Introduction-to-Computers/C2/Printer-Connection/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye mafunzo ya sauti kuhusu chaguzi za Google Drive.
00:06 Katika mafunzo haya, tutajifunza kuhusu chaguzi zinazopatikana katika Google Drive kama:
00:12 Kuunda waraka, laha ya data na wasilisho
00:17 Kupakia faili na folda na
00:20 chaguzi za kushiriki.
00:22 Kwa mafunzo haya, utahitaji muunganisho wa intaneti unaofanya kazi na kivinjari chochote.
00:29 Nitatumia kivinjari cha wavuti cha Firefox.
00:33 Kabla ya kuanza, unapaswa kuwa na uelewa wa msingi wa Gmail.
00:38 Kama huna, tafadhali tazama mafunzo ya Gmail kwenye tovuti yetu.
00:43 Tuanze.
00:45 Fungua kivinjari na ingia kwenye akaunti yako ya gmail.
00:49 Tayari nimefanya hivyo.
00:51 Juu kulia, tunaweza kuona ikoni ya gridi karibu na jina letu.
00:06 Unapohamisha kipanya juu yake, maandishi ya msaada yanasema Programu. Bofya hapa.
01:02 Hii itaonyesha programu kadhaa za Google kama: Google Plus, Search, YouTube, Maps, PlayStore, News, Mail, Drive, Calendar na nk.
01:18 Ukibofya yoyote kati ya hizi, utapelekwa kwenye programu husika ya Google.
01:24 Pia unaweza kupanga upya orodha hii kulingana na upendeleo wako kwa kuburuza ikoni ya programu hadi nafasi nyingine.
01:32 Katika mafunzo haya, tutajifunza hasa kuhusu Drive.
01:35 Hivyo, hebu tubofye Drive.
01:39 Hii itafungua ukurasa wa Google Drive kwenye kichupo kipya.
01:43 Juu ya ukurasa, tunaweza kuona sehemu ya utafutaji.
01:47 Kushoto, kuna menyu kadhaa.
01:51 Na juu kulia, kuna baadhi ya ikoni.
01:55 Katikati ya ukurasa, tunaweza kuona faili mbili.
01:59 Faili ya kwanza ilishirikiwa nasi wakati wa kuunda akaunti na timu ya Google.
02:05 Faili ya pili ni ile tuliyopakia sisi wenyewe hapo awali.
02:10 Sasa, hebu tuangalie menyu zilizopo upande wa kushoto.
02:14 Tuna menyu zifuatazo: New, My Drive, Shared with me, Google Photos, Recent, Starred na Trash.
02:27 Kwa chaguo-msingi, menyu ya My Drive itakuwa imechaguliwa na maudhui yake yataonyeshwa katikati.
02:34 Faili na folda zote zitaonekana katika eneo la kati.
02:38 Hivyo tunaweza kuona faili za PDF na ZIP tulizopakia kwenye somo la awali, hapa.
02:47 Faili ambazo tumeunda au kupakia zitawekwa chini ya My Drive.
02:53 Menyu inayofuata ni Shared with me. Hebu nibofye hapa.
02:58 Kama mtu atanishirikisha faili au waraka, itaonekana chini ya menyu hii.
03:03 Kwa sasa, hakuna mtu aliyenishirikisha faili yoyote. Kwa hivyo hii ni tupu.
03:09 Hivi karibuni, Google imeunda kiungo kifupi cha kufikia Google Photos ndani ya Drive.
03:15 Tutaruka chaguo hili katika mafunzo haya.
03:19 Menyu ya Recent itaonyesha orodha ya faili au waraka zilizofunguliwa hivi karibuni.
03:25 Itaonyesha yaliyomo kwenye My Drive na Shared with me.
03:30 Hivyo, hapa tunaweza kuona faili za pdf na zip kwa sababu tulizifungua hapo awali.
03:37 Starred – Ikiwa tumemwekea faili au waraka alama ya Umuhimu, faili hiyo itaonekana chini ya menyu hii.
03:45 Hebu turudi kwenye menyu ya My Drive na bonyeza-kulia faili yetu ya pdf.
03:51 Sasa, chagua chaguo la Add Star.
03:55 Kisha, bofya menyu ya Starred. Hapa ndipo faili letu lilipo.
04:00 Hebu nitengeneze nakala ya faili hili.
04:03 Hivyo, mara nyingine tena, bonyeza-kulia faili hilo na chagua- chaguo la Make a copy.
04:10 Sasa tunazo faili mbili.
04:13 Hebu tufute moja wapo. Chagua faili na bonyeza kitufe cha "Delete" kwenye kibodi.
04:20 Faili au waraka zilizofutwa zitaonyeshwa chini ya menyu ya Trash.
04:25 Kufuta huku ni kwa muda tu.
04:28 Tunaweza kufuta kabisa faili zote kutoka kwenye menyu ya Trash kwa kuchagua chaguo la Empty Trash.
04:36 Faili zote kwenye menyu ya Trash zitafutwa kabisa kutoka kwenye seva ya Google baada ya siku 30.
04:44 Sasa, hebu tujifunze jinsi ya kuunda na kupakia faili na folda.
04:49 Kuna njia nne za kufanya hivi: Njia ya kwanza ni kubofya kitufe chekundu cha New kilicho upande wa kushoto.
04:56 Njia ya pili: Bonyeza-kulia chaguo la My Drive.
05:00 Sasa, turudi kwenye My Drive. Katika chaguo la My Drive, tunaweza kubonyeza-kulia eneo la kati.
05:09 Mwisho, bofya menyu ya kunjuzi ya My Drive iliyo juu.
05:14 Hebu tuanze kuchunguza chaguo la New. Bofya kitufe cha New.
05:19 Kitaonyesha baadhi ya chaguzi kama: Folder, File Upload, Google Docs, Sheets, Slides na nk.
05:28 Tutaangalia kila chaguo, moja baada ya jingine.
05:31 Tunaweza kuunda folda kwa kutumia chaguo la Folder.
05:34 Bofya hapo. Mara moja dirisha linauliza jina.
05:40 Hebu tulipe jina folda hilo kuwa: “Spoken Tutorial” kisha bofya Create.
05:48 Kwa chaguo-msingi, folda hili litaonekana chini ya My Drive.
05:52 Tunaweza kuliona hapa, katika eneo la kati.
05:56 Folda husaidia kupanga faili zetu vizuri zaidi.
06:00 Hivyo, tunaweza kuunda folda tofauti. Kwa mfano – binafsi, kazi, n.k.
06:07 Ili kupakia faili yoyote – kwanza bofya kitufe cha New, kisha chagua File Upload.
06:13 Hii itafungua dirisha la kuchagua faili.
06:16 Vinjari na uchague faili unalotaka kupakia.
06:19 Nitachagua faili la “xyz.odt” kutoka Desktop na kubofya kitufe cha Open.
06:26 Chini kulia, tunaweza kuona maendeleo ya upakiaji.
06:30 Hii inaweza kuchukua muda kutegemea ukubwa wa faili na kasi ya intaneti.
06:35 Mara tu inapokamilika, faili lilopakiwa litaonekana katika eneo la kati.
06:41 Sasa, funga dirisha la maendeleo lililopo chini.
06:45 Kwa njia ile ile, tunaweza kupakia folda kwenye Drive tukitumia chaguo la Folder Upload.
06:52 Kipengele hiki huenda kikapatikana kwenye vivinjari maalum pekee. Kwa mfano: Google Chrome.
06:59 Tunawezaje kuhamisha faili lilopakiwa kwenda kwenye folda letu la Spoken Tutorial?
07:04 Rahisi tu – buruza faili na uliweke kwenye folda, kama hivi.
07:09 Sasa, upande wa kushoto, angalia kwa makini chaguo la My Drive.
07:14 Angalia pembetatu ndogo upande wa kushoto wa maandishi hayo.
07:18 Ukibofya hapo, utaona folda ndogo zilizo ndani ya My Drive.
07:22 Angalia, hapa kuna folda letu “Spoken Tutorial” na ndani yake kuna faili 'xyz.odt'.
07:31 Kwa kazi zetu za kila siku, tunatumia waraka, laha za data na wasilisho.
07:36 Je, inawezekana kuunda na kudhibiti hizi ndani ya Drive?
07:39 Ndiyo, inawezekana. Katika Google Drive, tunaweza kuunda – waraka, laha za data na wasilisho sawa kama kwenye Office Suite yoyote.
07:50 Hivyo, tunayo Google Docs kwa ajili ya kuunda waraka,
07:54 Google Sheets kwa ajili ya laha za data,
07:57 na Google Slides kwa ajili ya kuunda wasilisho.
08:01 Kwa madhumuni ya maonyesho, nitaonyesha tu jinsi ya kuunda waraka kwa kutumia Google Docs.
08:08 Ili kuunda waraka mpya, bofya kitufe cha New na uchague chaguo la Google Docs.
08:14 Hii itafungua waraka tupu katika kichupo kipya.
08:19 Tunaweza kuona kuwa menyu na chaguzi za upangaji wa maandishi ni sawa na zile za Office Suite nyingine.
08:26 Juu kabisa, angalia kuwa waraka imepewa jina la “Untitled document”.
08:31 Hili ni jina linaloweza kuhaririwa. Ili kubadilisha jina, bofya kwenye maandishi hayo.
08:38 Dirisha la “Rename document” linafunguka.
08:41 Hapa, tunaweza kuandika jina linalofaa kwa waraka yetu.
08:46 Nitaandika “My first google doc” kisha kubofya OK.
08:53 Angalia mabadiliko ya jina hapo juu.
08:56 Kisha, hebu niandike maandishi fulani hapa, tuseme – “Welcome to Google Docs”.
09:02 Mabadiliko yoyote, kuongezwa au kufutwa, yatahifadhiwa moja kwa moja.
09:08 Tafuta ujumbe unaosema “All changes saved in Drive”, karibu na menyu ya "Help", juu.
09:14 Ukibofya hapo, utaona Revision History upande wa kulia.
09:19 Inaonyesha tarehe na muda wa mwisho wa marekebisho pamoja na nani aliyefanya mabadiliko hayo.
09:26 Kwa sasa, waraka hii haijashirikiwa na mtu yeyote.
09:30 Hivyo tunaweza kuona mtumiaji mmoja tu “Rebecca Raymond” na tarehe ni ya leo pamoja na saa.
09:37 Ikiwa waraka hii ya Google Doc itashirikiwa na watu wengi, Revision History itaonyesha mabadiliko yote yaliyofanywa na kila mtumiaji kwa rangi tofauti.
09:48 Tutaangalia kipengele hiki baadaye kwenye mafunzo haya.
09:53 Funga dirisha la Revision History.
09:56 Hebu nifunge kichupo hiki. Waraka wa Google Doc utahifadhiwa moja kwa moja.
10:02 Sasa tumerudi kwenye My Drive na tunaweza kuona faili letu hapa.
10:07 Bofya mara mbili kufungua tena faili.
10:10 Sasa, nitakili-na kubandika mstari: “Welcome to Google Docs” mara mbili kisha nifunge kichupo.
10:17 Bofya mara mbili kwenye faili tena, ili kulifungua.
10:20 Kisha, nakili na ubandike tena mstari “Welcome to Google Docs” mara moja.
10:26 Sasa, bofya kwenye Revision History. Tunaweza kuona marekebisho yote ya faili pamoja na mihuri ya tarehe na muda na taarifa za mtumiaji.
10:36 Ikiwa marekebisho mengi hayaonekani, bofya kitufe cha Show detailed revisions kilichopo chini.
10:44 Marekebisho yamepangwa kwa mpangilio wa wakati, marekebisho mapya yakiwa juu kabisa.
10:50 Bofya kila toleo ili kuelewa jinsi kipengele hiki kinavyofanya kazi.
10:55 Sasa hebu tushirikishe waraka huu na watumiaji wengine wawili.
10:59 Kwa kufanya hivyo, bofya kitufe cha Share kilichopo juu kulia.
11:03 Dirisha la “Share with others” linaonekana.
11:07 Katika kisanduku cha People, tunapaswa kuandika barua pepe za watu, tunaotaka kushirikiana nao kwenye waraka huu.
11:15 Hivyo, nitaandika: 0808iambecky@gmail.com.
11:23 Kumbuka kuwa kipengele cha kujaza ki-otomatiki kinapatikana hapa kwa barua pepe ambazo tumezitumia awali.
11:31 Kuna njia tatu za kushiriki waraka na watumiaji wengine.
11:36 Bofya kitufe hapa ili kuona njia hizi tatu: Can edit, Can comment, Can view.
11:44 Chaguo la Can edit linampa mtumiaji ruhusa ya kufanya mabadiliko kwenye waraka.
11:51 Can comment linampa ruhusa ya kupendekeza mabadiliko pekee.
11:56 Chaguo la "Can view" linawapa watumiaji wengine ruhusa ya kutazama tu.
12:00 Hawawezi kufanya au kupendekeza mabadiliko yoyote.
12:04 Hebu tumpe 0808iambecky ruhusa ya Can edit.
12:09 Nitamuongeza pia: stlibreoffice@gmail.com.
12:16 Kumbuka kutumia koma kutenganisha barua pepe mbili au zaidi.
12:21 Mara tu tunapoandika barua pepe, dirisha hili hubadilika.
12:25 Tutaona sehemu ya kuandika ujumbe, “Add a note”.
12:28 Ikiwa tunataka kutuma maelezo kuhusu waraka huu kwa watumiaji wengine, tunaweza kuyaandika hapa.
12:36 Nitaandika: “Tafadhali angalia waraka hii kwa madhumuni ya majaribio. Tafadhali fanya marekebisho au toa mapendekezo kulingana na ruhusa uliyopewa. Asante, Ray.Becky.”
12:47 Mwisho, bofya kitufe cha Send ili kukamilisha mchakato wa kushirikiana.
12:52 Hii itatuma arafa kwa njia ya barua pepe pamoja na ujumbe wetu na kiungo cha waraka, kwa watumiaji wengine.
12:59 Bofya tena kitufe cha Share.
13:02 Kisha bofya Advanced.
13:05 Sasa, kwa mtumiaji stlibreoffice, tutabadilisha ruhusa yake kuwa Can comment.
13:12 Mwisho, bofya kitufe cha Save changes kisha Done.
13:18 Kisha funga waraka huu.
13:21 Sasa, fikiria kwamba watumiaji wote wawili wamefanya baadhi ya mabadiliko kwenye waraka huu waliopewa.
13:27 Tunapofungua tena waraka baada ya muda, tunaweza kuona mabadiliko yaliyofanywa na watumiaji tulioshirikiana nao.
13:34 Kwa kuwa stlibreoffice@gmail.com alipewa ruhusa ya kupendekeza tu, tunaweza kuona mapendekezo yaliyotolewa na mtumiaji huyu.
13:43 Elekeza kipanya kwenye kisanduku cha pendekezo, juu ya alama ya tiki na alama ya X.
13:49 Alama ya tiki inamaanisha Accept suggestion na alama ya X inamaanisha Reject suggestion.
13:56 Hebu nikubali pendekezo moja na kukataa lingine.
14:02 Tunaweza kuona maoni kutoka kwa 0808iambecky hapa.
14:07 Na hapa, tunaweza kuona kitufe cha Resolve.
14:11 Watumiaji walio na ruhusa ya Can edit, wanaweza kujibu maoni hayo kwa kubofya maandishi ya maoni.
14:18 Ili kuondoa mjadala wa maoni, bofya Resolve.
14:22 Hatuwezi kuona mabadiliko yoyote yaliyofanywa na 0808iambecky kwenye waraka.
14:29 Kumbuka, mtumiaji huyu alikuwa na ruhusa ya kuhariri waraka.
14:34 Basi, tunawezaje kujua ni mabadiliko gani aliyofanya?
14:39 Kwa hiyo, tunaweza kuangalia Revision History yetu.
14:43 Ili kuifungua, bofya File kisha See revision history.
14:50 Tunaweza kuona kuwa 0808iambecky alifanya baadhi ya mabadiliko, na haya yanaonekana kwa rangi tofauti.
14:58 Pia tunaweza kuona mapendekezo yaliyotolewa na stlibreoffice@gmail.com kwa rangi tofauti.
15:05 Na bila shaka, kama mmiliki, tunaweza kuona kazi yetu wenyewe kwa rangi tofauti pia.
15:11 Hebu tufunge dirisha la Revision History sasa.
15:14 Kuna njia nyingine ya kushiriki waraka. Bofya kitufe cha Share.
15:20 Katika dirisha la Share with others, upande wa juu kulia, tunaweza kuona maandishi Get shareable link. Bofya hapa.
15:29 Inaonyesha “Anyone with the link can view”.
15:32 Hii itatengeneza kiungo kwa waraka huu.
15:35 Sasa tunaweza kutuma kiungo hiki kwa anwani yoyote ya barua pepe, ambayo ina maana yeyote mwenye kiungo hiki anaweza kuona waraka.
15:44 Kwa hayo, tunafika mwisho wa mafunzo haya.
15:47 Tufanye muhtasari.
15:49 Katika mafunzo haya, tulijifunza:
15:51 Kufikia Google Drive, Kuunda na Kupakia faili, Kuunda waraka kwa kutumia Google Docs na Kutumia chaguzi za kushirikiana.
16:00 Video katika kiungo kilicho hapa chini inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial. Tafadhali pakua na uitazame.
16:07 Tunaendesha warsha na kutoa vyeti kwa wale wanaofaulu mitihani yetu ya mtandaoni. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie.
16:16 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na NME-ICT, MHRD, Serikali ya India. Maelezo zaidi kuhusu dhamira hii yanapatikana kwenye kiungo hiki
16:27 waraka huu umetolewa na Praveen, na mimi ni Hokins Moshi kutoka IIT Bombay, ninasema kwaheri. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina