyesho katika sehemu ya onyesho la awali (preview area).
09:40 Kulingana na chaguo letu, Format code ita-sasishwa. Kwa upande wangu ni DD, MM na YYYY.
09:52 Baada ya kusa-sisha muundo, bofya kitufe cha OK kilicho chini kulia.
09:58 Sasa, hebu tujaribu chaguzi za saa.
10:02 Bofya kwenye cell yoyote ya bahati nasibu. Andika time kama inavyoonyeshwa.
10:08 Nimetenganisha vipengele vya time kwa kutumia colons.
10:12 Ili kubinafsisha zaidi fomati ya time, bofya kulia kwenye cell husika na uchague Format Cells.
10:20 Bofya kwenye kichupo cha Numbers juu.
10:23 Chini ya Category, chagua Time na fomati unayopendelea chini ya Format. Nitachagua 13 colon 37 colon 46.
10:35 Angalia maonyesho katika sehemu ya (onyesho la awali).
10:39 Pia, Format code inaonyeshwa chini kama HH colon MM colon SS.
10:48 Unaweza kubadilisha Format code moja kwa moja pia.
10:51 Bofya kitufe cha OK kilicho chini kulia.
10:56 Hebu tufute maandishi yote ya time kutoka kwenye spreadsheet.
11:01 Sasa tutajifunza jinsi ya kusogeza ndani ya spreadsheet kutoka cell hadi cell.
11:07 Tunaweza kufikia cell fulani kwa kubofya tu kwenye cell hiyo kwa kutumia cursor.
11:13 Hii hubadilisha mkazo /kwenda kwenye new cell.
11:17 Njia hii ni ya manufaa zaidi iwapo cells mbili ziko mbali.
11:22 Njia nyingine ya kufikia cell fulani ni kwa kutumia (rejeleo la cell)
11:28 Bofya kwenye Name Box iliyoko juu upande wa kushoto, chini ya Font Name.
11:35 Futa rejeleo la cell lililopo na andika rejeleo la cell unayotaka kufikia.
11:42 Nitataja B4 na kubofya Enter.
11:47 Tazama kuwa cell B4 inang'aa.
11:52 Tunaweza pia kusogeza kati ya cells kwa kutumia kibodi.
11:57 Bofya kitufe cha Tab ili kwenda kwenye cell inayofuata katika mstari.
12:02 Shift + Tab ili kurudi kwenye cell ya awali katika mstari.
12:07 Bofya Enter ili kwenda kwenye cell inayofuata katika safu.
12:12 Shift pamoja na Enter; ili kurudi kwenye cell ya awali katika safu.
12:17 Sasa, tutajifunza jinsi ya kuchagua anuwai ya cells zinazofuatana kwa kutumia cursor.
12:24 Kwanza, bofya kwenye cell na shikilia kitufe cha mouse cha kushoto.
12:29 Vuta cursor kwenye sheet.
12:32 Mara tu; cells zinazohitajika zime-angazwa, achia kitufe cha mouse cha kushoto.
12:38 Tunaona kuwa cells zilizochaguliwa zime-angazwa.
12:42 Sasa, tutajifunza jinsi ya kuchagua columns au rows kadhaa zinazofuatana.
12:50 Bofya kwenye column au row ya kwanza unayotaka kuchagua.
12:55 Sasa shikilia kitufe cha Shift na bofya kwenye column au row ya mwisho unayotaka kuchagua. Tunaona kuwa cells zilizochaguliwa zime-angazwa.
13:08 Hebu tujifunze kuchagua columns au rows kadhaa ambazo si za mfuatano.
13:14 Bofya kwenye column au row ya kwanza unayotaka kuchagua.
13:19 Shikilia kitufe cha Control.
13:22 Sasa bofya kwenye columns au rows zote zinazofuata unazotaka kuchagua.
13:29 Tunaona kuwa cells zilizochaguliwa zime-angazwa.
13:34 Hifadhi faili kwa kubofya Ctrl na S kwenye kibodi.
13:40 Sasa funga faili kwa kubofya ikoni ya X kwenye kona ya juu kulia.
13:46 Hii inatufikisha mwishoni mwa tutorial hii, hebu tufupishe.
13:52 Katika tutorial hii, tulijifunza: Kuandika numbers, text, date na time katika Calc.
14:01 Kutumia kisanduku cha mazungumzo cha Format Cells.
14:05 Kusogeza kati ya cells na
14:09 Kuchagua vitu katika rows na columns.
14:13 Kama kazi ya nyumbani: Fungua Spreadsheet hyphen Practice dot ods.
14:19 Chini ya SN andika nambari za serial kutoka 1 hadi 5 moja baada ya nyingine na Align Center.
14:27 Ongeza vichwa vya column Date na Time na text format ile ile.
14:33 Andika baadhi ya thamani katika columns hizo.
14:37 Tumia chaguzi za kisanduku cha mazungumzo cha Format Cells ili kubinafsisha cells.
14:43 Taja kiungo cha Code files kwa ajili ya data.
14:47 Hifadhi na funga faili.
14:50 Video kwenye kiungo kilichofuata inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial. Tafadhali pakua na tazama.
14:58 Tunafanya warsha kwa kutumia Spoken Tutorials na tunatoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie.
15:08 Tafadhali tuma maswali yako ya wakati, katika jukwaa hili.
15:13 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India.
15:19 Mafunzo haya yalitolewa awali na DesiCrew Solutions Pvt. Ltd. mwaka 2011 Mimi ni Hokins Moshi pamoja na timu ya Spoken Tutorial kutoka IIT Bombay, tunahitimisha kwa sasa. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina