LibreOffice-Suite-Writer-6.3/C2/Tables-and-table-properties-in-Writer/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Revision as of 22:21, 14 May 2025 by Ketkinaina (Talk | contribs)

(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye spoken tutorial kuhusu Table and table properties.
00:07 Katika somo hili tutajifunza jinsi ya:
00:12 Kuweka table kwenye document ya Writer
00:15 Kuongeza na kubadilisha rows na columns
00:18 Na kurekebisha table properties kulingana na tunavyopendelea.
00:23 Somo hili limerekodiwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS 18.04 na LibreOffice Suite toleo la 6.3.5
00:36 Umepewa mafaili mawili kwenye kiungo cha Code files kwenye ukurasa huu wa mafunzo. Tafadhali yapakue na uyafungue.
00:46 Tengeneza nakala, kisha uyatumie kwa mazoezi.
00:50 Fungua faili la Resume.odt tulilounda awali.
00:56 Sasa tujifunze jinsi ya kuingiza Tables kwenye document ya Writer.
01:02 Weka mshale mwisho wa EDUCATION DETAILS kisha bonyeza Enter.
01:08 Ili kuingiza table kwenye document, bonyeza aikoni ya Insert table kwenye Standard toolbar.
01:15 Sasa, chagua ukubwa wa table, yaani idadi ya rows na columns unazohitaji.
01:22 Nitachagua chaguo la 2X4 linalonipa rows 4 na columns 2.
01:30 Ngoja nikuonyeshe njia nyingine ya kuingiza table kwenye document ya Writer.
01:36 Kabla ya hapo, bonyeza Ctrl + Z ili kufuta mabadiliko.
01:43 Sasa bonyeza Table menu kwenye menu bar, kisha chagua Insert table.
01:51 Kisanduku cha Insert Table kinafunguka kikiwa na fields kadhaa.
01:56 Kwenye Name tuandike jina la table kuwa Resumetable.
02:02 Tutaacha idadi ya Columns kuwa 2.
02:06 Kwenye Rows, bonyeza kitufe cha Plus kuongeza idadi.
02:13 Bonyeza kitufe cha Minus kupunguza idadi. Tuirudishe hadi 3.
02:20 Chini kuna orodha ya Styles.
02:24 Tunaweza kuchagua style ya table kutoka hapa tukitaka.
02:30 Kwa sasa, tutabonyeza chaguo la Default Style.
02:35 Kisha bonyeza kitufe cha Insert kilicho kona ya chini kulia.
02:40 Table yenye columns mbili na rows tatu inawekwa chini ya EDUCATION DETAILS.
02:47 Sasa tunaweza kuandika taarifa kwenye table kwa mtindo wa tabular.
02:53 Angalia toolbar mpya kwa chini.
02:57 Hapa kuna njia za mkato kwa vipengele vya kawaida vya table.
03:02 Bonyeza ndani ya cell ya row ya 1 na mstari wa 1 wa table.
03:08 Hapa tutaandika Secondary School Examination.
03:13 Sasa bonyeza cell ya karibu, andika 93 %.
03:19 Vivyo hivyo, tutaandika taarifa nyingine za elimu kwenye table, kama inavyoonyeshwa.
03:25 Kuongeza row mpya, tumia aikoni ya Rows below kwenye table toolbar chini.
03:33 Tukiwa kwenye row ya mwisho ya table, bonyeza kitufe cha Tab. Hii itaongeza row nyingine kwenye table.
03:43 Bonyeza row ya 2, column ya 1.
03:47 Kubonyeza Tab kunatusogeza mbele kutoka cell hadi cell.
03:52 Kubonyeza Shift + Tab kunatusogeza nyuma kutoka cell hadi cell.
03:57 Kwenye row ya mwisho, andika PhD CSE kwenye column ya 1 na 2015 kwenye column ya 2.
04:07 Kipengele kingine muhimu cha tables ni kubadilisha saizi ya rows na columns.
04:13 Tunaweza kurekebisha urefu na upana wa rows na columns kwa njia mbalimbali.
04:21 Tunaweza kuongeza upana wa column kwa kuvuta ukingo kwa kutumia cursor. Vivyo hivyo, tunaweza kupunguza upana pia.
04:32 Tunaweza kufanya hivyo hivyo kwa urefu wa row.
04:36 Sasa weka cursor kwenye column ya 2 ya row yoyote kisha bonyeza.
04:42 Kisha bonyeza Table menu kwenye Menu toolbar na uchague chaguo la Size.
04:49 Sasa chagua Minimize Column Width.
04:54 Upana wa column utajiweka moja kwa moja.
04:59 Unalingana na upana wa maudhui ya cells kwenye column hiyo.
05:04 Sasa tujifunze mbinu nzuri za kutumia tables.
05:08 Nitatumia faili la Table hyphen demo dot odt kwa sehemu hii ya maonyesho.
05:16 Fungua faili la Table hyphen demo dot odt ulilopakua awali kwenye Writer.
05:24 Hapa nina table yenye columns 2 na rows 5.
05:29 Kuchagua column nzima, peleka cursor juu ya column ya table.
05:35 Cursor hubadilika kuwa mshale unaoelekea chini.
05:39 Sasa bonyeza kitufe cha kushoto cha mausi. Column nzima inachaguliwa.
05:45 Tuweke maandishi katikati kwa kubonyeza aikoni ya Centre Align.
05:51 Maandishi yote kwenye column hii yatawekwa katikati.
05:55 Sasa bonyeza sehemu yoyote kwenye document ili kuondoa uchaguzi.
05:59 Halafu, peleka cursor juu kushoto mwa table.
06:04 Cursor hubadilika kuwa mshale ulioegemea chini kulia.
06:08 Bonyeza kitufe cha kushoto cha mausi. Table nzima inachaguliwa.
06:14 Sasa bonyeza sehemu yoyote ya document ili kuondoa uchaguzi.
06:18 Bonyeza ndani ya cell yoyote kwenye table.
06:22 Safari hii, chagua table nzima kwa kubonyeza aikoni ya Select Table kwenye toolbar.
06:29 Bonyeza Table menu kwenye menu bar, kisha uchague Properties.
06:35 Au bonyeza aikoni ya Table Properties kwenye table toolbar.
06:41 Njia zote zinafungua kisanduku cha Table Properties. Hapa tunaona tabs nyingi na chaguzi nyingi.
06:50 Kulia kabisa, utaona Alignment iko kwenye Automatic.
06:55 Kwanza, tubadili hii kuwa Left.
06:58 Ukifanya hivyo, chaguzi nyingine zinazokuwa zimezimwa zinawezeshwa.
07:04 Tuipe hii table jina la MyTable1 na tubadilishe Width kuwa sentimita 12.
07:12 Bonyeza kitufe cha OK kilicho chini ya kisanduku.
07:17 Angalia mabadiliko ya ukubwa wa columns.
07:21 Tena, bonyeza ndani ya cell yoyote kwenye table.
07:26 Bonyeza tena aikoni ya Table Properties kwenye table toolbar.
07:31 Bonyeza tab ya Column.
07:34 Chini ya sehemu ya Column Width, utaona 1 na 2 ndizo zenye kuwezeshwa. Hii ni kwa sababu tuna columns 2 tu kwenye table.
07:46 Hapa, badilisha thamani ya column ya pili kuwa 10cm.
07:52 Bonyeza kisanduku cha tiki cha Adjust columns proportionally.
07:57 Kisha bonyeza kitufe cha OK kilicho chini kulia.
08:02
08:06 Bonyeza aikoni ya Select Table kwenye table toolbar.
08:11 Sasa bonyeza aikoni ya Optimize Size kwenye table toolbar.
08:16 Hii ni njia ya mkato ya kurekebisha upana wa rows na columns.
08:21 Chagua chaguo la Distribute Columns Evenly.
08:25 Sasa columns zote zina upana sawa.
08:29 Tunaweza pia kuongeza upana wa column kwa kuvuta ukingo kwa cursor. Vivyo hivyo, tunaweza kupunguza upana pia.
08:40 Tunaweza kufanya hivyo hivyo kwa urefu wa row.
08:44 Sasa tujifunze namna ya kufanya kazi na cells ndani ya table.
08:49 Bonyeza ndani ya cell kwenye column ya pili, row ya 3.
08:54 Weka vitufe vya Shift na Ctrl vikiwa vimebanwa, kisha peleka cursor kwenye ukingo wa kushoto wa column.
09:01 Kisha tumia mausi kuvuta ukingo kuelekea kushoto kama inavyoonyeshwa. Ukingo wa cell hiyo unasogea!
09:11 Sasa tutajifunza kugawanya na kuunganisha cells.
09:16 Bonyeza ndani ya cell ya column ya pili, row ya 3.
09:21 Kwenye table toolbar, bonyeza aikoni ya Split Cells.
09:26 Kisanduku cha mazungumzo kinafunguka chenye chaguzi kadhaa.
09:30 Kwenye sehemu ya Split cell into, tutaandika 3.
09:35 Kwenye sehemu ya Direction, tuchague Vertically, kisha bonyeza kitufe cha OK.
09:42 Cell imegawanywa kuwa cells 3 sawa.
09:46 Sasa tuchague hizo cells 3 na tubonyeze aikoni ya Merge Cells kwenye table toolbar. Cells 3 zimeunganishwa.
09:56 Hivyo ndivyo tunavyogawanya na kuunganisha cells ndani ya table kwenye Writer.
10:01 Tena bonyeza ndani ya cell kwenye column ya pili, row ya 3.
10:07 Tunaweza hata kugawa table kuwa 2 kwa kubonyeza aikoni ya Split Table kwenye table toolbar.
10:14 Kisanduku cha mazungumzo kinafunguka, kinaonyesha chaguzi kadhaa.
10:18 Kulingana na chaguo tunalochagua, table itagawiwa ipasavyo.
10:23 Kwanza nitachagua No heading na kubonyeza kitufe cha OK.
10:28 Table inagawanywa kuwa tables 2. Bonyeza Ctrl + Z kufuta hatua hii.
10:35 Tena bonyeza ndani ya cell kwenye column ya pili, row ya 3.
10:41 Bonyeza aikoni ya Split Table kwenye table toolbar.
10:45 Nitachagua chaguo la Copy heading na kubonyeza kitufe cha OK.
10:50 Table inagawanywa kuwa tables 2 na headings sawa.
10:55 Hebu tujifunze zaidi kuhusu chaguzi za alignment.
10:59 Kabla ya hayo, vuta chini border ya row ya chini ya table's heading row ya pili.
11:05 Chagua row nzima ya header kama inavyoonyeshwa hapa.
11:09 Sasa, angalia chaguzi za alignment kwa cell, kwenye table toolbar.
11:15 Align Top imeteuliwa kwa chaguo-msingi.
11:18 Bonyeza Align Bottom na Centre Vertically kuona jinsi maandishi yanavyo alainiwa ndani ya cell.
11:25 Ili kutoa rangi ya nyuma ya cell, kwanza bonyeza ndani ya cell.
11:30 Katika table toolbar, bonyeza aikoni ya Table Cell Background Color.
11:35 Rangi ya manjano ni rangi ya kivuli ya chaguo-msingi.
11:38 Ili kufungua rangi zote, bonyeza mshale mwelekeo chini ya aikoni hiyo. Hapa sasa tunaweza kuchagua rangi nyingine.
11:48 Kando ya aikoni ya Background Color, tunaona aikoni ya Autoformat Styles.
11:54 Kisanduku cha mazungumzo cha AutoFormat kinafunguka.
11:57 Tunaona mitindo mbalimbali hapa ambayo tunaweza kutumia kwenye table yetu, ikiwa tunataka.
12:03 Bonyeza kitufe cha Cancel.
12:06 Katika table toolbar, tunaona aikoni za kuchagua mipaka tofauti, mitindo ya border, rangi za border.
12:15 Pia kuna aikoni za njia fupi za miundo ya nambari kwenye table toolbar.
12:21 Chunguza chaguzi zote hizi wewe mwenyewe.
12:24 Hifadhi faili letu kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl + S. Kisha lifunge kwa kubonyeza aikoni ya X kwenye kona ya juu kulia.
12:32 Hii inatufikisha mwisho wa tutorial hii.
12:36 Katika tutorial hii, tulijifunza jinsi ya Kuongeza table kwenye Writer document
12:42 Kuongeza na kubadili row na column
12:46 Kusawazisha table properties kulingana na upendeleo wetu
12:50 Kama kazi ya nyumbani Fungua practice.odt.
12:54 Ingiza table yenye row 3 na column 2
12:58 Ongeza vichwa vya row kama "Column One" na "Column Two"
13:03 Ongeza maandishi katika cells zote za table Hifadhi na funga faili
13:10 Video inayofuata inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial Tafadhali pakua na itazame.
13:18 Tunafanya semina kwa kutumia spoken tutorials na tunatoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, Tafadhali wasiliana nasi.
13:27 Tafadhali tuma maswali yako na wakati katika jukwaa hili.
13:31 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD Serikali ya India
13:36 Script ya tutorial hii imetolewa na Nancy Varkey kutoka IIT Bombay. Mimi ni Maira Magoma kutoka IIT Bombay kwaheri.. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina