LibreOffice-Suite-Writer-6.3/C3/Header,-Footer-and-Notes/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye spoken tutorial kuhusu Header, Footer and Notes.
00:07 Katika mafunzo haya, tutajifunza jinsi ya:
00:11 Kuingiza Header
00:13 Kuingiza Footer
00:15 Kuondoa Header na Footer kutoka kwenye ukurasa wa kwanza na
00:19 Kuingiza Footnote na Endnote kwenye document
00:24 Mafunzo haya yameandikwa kwa kutumia

Ubuntu Linux OS toleo 18.04 na LibreOffice Suite toleo 6.3.5

00:37 Fungua faili Newsletter.odt tulilounda awali.
00:43 Faili hili limewekwa kwako kupitia kiungo cha Code files kwenye ukurasa huu.
00:49 Tafadhali pakua na lifutungue faili hilo.
00:52 Tengeneza copy kisha uitumie kwa mazoezi.
00:57 Kwanza tutajifunza jinsi ya kuongeza Footer kwenye document.
01:02 Bonyeza menyu ya Insert kwenye menu bar kisha uchague chaguo la Header and Footer.
01:08 Weka tiki kwenye chaguo la Use header/footer menu ikiwa halijachaguliwa.
01:15 Scroll ukurasa na bonyeza chini ya maandishi ili kuonyesha alama ya Footer.
01:21 Alama ya Footer inaonekana kwenye document yetu.
01:25 Bonyeza alama ya Plus iliyo karibu na neno Footer.
01:29 Tunaona Footer imeongezwa chini ya ukurasa.
01:34 Njia nyingine ya kuongeza Footer kwenye document ni kubonyeza Insert menu kwenye menu bar.
01:41 Nenda kwenye chaguo la Header and Footer.
01:44 Chagua menyu ndogo ya Footer kisha uchague chaguo la Default style.
01:50 Kwa njia zote, mshale uko kwenye eneo la footer.
01:54 Ili kuongeza nambari ya kurasa kwenye footer, bonyeza mshale chini wa Footer Default style.
02:00 Kisha uchague chaguo la Insert Page Number.
02:04 Mara moja, tunaona nambari 1 inaonekana kwenye footer.
02:09 Ili kutoa styles tofauti kwa nambari ya ukurasa, bonyeza mara mbili nambari 1.
02:15 Kisanduku cha Edit Fields kitafunguka.
02:18 Kuna sehemu 3 tofauti ndani ya Edit fields:

Type, Select na Format

02:26 Kwenye sehemu ya Format, tunaona formats nyingi kama a b c kwa herufi ndogo, A B C kwa herufi kubwa na nyinginezo
02:38 Nitachagua format 1st 2nd 3rd kisha nibonyeze kitufe cha OK kilicho chini.
02:46 Angalia kuwa format ya nambari ya ukurasa 1 hubadilika kutoka 1 hadi 1st.
02:52 Sasa tutajifunza jinsi ya kuingiza Header kwenye document.
02:57 Scroll juu na bonyeza sehemu ya juu ya maandishi kwenye document.
03:03 Alama ya Header inaonekana kwenye document yetu.
03:06 Ikiwa haionekani, bonyeza alama ya plus karibu na neno Header.
03:11 Header itaongezwa juu ya ukurasa.
03:15 Sasa tuweke tarehe kwenye Header.
03:19 Ili kufanya hivyo, nenda kwenye aikoni ya Insert field iliyo kwenye Standard toolbar.
03:25 Sasa bonyeza mshale wa chini kisha uchague chaguo la Date kwenye orodha.
03:31 Tarehe ya sasa inaonekana kwenye eneo la Header.
03:35 Unaweza kuibadilisha kuwa tarehe yoyote unayotaka, ikiwa unataka.
03:40 Kubadilisha format ya tarehe, bonyeza mara mbili kwenye tarehe.
03:44 Hapa tuchague format kama 31. Dec. 1999 kisha bonyeza kitufe cha OK.
03:53 Format ya tarehe sasa imebadilika kulingana na tulivyochagua.
03:57 Ikiwa mpangilio wa maandishi umebadilika, tafadhali urekebishe kwa kubonyeza Backspace.
04:04 Rudia hadi maandishi yawe kwenye ukurasa wa 1 na column 2.
04:09 Kisha bonyeza Enter mara kadhaa ili kupanga maandishi chini ya banner.
04:15 Sasa bonyeza aikoni ya Toggle print preview kwenye Standard toolbar.
04:21 Tarehe inaonekana juu ya kila ukurasa na nambari chini.
04:27 Kumbuka header na footer vitaonekana kwenye kila ukurasa wa document.
04:33 Bonyeza kitufe cha Close Preview ili kufunga onyesho
04:38 Sasa tujifunze jinsi ya kuongeza margin na shadow style kwenye document
04:44 Bonyeza aikoni ya Page iliyo kwenye Sidebar deck
04:49 Chini ya chaguo la Styles, bonyeza aikoni ya More Options au gear.
04:55 Kisanduku cha mazungumzo cha Page Style: Default Style kitafunguka.
04:59 Kuna tabs nyingi zinazoweza kutumika kurekebisha page style kulingana na matakwa yetu.
05:05 Bonyeza kwenye tab ya Footer.
05:07 Weka tiki kwenye chaguo la Footer on, kama halijachaguliwa tayari.
05:13 Sasa weka nafasi ya left margin kuwa 1.00 cm kwa kubonyeza alama ya plus mara kadhaa.
05:21 Ili kuongeza border au shadow kwenye footer, bonyeza kitufe cha More.
05:26 Kisanduku cha mazungumzo cha Border/Background kitafunguka.
05:29 Bonyeza tab ya Borders ikiwa haijachaguliwa.
05:33 Kwenye sehemu ya Shadow Style, tunaona chaguzi mbalimbali za kuweka kivuli.
05:39 Chagua aikoni ya Cast shadow to bottom right.
05:43 Chini ya chaguo la Color, Gray ni rangi chaguo-msingi ya kivuli.
05:48 Kuchagua rangi nyingine, bonyeza mshale wa chini.
05:52 Unaweza kuchagua rangi yoyote unayopenda kutoka kwenye kisanduku cha Color palette. Nitachagua blue.
06:00 Acha mipangilio mingine yote kama ilivyo kwenye kisanduku cha Border/Background.
06:06 Kisha bonyeza kitufe cha OK.
06:09 Kwenye kisanduku cha Page Style: Default Style, bonyeza kitufe cha Apply kisha OK.
06:17 Funga Sidebar deck.
06:19 Scroll chini ili kuona shadow effect iliyoongezwa kwenye Footer.
06:25 Sasa tutajifunza jinsi ya kuondoa Header na Footer kutoka kwenye ukurasa maalum.
06:31 Tuanze kwa kuondoa Header kwenye ukurasa wa kwanza wa document.
06:35 Kwa hiyo, weka mshale sehemu yoyote kwenye ukurasa wa kwanza wa document.
06:40 Kwenye Sidebar deck, chagua aikoni ya Styles.
06:44 Styles panel hufunguka.
06:47 Bonyeza aikoni ya Page Styles na uchague First Page kwenye orodha.
06:55 Bonyeza mara mbili chaguo la First Page
06:59 Funga Sidebar deck.
07:02 Angalia kuwa Header na Footer zimeondolewa tu kwenye ukurasa wa kwanza.
07:09 Huenda ukahitaji tena kurekebisha mpangilio wa maandishi kama ilivyoonyeshwa.
07:19 Sasa tujifunze kuhusu Footnotes na Endnotes katika Writer.
07:24 Footnotes huonekana chini ya ukurasa uliotajwa.
07:29 Endnotes huwekwa mwishoni mwa document au chapter.
07:35 Anchor ya note huwekwa kwenye nafasi ya sasa ya mshale.
07:40 Anchor huwasaidia watumiaji kufikia sehemu fulani moja kwa moja.
07:46 Unaweza kuchagua kati ya automatic numbering au custom symbol kwa ajili ya notes.
07:52 Tuone jinsi ya kuongeza Footnote kwenye neno ndani ya document.
07:57 Chagua neno Apache License kwenye aya ya pili, safu ya 1 ya ukurasa 1.
08:04 Bonyeza aikoni ya Insert Footnote kwenye Standard toolbar.
08:09 Tunaweza pia kuongeza Footnote kwenye document kupitia menyu ya Insert.
08:15 Kisha bonyeza Footnote and Endnote na uchague chaguo la Footnote.
08:21 Kwa njia zote, Footnote itaongezwa kwenye document na character yake ikiwa 1.
08:27 Hebu tuandike maandishi ya Footnote yetu.
08:30 Andika “open source software license”.
08:34 Kwa njia hiyo hiyo, tuongeze footnote nyingine kwenye document.
08:39 Chagua neno copyleft kutoka safu ya pili ya ukurasa wa 1.
08:44 Bonyeza aikoni ya Insert Footnote kwenye Standard toolbar.
08:48 Footnote nyingine itaongezwa chini ya safu ya pili ya ukurasa.
08:54 Andika maandishi ya footnote kama “permissive license”.
09:00 Bonyeza character 1 ya Footnote chini ya safu ya 1.
09:05 Tutaelekezwa kwenye neno Apache License kwenye document.
09:10 Angalia character 1 karibu na neno Apache License.
09:15 Hii ndiyo anchor ya Footnote iliyowekwa
09:19 Elekeza mshale polepole juu ya anchor hii.
09:23 Mshale hubadilika kuwa kidole cha kuashiria.
09:27 Sasa bonyeza hapo.
09:29 Tutaelekezwa mara moja chini ya ukurasa kwenye Footnote iliyoandikwa.
09:35 Chaguo la Character hutumika kuchagua character au symbol ya Footnote ya sasa.
09:42 Hebu nionyeshe jinsi ya kubadilisha character ya Footnote 1.
09:47 Scroll juu na weka mshale kati ya neno License na footnote anchor 1.
09:54 Kisha bonyeza kulia na uchague Footnote or Endnote.
10:00 Kisanduku cha Edit Footnote/Endnote kitafunguka.
10:04 Numbering ni aina ya nambari tunayotaka kutumia kwa Footnotes na Endnotes.
10:10 Chaguo la “Automatic” linapanga nambari moja kwa moja kwa Footnotes au Endnotes.
10:16 Bonyeza kitufe cha Choose karibu na sehemu ya Character.
10:20 Chagua asterisk kisha bonyeza kitufe cha OK.
10:25 Bonyeza OK kufunga kisanduku cha Edit.
10:29 Character ya footnote 1 sasa imebadilishwa kuwa asterisk symbol.
10:34 Bonyeza kwenye anchor.
10:37 Footnote 1 sasa inaonekana kama asterisk symbol.
10:41 Tunaweza pia kuona footnote ya pili imekuwa 1 ya kawaida.
10:47 Sasa tubadilishe character ya Footnote 1 kuwa numerical tena.
10:53 Scroll juu na weka mshale kati ya neno License na footnote anchor asterisk.
11:00 Bonyeza kulia na uchague Footnote or Endnote.
11:05 Kisanduku cha Edit Footnote/Endnote kitafunguka.
11:09 Chini ya Numbering, chagua Automatic kisha bonyeza OK.
11:16 Tunaona asterisk symbol imebadilika tena kuwa numerical.
11:21 Scroll chini na angalia footnotes ili kuona mabadiliko.
11:26 Sasa tujifunze jinsi ya kuangazia footnotes.
11:29 Bonyeza maandishi ya footnote yoyote
11:32 Tazama menyu kunjuzi ya formatting upande wa juu kushoto, inasema Footnote.
11:38 Bonyeza mshale wa kushuka.
11:41 Bonyeza mshale kando ya Footnote kisha uchague Edit Style.
11:48 Kisanduku cha Paragraph Style: Footnote kitafunguka.
11:52 Bonyeza tab ya Highlighting, kisha Color.
11:56 Kwenye rangi, chagua rangi ya kuangazia. Nitachagua njano.
12:02 Bonyeza kitufe cha Apply kisha OK chini.
12:08 Tazama footnotes na uone rangi ya kuangazia.
12:12 Sasa nitaonyesha jinsi ya kuongeza endnote kwenye document
12:18 Chagua neno Mozilla Public License kwenye aya ya 2, safu ya 1 ya ukurasa wa 1.
12:26 Bonyeza aikoni ya Insert Endnote kwenye Standard toolbar.
12:31 Endnote itaongezwa mwishoni mwa document, kwenye ukurasa mpya
12:36 Kama document ina sura, basi endnotes huonekana mwisho wa kila sura.
12:42 Andika maandishi haya kwenye endnote – “an open source/free software license”
12:49 Tunaweza kubadilisha Roman numerals chaguomsingi kuwa style nyingine.
12:54 Ili kufanya hivyo, bonyeza menyu ya Tools kisha chagua Footnote and Endnotes.
13:01 Kisanduku cha Footnote/Endnote settings kitafunguka.
13:05 Kwenye tab ya Endnotes, tunaona sehemu ya Auto Numbering.
13:10 Kwa kutumia chaguo hili, tunaweza kubadilisha Numbering style tunayopendelea.
13:15 Unaweza kuchunguza zaidi hii wewe mwenyewe.
13:19 Funga kisanduku kwa kubonyeza aikoni ya X.
13:23 Sasa tuhifadhi mabadiliko yote na tufunge faili.
13:28 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. Hebu tufanye muhtasari.
13:33 Katika mafunzo haya, tumejifunza jinsi ya:
13:37 Kuingiza Header, kuingiza Footer
13:41 Kuondoa Header na Footer kutoka kwenye ukurasa wa kwanza
13:45 Kuingiza Footnote na Endnote kwenye document
13:49 Kama kazi ya nyumbani Fungua faili practice.odt
13:54 Ongeza Header na Footer kwenye document
13:58 Andika jina lako kwenye Header
14:01 Ongeza Page Count kwenye Footer
14:04 Ongeza Header na Footer kwenye document
14:08 Video ifuatayo inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial Tafadhali ipakue na uiangalie.
14:15 Tunaendesha workshop kwa kutumia spoken tutorials na kutoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi.
14:24 Tuma maswali yako na wakati kwenye jukwaa hili.
14:28 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India.
14:33 Mafunzo haya yalitolewa awali na DesiCrew Solutions Pvt. Ltd. mwaka 2011.
14:39 Mimi ni Maira Magoma pamoja na timu ya Spoken Tutorial kutoka IIT Bombay kwaheri. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina