LibreOffice-Suite-Writer-6.3/C2/Viewing-and-printing-a-document-in-Writer/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Revision as of 22:28, 14 May 2025 by Ketkinaina (Talk | contribs)

(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye spoken tutorial kuhusu Viewing and Printing text documents.
00:07 Katika tutorial hii tutajifunza jinsi ya Kuangalia maandishi na Kuchapisha maandishi kwenye LibreOffice Writer.
00:17 Tutorial hii imerekodiwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS toleo 18.04 na
00:25 LibreOffice Suite toleo 6.3.5
00:29 Chaguzi za kutazama Tutaanza kwa kujifunza kuhusu chaguzi mbalimbali za kutazama katika LibreOffice Writer.
00:37 Kuna chaguzi mbili zinazotumika sana za kutazama katika Writer.
00:42 Hizo ni Normal na Web.
00:45 Chaguo la Normal linaonyesha jinsi maandishi yatakavyoonekana yakichapishwa.
00:50 Chaguo la Web linaonyesha maandishi kama yanavyoonekana kwenye web browser.
00:55 Hii ni muhimu tunapotaka kuunda maandishi ya HTML.
01:00 Hii pia ni muhimu tunapotaka kutazama maandishi katika hali ya full screen kwa ajili ya kuyahariri.
01:07 Fungua faili “Resume.odt” ambalo tuliunda awali.
01:12 Faili hili limewekwa kwako kwenye kiungo cha Code files katika ukurasa huu wa tutorial.
01:17 Tafadhali pakua na lichambue faili hilo.
01:20 Tengeneza nakala na kisha litumie kwa kufanya mazoezi.
01:24 Ili kufikia chaguo la Normal, bonyeza View menu katika menu bar. Kisha bonyeza chaguo la Normal.
01:34 Ili kufikia chaguo la Web, bonyeza View menu katika menu bar. Halafu bonyeza chaguo la Web.
01:42 Mbali na chaguzi hizi mbili, mtu anaweza pia kutazama maandishi katika hali ya full screen.
01:49 Bonyeza View menu katika menu bar na kisha chagua chaguo la Full Screen.
01:55 Hali ya Full screen ni muhimu kwa kuhariri maandishi.
01:59 Pia ni muhimu kwa kuyaonyesha kwenye projeta.
02:04 Bonyeza kitufe cha Full Screen au Escape ili kutoka kwenye hali ya full screen.
02:10 Tumerudi kwenye dirisha la Writer.
02:13 Sasa, hebu bonyeza tena View menu na kisha kwenye chaguo la Normal.
02:20 Kabla ya kuendelea zaidi, hebu tuongeze ukurasa mpya kwenye maandishi yetu.
02:25 Bonyeza Insert menu kwenye menu bar, kisha chagua chaguo la Page break.
02:32 Tumehamia kwenye ukurasa mpya katika maandishi.
02:36 Bonyeza funguo za Ctrl+Z ili kufuta mabadiliko haya.
02:40 Hebu nionyeshe njia nyingine ya kuongeza ukurasa mpya.
02:44 Bonyeza Insert menu katika menu bar kisha chagua More Breaks. Chagua Manual Break kama chaguo dogo.
02:54 Dirisha la mazungumzo la Insert Break linafunguka.
02:58 Hapa, chagua chaguo la Page break.
03:02 Kisha bonyeza kitufe cha OK katika dirisha hilo.
03:07 Sasa hebu tuandike maandishi ya mfano kwenye mistari michache ya ukurasa huu mpya.
03:13 Tutaongeza ukurasa mwingine kwa kubonyeza pamoja funguo za Ctrl+Enter.
03:19 Na tuandike maandishi haya ya mfano kwenye ukurasa huu mpya.
03:23 Bonyeza funguo za Ctrl+Enter tena na unda ukurasa mwingine mpya.
03:29 Kisha andika maandishi haya ya mfano katika ukurasa huo mpya.
03:33 Sasa, hebu tujifunze kutumia chaguo la Zoom.
03:37 Njia rahisi ya kukuza au kupunguza maandishi ni kutumia Zoom slider.
03:43 Hii iko kwenye kona ya chini kulia ya dirisha la Writer.
03:48 Tunaweza kutumia alama za plus na minus pande zote mbili za slider, kama hivi.
03:56 Au tunaweza kuvuta Zoom head ili kuongeza au kupunguza ukubwa wa maandishi, kama hivi.
04:03 Hebu tujifunze njia nyingine ya kutumia Zoom.
04:06 Bonyeza View menu kwenye menu bar na kisha bonyeza Zoom.
04:11 Chaguo kadhaa zinaonyeshwa kwenye menyu ya muktadha.
04:15 Tutapuuza hizi na kubonyeza chaguo la Zoom.
04:19 Dirisha la mazungumzo la Zoom & View Layout linafunguka.
04:23 Lina vichwa viwili vya habari ambavyo ni - Zoom Factor na View Layout.
04:29 Zoom Factor huweka kiwango cha kukuza ambacho kitaonyesha maandishi.
04:34 Chini ya Zoom Factor tunaona chaguo nyingi.
04:38 Bonyeza Optimal na kisha bonyeza kitufe cha Ok kilicho kona ya chini kulia.
04:43 Ukifanya hivyo, utapata mwonekano wa maandishi ulio bora zaidi na wa kustarehesha.
04:48 Fungua tena dirisha la mazungumzo la Zoom & View Layout.
04:52 Bonyeza Fit width and height kisha bonyeza Ok upande wa chini kulia.
04:58 Mwonekano huu hulinganisha maandishi na upana na urefu wa ukurasa mzima. Kwa hivyo, ukurasa mmoja huonyeshwa kwa wakati mmoja.
05:07 Chaguo linalofuata ni Fit Width. Hili hulinganisha ukurasa kwa upana wake.
05:13 Mwonekano wa 100% utaonyesha ukurasa kwa ukubwa wake halisi.
05:17 Jaribu chaguo hizi mbili peke yako.
05:20 Sasa tuna chaguo muhimu zaidi la zoom linaloitwa Variable.
05:25 Hapa, tunaweza kuandika kiwango cha kukuza tunachotaka kuona maandishi nacho.
05:31 Kwa mfano, hebu tuandike thamani 75% kwenye sehemu ya Variable, kisha bonyeza kitufe cha OK.
05:41 Angalia jinsi maandishi yanavyokuzwa.
05:45 Kipengele kingine kwenye dirisha la mazungumzo ni View Layout.
05:50 Tunaona chaguzi mbili hapa - Automatic na Single page.
05:55 Chaguo la Automatic huonyesha kurasa sambamba upande kwa upande.
05:59 Single page huonyesha kurasa moja chini ya nyingine.
06:03 Hebu tujaribu mchanganyiko wa baadhi ya haya.
06:06 Kwa mfano - tuchague chaguo la Fit width and height chini ya Zoom Factor.
06:12 Kisha bonyeza chaguo la Automatic chini ya View Layout, na bonyeza kitufe cha OK.
06:20 Tunaona kuwa kurasa zinaonyeshwa kando kwa kando.
06:24 Fungua tena dirisha la mazungumzo la Zoom & View Layout, kama inavyoonyeshwa hapa.
06:30 Wakati huu tuchague Single page chini ya View Layout na bonyeza kitufe cha OK.
06:37 Tunaona kuwa kurasa zinaonyeshwa moja chini ya nyingine.
06:41 Tumia zoom slider na ulete Zoom head katikati ya slider.
06:47 Kuna vidhibiti vingine 3 kwenye Writer Status Bar ambavyo vinaweza kutumika kuonyesha kurasa.
06:53 Hivi pia vinaturuhusu kubadilisha zoom na view layout ya document yetu.
06:59 Aikoni ni kama ifuatavyo:
07:02 Single-page view, Multiple-page view na Book view.
07:08 Book view huonyesha kurasa mbili zilizo jirani, kama kitabu kilichofunguliwa.
07:14 Bonyeza Single page view na ulete Zoom head katikati ya zoom slider.
07:21 Sasa tutajifunza kuhusu Print Preview.
07:25 Bonyeza aikoni ya Toggle Print Preview kwenye Standard toolbar.
07:29 Print Preview bar huonekana tunapoiangalia document katika hali ya kuangalia kabla ya kuchapisha.
07:35 Kimsingi inaonyesha jinsi document itakavyoonekana itakapochapishwa.
07:40 Sogeza chini kuona kurasa zote katika document.
07:45 Kutoka kwenye skrini hii, mtu anaweza kuendelea kuchapisha document kwa kubonyeza aikoni ya Print. Lakini sitafanya hivyo sasa.
07:54 Bonyeza kitufe cha Close Preview ili kufunga mwonekano wa chapisho.
07:58 Tunaweza pia kubonyeza File menu kwenye menu bar na kuchagua Print Preview.
08:05 Kisha, tutajifunza jinsi ya print document yetu ya LibreOffice Writer.
08:10 Tafadhali hakikisha kwamba muunganisho wa printa umewekwa vizuri kwenye kompyuta yako.
08:15 Ili kuprint document yote moja kwa moja, bonyeza aikoni ya Print kwenye Standard toolbar. Hii inajulikana kama uchapishaji wa haraka.
08:24 Tunaweza kupata udhibiti zaidi wa kuchapisha document yetu kwa kutumia chaguo la Print.
08:30 Bonyeza kwenye File menu katika menu bar kisha bonyeza Print.
08:37 Kisanduku cha mazungumzo cha Print kitaonekana kwenye skrini.
08:41 Kuna tabs mbili zenye mipangilio tofauti katika kisanduku hiki.
08:46 Tunaweza kuziacha kama zilivyo au kubadilisha kulingana na mahitaji yetu ya kuchapisha.
08:53 Chini ya Printer drop-down, tuchague chaguo la Print to File.
08:59 Chaguo hili hutumika zaidi kuchapisha document kama faili ya aina ya PDF.
09:05 Kitufe kilicho chini ya kisanduku cha mazungumzo kinasema Print to File. Bonyeza hapo.
09:12 Chagua sehemu ya kuhifadhi na andika jina la faili jipya. Kisha bonyeza kitufe cha Save kilicho juu kulia.
09:21 Document itachapishwa kama faili.
09:24 Bonyeza funguo za Ctrl+P kwenye kibodi yako. Hii ni njia ya mkato kufungua kisanduku cha Print.
09:31 Wakati huu chini ya Printer, tutachagua jina la printa tuliyoipangilia.
09:37 Chini ya Range and Copies, Nitachagua Pages kuwa 2 na Number of copies kuwa 3.
09:46 Mwisho, bonyeza kitufe cha OK kuanza kuchapisha.
09:51 Kurasa na nakala tulizotaja sasa zitachapishwa.
09:56 Sasa, tutaona jinsi ya kufikia chaguo nyingine za Print.
10:01 Bonyeza Tools menu katika menu bar kisha bonyeza Options.
10:07 Bonyeza mshale pembeni mwa LibreOffice kisha bonyeza Print.
10:12 Kisanduku cha mazungumzo kitaonekana kwenye skrini kikitoa chaguzi mbalimbali za kuchagua.
10:18 Chagua chaguzi hizi kulingana na mahitaji yako.
10:21 Mipangilio hii sasa itatumika kwa uchapishaji wote kutoka LibreOffice Writer, siku zijazo.
10:27 Nitabaki na mipangilio ya awali kisha bonyeza kitufe cha OK kilicho chini.
10:33 Hifadhi faili letu kwa kubonyeza funguo za Ctrl + S.
10:37 Kisha lifunge kwa kubonyeza ikoni ya X iliyopo juu kulia.
10:42 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. Hebu tufanye muhtasari.
10:47 Katika mafunzo haya, tulijifunza: Kuangalia document, Print document kwenye LibreOffice Writer
10:56 Kama zoezi Fungua faili ya practice.odt
11:00 Andika maandishi “This is LibreOffice Writer”
11:04 Chagua View na uchague chaguo la Full Screen
11:08 Toka kwenye chaguo la Full Screen
11:11 Chunguza chaguo zote za Zoom zilizopo
11:14 Chunguza chaguo zote za Page preview zilizopo
11:18 Video ifuatayo inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial. Tafadhali ipakue na uitazame.
11:25 Tunaendesha workshop kwa kutumia spoken tutorials na tunatoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi.
11:33 Tuma maswali yako yenye muda maalum kwenye jukwaa hili.
11:36 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India.
11:41 Mafunzo haya yalitolewa awali na DesiCrew Solutions Pvt. Ltd. mwaka 2011
11:48 Mimi ni Maira Magoma pamoja na timu ya Spoken Tutorial kutoka IIT Bombay kwaheri. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina