Introduction-to-Computers/C2/Compose-Options-for-Email/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye Mafunzo Simulizi kuhusu, Utangulizi wa Gmail.
00:06 Katika mafunzo haya, tutajifunza jinsi ya-
00:09 Kuunda akaunti mpya ya Google
00:12 Ingia kwenye Gmail ukitumia akaunti ya google
00:16 Andika barua pepe
00:18 Tuma barua pepe
00:20 Tazama barua pepe na
00:22 Ondoka kwenye Gmail
00:24 Pia, tutajifunza kuhusu baadhi ya sanduku la barua muhimu kama Inbox.
00:30 Kwa mafunzo haya, utahitaji - muunganisho wa Intaneti unaofanya kazi.
00:35 na kivinjari cha wavuti.
00:37 Kwa maonyesho, nitakuwa nikitumia kivinjari cha wavuti cha Firefox.
00:42 Karibuni, Google imeweka akaunti moja kwa bidhaa zote za Google kama:
00:48 Gmail YouTube
00:50 Google Play Google Docs/Drive
00:53 Google Calendar.... nk.
00:57 Kwa hivyo, kwa ingizo hilo hilo, unaweza kuendesha chochote kati ya hivi.
01:02 Tuanze kwa kuunda akaunti mpya ya google.
01:06 Fungua kivinjari chako cha wavuti na uandike:http colon slash slash gmail dot com (http://gmail.com).
01:16 Itatufikisha kwenye ukurusa ambapo tunaweza kuona chaguzi mbili upande wa juu kulia-
01:22 Fungua akaunti na Ingia.
01:25 Ikiwa hii ni mara ya kwanza ukurasa huu unafikiwa kutoka kwenye mashine yako, utaonekana hivi.
01:32 Ikiwa page hii tayari imetumika kutoka kwa kifaa chako, basi ukurasa utakuwa hivi.
01:39 Hivyo, utaona masanduku ya kuingiza jina la mtumiaji la email yako na nywila.
01:46 Na kitufe kikubwa kinachosema Sign In.
01:50 Chini ya hii, utaona kiungo kinachosema Fungua akaunti.
01:55 Sawa, hebu tubofye kwenye kiungo cha Fungua akaunti.
01:59 Sasa tuko kwenye ukurasa wa kuunda Akaunti ya Google.
02:03 Tunaona form upande wa kulia, ambapo tunahitaji kujaza maelezo yetu ya akaunti na binafsi.
02:11 Hebu tuingize majina yetu ya kwanza na ya mwisho kwenye masanduku ya maandishi husika.
02:17 Nitaweka jina langu kama Rebecca Raymond.
02:23 Kisha, tunapaswa kuchagua jina la mtumiaji.
02:27 Jina la mtumiaji lazima liwe la kipekee na linaweza kujumuisha herufi au mchanganyiko wa herufi na nambari.
02:37 hebu tuweke jina la mtumiaji kama: "becky0808."
02:43 Ikiwa jina la mtumiaji tayari limetumika, tutaona ujumbe ufuatao:
02:49 "Someone already has that user name, Try another"
02:54 Google pia itapendekeza baadhi ya jina la mtumiaji kulingana na majina yetu ya kwanza na ya mwisho tuliyoyatoa.
03:01 Tunaweza kutoa jina la mtumiaji yoyote tunalopenda na kuangalia upatikanaji wake.
03:07 Sasa, nitatoa jina la mtumiaji kama: ray.becky.0808.
03:18 Hapa inapita, ambapo inaonyesha kuwa jina hili la mtumiaji linapatikana
03:24 Sasa, tunahitaji kuunda nywila kwa ajili ya akaunti hii.
03:30 Sanduku la maelezo upande wa kushoto linatufahamisha ni kwa ukubwa gani, nywila inapaswa kuwa.
03:36 Andika nywila inayofaa kwa chaguo lako.
03:41 Kisha andika tena nywila ili kuthibitisha.
03:44 Baada ya hili, inafuata tarehe ya kuzaliwa.
03:48 Chagua mwezi kutoka kwenye orodha kunjuzi.
03:51 Kisha andika siku na mwaka katika masanduku ya maandishi husika.
03:57 Sasa chagua jinsia yako.
04:00 Ninachagua "Female."
04:03 Sehemu inayofuata ni Namba ya Simu.
04:06 Nitaachana na hii kwa sasa.
04:08 Baada ya hii, kuna kisanduku cha maandishi kinachouliza anwani yetu ya barua pepe ya sasa
04:14 Ikiwa una anwani mbadala ya barua pepe, mbali na ile unayounda sasa, iandike hapa.
04:21 Ikiwa huna, acha waza.
04:23 Hebu tujaze maelezo yaliyobaki sasa.
04:26 Sehemu inayofuata “Thibitisha kuwa wewe si roboti” ina hatua 2 za uthibitishaji.
04:32 Uthibitishaji kwa simu
04:34 Uthibitishaji kwa chemsha bongo.
04:36 Tunaweza kuendelea na mojawapo ya chaguo hizi 2
04:40 Nitachagua, chemsha bongo.
04:43 Andika maandishi/namba zilizoonyeshwa kwenye picha, kwenye Type the text text-box.
04:49 Nchi ulipo inaonyeshwa, kwa chaguo-msingi, kwenye orodha kunjuzi ya Eneo.
04:55 Niko nchini India. Hivyo, India inaonyeshwa kwenye orodha kunjuzi ya Eneo.
05:02 Mwisho, bofya kwenye kisanduku cha: "I agree to the Google Terms of service and Privacy Policy, ili kuki-tiki.
05:10 Mara maelezo yote yamejazwa kwenye form, tunahitaji kubofya kitufe cha Next Step.
05:17 Hivi sasa, hatutafanya hivyo.
05:20 Hebu tuone tutakachofanya, ikiwa tutachagua “Uthibitishaji kwa simu.”
05:25 Bofya kwenye kisanduku cha “Skip this verification (Phone Verification may be required)”.
05:32 Chagua eneo kama India
05:35 Kisha bofya kwenye kisanduku cha "I agree to the Google Terms and Privacy Policy."
05:41 Na mwishowe, bofya kwenye Next Step.
05:45 Itahama kwenye ukurasa wa Uthibitishaji kwa simu.
05:50 Chagua bendera ya nchi kutoka kwenye orodha kunjuzi, mimi na chagua India.
05:55 Ingiza namba yako ya simu kwenye kisanduku kilichopo.
06:00 Chagua, chaguo la "Text message (SMS). Kwa kawaida, itachaguliwa kwa kudhibiti.
06:07 Kisha bofya kitufe cha Continue.
06:10 Utapokea Ujumbe kwenye simu yako.
06:13 Sasa itakupeleka kwenye sehemu inayofuata ya uthibitishaji.
06:17 Andika msimbo wa uthibitishaji ulio tumiwa kutoka kwa Google kupitia Ujumbe, kwenye kisanduku kilichopo
06:24 Bofya kwenye Continue.
06:27 Sasa tuko kwenye ukurasa wa : 'Create your public Google+ profile'.
06:32 Hapa, unaweza kuona jina lako.
06:35 Chini ya hili, kuna chaguo la “Add a photo.”
06:39 Unaweza kubofya hapa kuongeza picha kwa Google profile yako.
06:44 Pia kuna kitufe kinachoitwa “Create your profile.”
06:48 Kwa sasa, nitaachana na hatua hizi.
06:51 Badala yake, nitabofya kwenye kitufe cha "No Thanks kuendelea kwenye akaunti yangu ya email.
06:58 Sasa, tuko kwenye ukurasa wa welcome.
07:02 Na kwa upande wangu, inasema “Welcome, Rebecca.”
07:06 Anuani yangu mpya ya email: ray.becky.0808@gmail.com pia inaonyeshwa.
07:16 Sasa, bofya kwenye kitufe cha Continue to Gmail.
07:22 Itaanza kupakia akaunti yako ya barua pepe.
07:24 Kulingana na kasi ya mtandao wako, hii inaweza kuchukua muda.
07:28 Ikiwa mtandao wetu unakasi ndogo, tunaweza kubofya kwenye Load basic HTML.
07:33 Inapatikana upande wa kulia chini.
07:37 Itapakia gmail bila muonekano wa picha.
07:41 Baadhi ya masanduku ya taarifa yatajitokeza kwenye skrini.
07:46 Soma au chunguza zaidi kwa kubofya kitufe cha Next kisha funga.
07:53 Huu ndio muonekano mkuu au Mtazamo wa kawaida wa akaunti yako ya Gmail.
07:58 Eneo la katikati la skrini ndipo tunaweza kuona barua pepe zetu, zote.
08:04 Angalia, kuna vichupo vitatu hapa. Tutajifunza kuhusu hivyo kwa kina, katika mafunzo yajayo.
08:12 Upande wa kushoto, tunaweza kuona baadhi ya vipengee vya menyu vilivyoandikwa.
08:16 Inbox, Starred, Sent Mail, Drafts, na More; ni baadhi ya sanduku la barua muhimu za Gmai
08:29 Kwa kudhibiti, Inbox inachaguliwa na maudhui yake yanaonyeshwa kwenye eneo la kuonyesha.
08:36 Angalia kuwa Inbox ina namba 3 ndani ya mabano.
08:41 Hii inaonyesha idadi ya barua pepe mpya ambazo umepokea.
08:46 Tunapounda akaunti mpya ya google, tunapata baadhi ya barua pepe kutoka kwa Gmail Team.
8:52 Unaweza kuzisoma kwa maelezo zaidi juu ya jinsi ya kutumia vipengele vya Gmail.
8:58 Sasa, hebu tujifunze jinsi ya kuandika email.
9:02 Bofya kwenye kitufe cha COMPOSE upande wa kushoto.
9:06 Dirisha lenye jina la New Message litafunguka.
9:10 Lina sehemu nne.
9:13 To – ni mahali ambapo tunandika anwani ya barua pepe ya mtu ambaye tunataka kumtumia barua pepe.
9:21 Hapa, nitandika email-id ile ile tuliyounda sasa hivi, yaani: ray.becky.0808@gmail.com
9:35 Hii inamaanisha kuwa ninatuma barua pepe kwangu mwenyewe.
9:39 Sehemu inayofuata ni Subject.
9:42 Hapa, tunaweza kuandika mstari mfupi wa kichwa cha habari cha barua pepe.
9:46 Tuseme “Welcome mail.”
9:50 Ifuatayo ni eneo la maudhui.
9:53 Hapa tunapaswa kuandika ujumbe wetu tunaotaka kutuma.
9:57 Tutaandika, “Greetings to all from the Spoken Tutorial Project.”
10:03 Katika sehemu ya mwisho, kuna kitufe cha buluu kinachosema Send.
10:08 Bofya kitufe hicho kutuma barua pepe.
10:11 Tazama idadi ya barua pepe kwenye Inbox sasa ni 4.
10:16 Ili kusoma barua pepe maalum, bonyeza tu juu yake.
10:20 Hii hapa ni barua pepe niliyotuma kwangu mwenyewe.
10:23 Hebu tuangalie.
10:26 Bofya kwenye mshale wa Show details.
10:29 Hapa ni anwani za barua pepe za mtumaji na mpokeaji.
10:34 Hapa ni tarehe na wakati ambapo barua pepe ilitumwa.
10:39 Hapa ni mstari wa kichwa cha habari cha barua pepe.
10:43 Na maudhui yako, yapo hapa.
10:47 Sasa, tazama kwamba idadi ya barua pepe zisizosomwa kwenye Inbox ni 3.
10:54 Sasa, hebu tujifunze jinsi ya sign out kutoka Gmail.
10:58 Juu kulia, utaona email-id yako.
11:03 Ikiwa ulipakia picha wakati wa kuunda akaunti, basi utaona hiyo hapa badala yake.
11:08 Bofya juu yake.
11:10 Hapa kuna kitufe cha Sign Out. Bofya tu,.. ili sign out.
11:17 Umetoka, kwa mafanikio kutoka Gmail.
11:21 Hii inaashiria kumalizika kwa mafunzo haya.
11:25 Hebu tufupishe. Tulijifunza kuhusu-
11:28 Kuunda akaunti mpya ya google
11:31 Ingia kwenye gmail ukitumia akaunti ya google
11:34 Andika email
11:36 Tuma email, angalia email na
11:39 logout kutoka gmail.
11:41 Video kwenye kiungo kilichotolewa inafupisha mradi wa Spoken Tutorial.
11:45 Tafadhali pakua na itazame.
11:49 Tunafanya warsha na kutoa vyeti kwa wale wanaofaulu mitihani yetu ya mtandao.
11:55 Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuma barua pepe kwetu.
11:58 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na NMEICT, MHRD, Serikali ya India.
12:05 Maelezo zaidi kuhusu misheni hii yanapatikana kwenye kiungo hiki.
12:10 Script hii imetolewa na Praveen.
12:12 Ni mimi Hokins Moshi, kutoka Spoken Tutorial, nakuaga. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina