Introduction-to-Computers/C2/Getting-to-know-computers/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Jump to: navigation, search


Time Narration
00:01 Karibu kwenye Mafunzo ya simulizi Kuifahamu Kompyuta.
00:06 Katika mafunzo haya, tutajifunza kuhusu...
00:09 vipengele mbalimbali vya kompyuta.
00:11 Tutajifunza kuunganisha vipengele mbalimbali.
00:15 Kwa ujumla, kuna aina 2 za kompyuta -
00:18 Kompyuta ya Mezani au binafsi na kompyuta mpakato.
00:23 Siku hizi, Kompyuta kibao au tabs, ni maarufu sana
00:31 Kazi za kompyuta -
00:33 Kompyuta hufanya kazi kuu tano bila kujali ukubwa wake:
00:40 Hupokea data au maagizo kwa njia ya ingizo.
00:45 Huchakata data kama inavyotakiwa na mtumiaji.
00:50 Huhifadhi data.
00:52 Hutoa matokeo katika mfumo wa pato.
00:56 Hudhibiti shughuli zote ndani ya kompyuta.
01:01 Mpangilio wa kimsingi wa kompyuta ni kama unavyoonyeshwa kwenye mchoro huu wa vizuizi
01:08 Kitengo cha Ingizo, Kitengo cha Usindikaji Mkuu,
01:11 Kitengo cha Pato.
01:14 Kitengo cha Ingizo husaidia...
01:16 kuingiza data na programu kwenye mfumo wa kompyuta kwa njia iliyopangwa.
01:23 Kibodi, kipanya, kamera na skana ni baadhi ya vifaa vya ingizo.
01:31 Kitengo cha Usindikaji Mkuu
01:33 hufanya shughuli kama hesabu na mantiki na
01:38 huhifadhi data na maagizo.
01:41 Kwa kawaida, Kitengo cha Usindikaji Mkuu au CPU kinaonekana kama hiki.
01:48 Ina bandari nyingi mbele na nyuma ya kitengo.
01:53 Tutajifunza kuhusu hizo hivi punde
01:57 Huchukua data na maagizo, huichakata na kutoa pato au matokeo.
02:05 Kazi ya kufanya shughuli inaitwa usindikaji.
02:11 Pato huhifadhiwa pamoja na data na maagizo kwenye kitengo cha hifadhi.
02:18 Kitengo kinachosaidia mchakato wa kutoa matokeo kutoka kwa data, ni kitengo cha pato.
02:26 Kichunguzi na printa ni baadhi ya vifaa vya pato.
02:33 Kwa kawaida, kompyuta ya mezani ina vipengele 4 kuu:
02:38 Kichunguzi, CPU
02:40 Kibodi na Kipanya.
02:43 Kamera, printa au skana pia inaweza kuunganishwa kwenye kompyuta.
02:50 Hiki ni kichunguzi au skrini ya kompyuta kama tunavyoiita.
02:55 Inaonekana kama skrini ya televisheni.
02:57 Ni kitengo cha kuonyesha picha cha kompyuta.
03:02 Inaonyesha kiolesura cha mtumiaji cha kompyuta.
03:05 Mtu anaweza kufungua programu mbalimbali na kuingiliana na kompyuta kwa kutumia kibodi na kipanya.
03:13 Kibodi imeundwa kuingiza maandishi, herufi na amri zingine kwenye kompyuta.
03:21 Hiki ni kipanya cha kompyuta.
03:24 Kwa kawaida, ina vifungo 2 vinavyoweza kubofya na kitufe cha kusogeza katikati.
03:31 Kubonyeza kitufe cha kushoto cha kipanya, huamilisha vitendo vingi.
03:35 Kubonyeza kitufe cha kulia cha kipanya, huamilisha vitendo visivyo vya kawaida kama njia za mkato.
03:43 Gurudumu la kipanya linatumika kusogeza juu na chini kwa kukizungusha kitufe cha kusogeza.
03:49 Kipanya cha kompyuta ni njia mbadala ya kuingiliana na kompyuta badala ya kibodi.
03:57 Sasa, hebu tuangalie sehemu mbalimbali za CPU.
04:02 Kuna kitufe maarufu mbele ya CPU ambacho ni swichi ya kuwasha.
04:08 Ili kuwasha kompyuta, mtu anahitaji kubonyeza swichi hii.
04:14 Kuna kitufe cha kuweka upya pia ambacho kinatusaidia kuwasha upya kompyuta, ikiwa inahitajika.
04:21 Pia, upande wa mbele, utaona bandari 2 au zaidi za USB na kisoma-mwandishi cha DVD/CD-ROM.
04:30 Bandari za USB hutumiwa kuunganisha viendeshi vya kalamu kwenye kompyuta.
04:35 Na kisoma-mwandishi cha DVD/CD-ROM hutumiwa kusoma au kuandika CD au DVD.
04:43 Sasa hebu tuangalie nyuma ya kompyuta.
04:48 Bandari zilizo nyuma, hutumiwa kuunganisha CPU na vifaa vingine vya kompyuta.
04:55 Hii inafanywa kwa kutumia nyaya.
04:58 Kuna vipengele vingi ndani ya 'CPU'.
05:02 Kompyuta ikiwa IMEWASHWA, vipengele hivi vyote hufanya kazi na kutoa joto.
05:08 hokin: RUDIA KUREKODI Feni zilizoko nyuma hutoa mtiririko wa hewa unaohitajika kupooza vipengele
05:14 Vinginevyo, kupasha moto kupita kiasi kunaweza kusababisha uharibifu kwa 'CPU', mara nyingi kusababisha upotezaji wa data.
05:21 Hii ni feni ya kupoza kesi.
05:23 Inaweka halijoto ya CPU kuwa ya kawaida na kuzuia kupasha moto kupita kiasi.
05:30 Kitengo cha Ugavi wa Nguvu, kinachoitwa pia PSU, hutoa nguvu kwa kompyuta.
05:37 Sasa, hebu tujifunze jinsi ya kuunganisha vipengele mbalimbali kwenye CPU.
05:42 Weka vipengele vyote kwenye meza, kama inavyoonyeshwa.
05:46 Weka nyaya zote kwenye meza, kama inavyoonyeshwa.
05:51 Kwanza, hebu tuunganishe kichunguzi kwenye CPU.
05:55 Unganisha kebo ya umeme kwenye kichunguzi kama inavyoonyeshwa.
06:00 Sasa, unganisha ncha nyingine kwenye soketi ya usambazaji wa umeme.
06:04 Hii ni kebo ya umeme ya CPU.
06:08 Unganisha kwenye CPU kama inavyoonyeshwa.
06:11 Kisha, unganisha kwenye soketi ya usambazaji wa umeme.
06:14 Ifuatayo, unganisha kebo ya kibodi kwenye CPU kama inavyoonyeshwa.
06:19 Bandari ya kibodi kwa kawaida ni ya rangi "zambarau".
06:23 Unaweza kuunganisha kipanya kwenye bandari ambayo ni ya rangi "kijani".
06:28 Vinginevyo, unaweza kuunganisha kibodi na kipanya cha USB kwenye bandari yoyote ya USB.
06:35 Bandari zilizosalia za USB zinaweza kutumika kuunganisha kiendeshi cha kalamu, diski kuu n.k.
06:42 Hii ni kebo ya LAN.
06:44 na hii ni bandari ya LAN.
06:46 Ni muunganisho wa waya unaoruhusu kompyuta kuunganishwa kwenye mtandao.
06:52 Ncha nyingine ya kebo ya LAN imeunganishwa kwenye modemu au kipanga njia cha wi-fi.
06:58 Utajifunza kuhusu kusanidi miunganisho ya wi-fi katika mafunzo mengine.
07:03 Taa ya LED itapepesa wakati bandari ya LAN inafanya kazi na inapokea shughuli.
07:10 Unaweza kugundua kuwa kuna bandari zingine za serial kwenye CPU.
07:15 Hizi hutumiwa kuunganisha PDA, modemu au vifaa vingine vya serial.
07:21 Pia utagundua kuwa kuna bandari zingine sambamba kwenye CPU.
07:25 Hizi hutumiwa kuunganisha vifaa kama printa, skana n.k.
07:31 Sasa, hebu tuangalie jeki za sauti.
07:34 Bandari iliyo katika "pinki" hutumiwa kuunganisha maikrofoni.
07:38 Bandari iliyo katika "bluu" ni ya kuunganisha laini ya kuingiza, kwa mfano- kutoka kwa redio au kicheza tepi.
07:45 Bandari iliyo katika "kijani" ni ya kuunganisha vipokea sauti/spika au laini ya kutoa.
07:51 Sasa kwa kuwa tumeunganisha vifaa vyetu vyote, hebu tuwashe kompyuta.
07:57 Kwanza kabisa, washa vitufe vya usambazaji wa umeme vya kichunguzi na CPU.
08:03 Sasa, bonyeza kitufe cha KUWASHA kwenye kichunguzi.
08:07 Na kisha bonyeza swichi ya KUWASHA, mbele ya CPU.
08:12 Kwa kawaida, utaona mfuatano wa maneno kwenye skrini nyeusi kompyuta yako inapowashwa kwa mara ya kwanza.
08:18 Hii ni mfumo wa BIOS unaoonyesha taarifa kuhusu
08:22 kitengo cha usindikaji mkuu cha kompyuta,
08:25 taarifa kuhusu kumbukumbu kiasi gani kompyuta ina,
08:28 na taarifa kuhusu viendeshi vya diski kuu na viendeshi vya diski tepetevu.
08:33 BIOS ni programu ambayo huipa CPU maagizo yake ya kwanza kompyuta inapowashwa.
08:41 Mchakato mzima wa kupakia mfumo endeshi unaitwa kuwasha kompyuta.
08:48 Vipimo vyote vinavyohitajika vikikamilika, utaona kiolesura cha mfumo endeshi.
08:54 Ikiwa wewe ni mtumiaji wa Ubuntu Linux, utaona skrini hii.
08:58 Na ikiwa wewe ni mtumiaji wa Windows, utaona skrini hii.
09:02 Sasa, hebu tuangalie kwa ufupi kompyuta mpakato.
09:06 Kompyuta mpakato ni kompyuta zinazobebeka na zilizoshikana.
09:09 Kompyuta mpakato ni ndogo na nyepesi vya kutosha kuwekwa kwenye mapaja ya mtu wakati inatumika.
09:16 Kwa hivyo, inaitwa 'kompyuta mpakato'
09:18 Ina vipengele vingi sawa na kompyuta ya mezani ikijumuisha-
09:23 onyesho, kibodi,
09:25 kigusa ambacho ni kifaa cha kuashiria na kusogeza,
09:29 msomaji-mwandishi wa CD/DVD na
09:32 maikrofoni na spika zilizojengwa kwenye kitengo kimoja.
09:36 Pia ina bandari ya LAN na bandari za USB.
09:40 Kuna bandari ya video ambayo mtu anaweza kuunganisha projekta kwenye kompyuta ndogo.
09:46 Jeki za sauti zinatambulika kwa urahisi kwa aikoni husika za maikrofoni na vipokea sauti.
09:53 Hii ni feni ya kupoza iliyojengwa ndani ya kompyuta mapakato.
09:57 Hii husaidia kuzuia kompyuta ndogo kupata joto kupita kiasi.
10:01 Kompyuta ndogo huendeshwa na umeme kupitia adapta ya AC na ina betri inayoweza kuchajiwa.
10:09 Kwa hivyo, inabebeka na inaweza kutumika mbali na chanzo cha umeme.
10:16 Hebu tufanye muhtasari. Katika mafunzo haya, tumejifunza:
10:20 kuhusu vipengele mbalimbali vya kompyuta ya mezani na kompyuta ndogo
10:23 na jinsi ya kuunganisha vipengele mbalimbali vya kompyuta ya mezani.
10:28 Tazama video inayopatikana kwenye kiungo kifuatacho
10:31 Ni muhtasari wa mradi wa Mafunzo ya Mazungumzo.
10:34 Ikiwa huna kipimo data kizuri, unaweza kuipakua na kuitazama.
10:37 Timu ya mradi wa Spoken Tutorial: hufanya warsha kwa kutumia mafunzo ya mazungumzo.
10:42 Hutoa vyeti kwa wale wanaofaulu mtihani wa mtandaoni.
10:46 Kwa maelezo zaidi, tafadhali andika kwa: contact@spoken-tutorial.org
10:52 Mradi wa Spoken Tutorial ni sehemu ya mradi wa "Talk to a Teacher",
10:56 unaoungwa mkono na Misheni ya Kitaifa ya Elimu kupitia ICT, MHRD, Serikali ya India.
11:01 Maelezo zaidi kuhusu misheni hii yanapatikana kwenye kiungo kifuatacho.
11:06 Uhuishaji na uundaji wa 3D kwa mafunzo haya umefanywa na Arthi.
11:11 Ni mimi Hokins Moshi kutoka mradi wa Spoken Tutorial, IIT Bombay, Ninahitimisha.
11:16 Asante kwa kujiunga.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina