LibreOffice-Suite-Calc-6.3/C2/Basic-Data-manipulation-in-Calc/Swahili
From Script | Spoken-Tutorial
Revision as of 17:54, 14 May 2025 by Ketkinaina (Talk | contribs)
| Time | Narration |
| 00:01 | Karibu kwenye Mafunzo Simulizi kuhusu Basic Data Manipulation kwenye Calc. |
| 00:07 | Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya: |
| 00:11 | Kutumia baadhi ya Formula za msingi kwenye Calc |
| 00:15 | Kupanga kwa safu na Kuchuja data |
| 00:20 | Somo hili limeandikwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS toleo 18.04 na LibreOffice Suite toleo 6.3.5 |
| 00:34 | Je, formula ni nini? |
| 00:36 | Fomula ni mlinganyo unaotumia nambari na vigeu ili kupata jibu. |
| 00:43 | Variables ni cell locations zenye data muhimu kwa ajili ya equation. |
| 00:50 | Shughuli za Msingi za Hisabati Kwanza, tutajifunza jinsi ya kufanya baadhi ya mahesabu ya msingi ya hisabati katika Calc.. |
| 01:00 | Hiyo ni kujumlisha, kutoa, kuzidisha na gawanya. |
| 01:07 | Fungua faili la Personal Finance Tracker dot ods. |
| 01:12 | Hebu tujumlishe gharama ya matumizi yote yaliyotajwa chini ya heading Cost. |
| 01:19 | Tutaandika Jumla Kuu moja kwa moja chini ya Mengineyo. |
| 01:25 | Kisha bonyeza kwenye cell A8 na uandike namba ya mfuatano kama 7. |
| 01:33 | Sasa bonyeza kwenye cell C8 ambapo tunataka kuonyesha jumla ya costs. |
| 01:42 | Andika sawa-sawa na SUM na ndani ya mabano weka safu ya safu wima zitakazojumlishwa. Yaani C3 hadi C7 |
| 01:55 | Sasa bonyeza Enter. |
| 01:58 | Angalia kwamba kiasi chote chini ya Cost kimejumlishwa na jumla inaonekana kwenye cell C8. |
| 02:07 | Sasa, hebu tujifunze jinsi ya kufanya kutoa kwenye Calc. |
| 02:12 | Tuseme tunataka kutoa gharama za House Rent na Electricity Bill. |
| 02:19 | Tutaonyesha hii kwenye cell C10. |
| 02:23 | Bofya kwenye seli C10 kisha andika yafuatayo – “sawa-sawa na C3 kutoa C4”. |
| 02:33 | Bonyeza Enter. Angalia thamani kwenye cell C10. |
| 02:39 | Inaonyesha thamani ya kutoa kati ya C3 na C4. |
| 02:45 | Vivyo hivyo, mtu anaweza gawanya na zidisha data katika seli tofauti. |
| 02:52 | Bonyeza kwenye cell C11 na andika “is equal to C5 asterix C6” kisha bonyeza Enter. |
| 03:04 | Jibu la kuzidisha linaonyeshwa katika seli C11. |
| 03:10 | Bofya kwenye seli C12 kisha andika “sawa-sawa na C3 gawanya C6” na bonyeza Enter. |
| 03:22 | Jibu la mgawanyo linaonekana kwenye cell C12. |
| 03:27 | Hebu turudishe mabadiliko ya mgawanyiko, kuzidisha na kutoa tuliyoyafanya. |
| 03:35 | Ili kufanya hivyo, bonyeza kitufe cha Ctrl+Z mara tatu. |
| 03:41 | Operesheni nyingine ya msingi katika spreadsheet ni kupata wastani wa namba. Hebu tuone jinsi ya kufanya hivyo. |
| 03:50 | Kwenye cell B9, tuandike heading kama Average. |
| 03:56 | Hapa tunataka kuonyesha wastani wa gharama jumla. |
| 04:01 | Halafu bonyeza kwenye cell C9. |
| 04:05 | Na andika sawa-sawa na Average na ndani ya mabano C3 hadi C7. Bonyeza Enter |
| 04:16 | Tunaona kwamba wastani wa safu ya Cost unaonekana kwenye cell. |
| 04:23 | Hebu turejeshe mabadiliko kwa kubonyeza vitufe vya: Ctrl+Z. |
| 04:29 | Vivyo hivyo, tunaweza kupata wastani wa vitu kwenye safu ya mlalo pia. |
| 04:36 | Tutajifunza kuhusu fomula na vifanyikazi vingine baadaye katika mfululizo huu |
| 04:43 | Sasa hebu tujifunze jinsi ya kupanga data kwenye Calc spreadsheet. |
| 04:48 | Kupanga kunaweka safu na mstari katika spreadsheet kwa mpangilio unaoeleweka. |
| 04:55 | Kupanga kunatusaidia kuchambua na kuona data kwa ufanisi zaidi. |
| 05:02 | Hufanya iwe rahisi kutafuta na kupata kitu ndani ya sheet yote. |
| 05:09 | Tunaweza kupanga data tukitumia hadi vigezo vitatu, vinavyotumika mfululizo. |
| 05:17 | Kupanga kunaweza kutumika kwa sheet yote au sehemu ya cells. |
| 05:23 | Kwa kawaida, data hupangwa kulingana na thamani halisi. Kwa mfano: kupanda, kushuka, alfabeti, kushoto kwenda kulia, ya zamani hadi mpya, n.k. |
| 05:39 | Tutapanga data chini ya heading Costs kwa mpangilio wa kupanda. |
| 05:45 | Sasa, kwa kubonyeza kitufe cha kushoto cha panya, chagua cells C1 hadi C7. |
| 05:52 | Hii inachagua safu ya cells tunayotaka kupanga. |
| 05:57 | Nenda kwenye Standard toolbar. Hapa tunaweza kuona alama tatu tofauti za sorting. |
| 06:04 | Bonyeza ikoni ya Sort Ascending. |
| 06:07 | Kisanduku cha mazungumzo cha Sort range kinaonekana. |
| 06:11 | Bonyeza kitufe cha Current selection. |
| 06:14 | Angalia kuwa nambari kwenye cells zilizochaguliwa sasa zimepangwa kwa mpangilio wa kupanda. |
| 06:21 | Bonyeza ikoni ya Sort Descending. |
| 06:24 | Kwenye kisanduku cha mazungumzo cha Sort range, bonyeza kitufe cha Current selection. |
| 06:30 | Angalia kuwa nambari kwenye cells zilizochaguliwa sasa zimepangwa kwa mpangilio wa kushuka. |
| 06:37 | Rudisha mabadiliko haya kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl+Z mara mbili. |
| 06:43 | Nambari zote zimerudi kwenye cells zao za awali. |
| 06:48 | Ili kupata udhibiti zaidi wa kupanga data, bonyeza ikoni ya Sort. |
| 06:54 | Vinginevyo, tunaweza kwenda kwenye menu bar na kubonyeza Data. Kisha bonyeza Sort kutoka kwenye orodha ndogo. |
| 07:05 | Kwenye kisanduku cha mazungumzo cha Sort Range, bonyeza tena kitufe cha Current selection. |
| 07:11 | Wakati huu, kisanduku kingine cha Sort kinaonekana chenye tab mbili: Sort criteria na Options. |
| 07:19 | Tab ya Sort criteria imechaguliwa kwa chaguo-msingi. Chini yake, tunaweza kuona Sort keys tatu. |
| 07:27 | Chini ya orodha ya kuchagua kwenye Sort key 1, chagua Cost. |
| 07:32 | Kisha bonyeza chaguo la Ascending lililo karibu na hilo. |
| 07:37 | Ili kupanga kwa mpangilio wa kushuka, bonyeza chaguo la Descending. Mimi nitachagua chaguo la Ascending. |
| 07:46 | Sasa bonyeza kitufe cha OK kilichopo kona ya chini kulia. |
| 07:51 | Tunaona kwamba safu ya Cost imepangwa kwa mpangilio wa kupanda. |
| 07:57 | Hebu turejeshe mabadiliko haya kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl+Z. |
| 08:02 | Safu nyingi pia zinaweza kupangwa kwa mara moja. |
| 08:07 | Ili kufanya hivyo, chagua kwanza safu nyingi, kisha tumia chaguzi za sort. Nitakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo. |
| 08:16 | Tuseme tunataka kupanga Serial numbers, Items pamoja na Cost. |
| 08:23 | Kwa hiyo, chagua kwanza safu zote 3: SN, Items na Cost kama inavyoonyeshwa hapa. |
| 08:31 | Sasa nenda kwenye menu bar na bonyeza Data. Kutoka kwenye menyu ndogo, bonyeza Sort. |
| 08:40 | Kisanduku cha mazungumzo cha Sort kinafunguka. |
| 08:43 | Chini ya tab ya Sort criteria, kwenye menyu ya Sort key 1, chagua Cost. |
| 08:50 | Kisha kwenye menyu ya Sort key 2, chagua SN. |
| 08:55 | Na kwenye menyu ya Sort key 3, chagua Items. |
| 09:00 | Bonyeza Descending kwenye chaguzi mbili za kwanza za sort. |
| 09:05 | Bonyeza Ascending kwenye chaguo la tatu la sort. |
| 09:09 | Kisha bonyeza kitufe cha OK. |
| 09:13 | Angalia mabadiliko. Tunaona kuwa safu zote zimepangwa kulingana na maagizo yaliyowekwa. |
| 09:22 | Hebu turejeshe mabadiliko haya. |
| 09:26 | Sasa hebu tujifunze jinsi ya kuchuja data kwenye Calc. |
| 09:31 | Filter ni orodha ya masharti ambayo kila kipengele kinapaswa kutimiza ili kionekane. |
| 09:39 | Nitakuonyesha kipengele hiki. |
| 09:43 | Ili kutumia filter, bonyeza kwenye cell yoyote, kwa mfano cell. iliyoandikwa Items |
| 09:52 | Bonyeza ikoni ya Auto Filter kwenye Standard toolbar. |
| 09:57 | Vinginevyo, unaweza kwenda kwenye menu bar na kubonyeza Data. Kisha bonyeza Auto Filter kutoka kwenye menyu ndogo. |
| 10:08 | Tunaona mshale wa kushuka umeonekana kwenye kichwa cha Items. |
| 10:15 | Bonyeza mshale huo wa kushuka. |
| 10:18 | Kisanduku cha pop-up cha Filter kinafunguka. |
| 10:21 | Sasa tuseme tunataka kuonyesha data ya Electricity Bill pekee. |
| 10:27 | Kwa hiyo, kwanza toa alama kwenye chaguo la All. |
| 10:32 | Kisha weka alama kwenye chaguo la Electricity Bill na bonyeza kitufe cha Ok. |
| 10:39 | Ni data ya Electricity Bill pekee inayoonekana kwenye sheet. Vipengele vingine vimechujwa. |
| 10:49 | Ili kuona tena data yote, bonyeza mshale wa kushuka kwenye cell Items. |
| 10:57 | Weka alama kwenye chaguo la All. |
| 11:00 | Hakikisha kuwa vichwa vyote vimechaguliwa kisha bonyeza kitufe cha Ok. |
| 11:05 | Sasa tunaweza kuona data yote tuliyokuwa nayo kwenye sheet. |
| 11:12 | Kuna filters nyingine katika Calc ambazo tutajifunza kwenye mafunzo yajayo ya mfululizo huu. |
| 11:19 | Tuweke na tufunge faili. |
| 11:22 | Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. Hebu tufanye muhtasari. |
| 11:27 | Katika mafunzo haya, tulijifunza jinsi ya: Kutumia Formula ya msingi kwenye Calc, Kupanga kwa safu na Kuchuja data |
| 11:38 | Kama kazi ya nyumbani: |
| 11:40 | Fungua “spreadsheet hyphen practice dot ods” faili. |
| 11:45 | Panga safu ya Salary kwa mpangilio wa Ascending |
| 11:49 | Chuja safu ya Name na uonyeshe Rahul’s data. |
| 11:54 | Rejesha mabadiliko. |
| 11:57 | Video kwenye kiungo kifuatacho inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial. Tafadhali ipakue na uiangalie. |
| 12:05 | Timu ya Mradi wa Spoken Tutorial huendesha warsha na kutoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie. |
| 12:15 | Tafadhali tuma maswali yako yaliyo na muda kwenye jukwaa hili. |
| 12:19 | Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India. |
| 12:25 | Mimi ni msimulizi wako, Hokins Moshi kutoka IIT Bombay; Na Kwa heri. Asante kwa kutazama. |