LibreOffice-Suite-Calc-6.3/C2/Introduction-to-LibreOffice-Calc/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Revision as of 15:41, 14 May 2025 by Ketkinaina (Talk | contribs)

(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye mafunzo simulizi ya awali kuhusu LibreOffice Calc.
00:06 Katika mafunzo haya, tutajifunza:
00:09 Kuhusu LibreOffice Calc
00:12 Menyu mbalimbali za toolbars
00:14 Jinsi ya kufungua spreadsheet mpya na iliyopo tayari.
00:18 Jinsi ya kuhifadhi na kufunga spreadsheet katika Calc
00:22 Jinsi ya kuhifadhi kama MS Excel spreadsheet na
00:26 Jinsi ya kuhamisha kuwa hati ya PDF
00:30 Nini maana ya LibreOffice Calc? LibreOffice Calc ni sehemu ya spreadsheet katika LibreOffice Suite.
00:38 Ni sawa na Microsoft Excel katika Microsoft Office Suite.
00:43 Ni programu huria na ya bure.
00:47 Inaweza kushirikiwa, kubadilishwa na kusambazwa bila vikwazo vyovyote.
00:53 LibreOffice Calc inaweza kufanya kazi katika mifumo ifuatayo:
00:57 Microsoft Windows 8 au matoleo ya juu zaidi
01:02 GNU/Linux OS na Mac OSX
01:08 Mafunzo haya yameandikwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS toleo 18.04 na LibreOffice Suite toleo 6.3.5
01:22 Kwa kawaida, toleo jipya la Ubuntu Linux OS huwa na LibreOffice tayari limewekwa.
01:29 Ili kusanidi toleo maalum, angalia mfululizo wa LibreOffice Installation kwenye tovuti hii.
01:37 Sasa tujifunze kufungua LibreOffice Calc.
01:41 Katika Ubuntu Linux OS, bonyeza ikoni ya Show Applications iliyoko chini kushoto.
01:49 Kwenye search bar, andika Calc.
01:53 Kutoka kwenye orodha inayoonekana, bonyeza ikoni ya Libreoffice Calc.
01:59 Katika Windows OS, bonyeza ikoni ya Start Menu iliyoko chini kushoto.
02:06 Kwenye search bar, andika Calc.
02:10 Kutoka kwenye orodha inayoonekana, bonyeza ikoni ya Libreoffice Calc.
02:16 Hii itafungua hati tupu ya spreadsheet kwenye dirisha kuu la Calc.
02:22 Sasa tujifunze kuhusu sehemu kuu za dirisha la Calc.
02:28 Dirisha la Calc lina toolbars mbalimbali.
02:32 Title bar, Menu bar, Standard toolbar, Formatting bar, Formula bar, Status bar na Sidebar.
02:47 Tutajifunza kuhusu haya kadri mfululizo unavyoendelea.
02:51 Hati nzima ya spreadsheet katika Calc inaitwa workbook.
02:56 Eneo la kazi ambapo data inaandikwa lina cells mbalimbali kwa mfumo wa gridi.
03:04 Kwa maneno mengine, cells zimepangiliwa katika rows na columns.
03:10 Cell maalum huwakilisha muunganiko wa row na column.
03:16 Hutambulika kwa row number na herufi ya column.
03:22 Cells zinaweza kubeba taarifa kama maandishi, namba, fomula, na vipengele vingine vya data.
03:31 Cells zinaweza kutumika kuonyesha na kuendesha data.
03:36 Tunaweza kuona kichupo cha sheet chini kushoto mwa-spreadsheet. Kichupo hiki hutoa ufikiaji wa sheet.
03:46 Kwa kawaida, tunaona sheet moja kwenye kiolesura na inaitwa Sheet 1.
03:53 Kila spreadsheet inaweza kuwa na sheets kadhaa.
03:57 Kila sheet inaweza kuwa na zaidi ya milioni moja rows na zaidi ya elfu moja columns.
04:03 Hii ni zaidi ya bilioni moja au seli laki mia moja za cells kwenye sheet moja.
04:09 Kila row hutambulika kwa number na kila column kwa herufi ya Kiingereza.
04:16 Kuna mfululizo wa grey boxes zilizo na herufi juu ya kila column.
04:22 Vivyo hivyo, tunaona grey boxes zilizo na namba upande wa kushoto wa rows.
04:29 Hizi ni column na row headers.
04:33 Columns huanza na “A” na kuendelea kulia.
04:38 Na rows huanza na “1” na kwenda chini.
04:43 Pamoja na toolbars, kuna sehemu mbili za ziada juu kabisa. Name box na Input line.
04:53 Column na row headers huunda cell references. Na hizi huonekana kwenye sehemu ya Name box.
05:02 Haya yalikuwa maelezo mafupi ya vipengele mbalimbali vya Calc.
05:06 Sasa tujifunze jinsi ya kufungua spreadsheet mpya katika Calc.
05:12 Tunaweza kufungua spreadsheet mpya kwa kubonyeza ikoni ya New kwenye Standard toolbar.
05:19 Vinginevyo, nenda kwenye menyu ya File menu kwenye menu bar.
05:24 Kisha bonyeza menyu ndogo ya New na uchague chaguo la Spreadsheet.
05:31 Calc spreadsheet mpya inayoitwa Untitled 2 itafunguka.
05:37 Funga spreadsheet mpya iliyoitwa “Untitled 2” kwa kubonyeza ikoni ya X iliyo juu kulia.
05:45 Sasa tutajifunza jinsi ya kutengeneza “Personal Finance Tracker” kwenye spreadsheet.
05:50 Bonyeza kwenye cell inayoitwa A1 ndani ya spreadsheet.
05:55 Andika kichwa cha habari “SN”.
06:00 Hii inawakilisha number ya mfuatano wa vitu ambavyo tutaweka kwenye spreadsheet.
06:06 Sasa bonyeza kwenye cell ya B1 na andika kichwa kingine “Items”.
06:13 Majina yote ya vitu tutakavyotumia kwenye spreadsheet yatawekwa chini ya kichwa hiki.
06:19 Vivyo hivyo, bonyeza kwenye cells za C1, D1, E1, F1 na G1 moja baada ya nyingine.
06:29 Andika vichwa vya habari kama “Cost”, “Spent”, “Received”, “Date” na “Account” kwa mpangilio huo.
06:43 Baada ya kumaliza kuandika hati yetu, tunapaswa kuihifadhi kwa matumizi ya baadaye.
06:49 Ili kuhifadhi faili, bonyeza ikoni ya Save kwenye Standard toolbar.
06:55 Kisanduku cha mazungumzo kitaonekana kwenye skrini.
06:59 Kitatuomba tuingize jina la faili letu kwenye sehemu ya Name.
07:04 Nitaandika jina la faili kama “Personal Finance Tracker”.
07:11 Upande wa kushoto, nitachagua Desktop kama sehemu ya kuhifadhi faili.
07:18 Angalia, kuna menyu kunjuzi ya File type chini kulia.
07:24 Bonyeza menyu hii kunjuzi.
07:27 Inaonyesha orodha ya file types au file extensions ambazo tunaweza kuhifadhi faili letu.
07:35 File type chaguo-msingi katika LibreOffice Calc ni ODF Spreadsheet (.ods).
07:43 ODF ni kifupi cha Open Document Format ambacho ni kiwango huria.
07:49 Nitabonyeza chaguo la ODF Spreadsheet ili kuhifadhi faili langu. Fanya vivyo hivyo kwenye mashine yako.
07:58 Bonyeza kitufe cha Save kilicho juu kulia mwa kisanduku cha mazungumzo.
08:04 Tutarejeshwa kwenye dirisha la Calc.
08:08 Angalia mabadiliko kwenye title bar sasa.
08:12 Sasa limebadilika kuwa Personal Finance Tracker dot ods
08:18 Mbali na kuhifadhi kwa fomati ya dot ods, tunaweza pia kuhifadhi faili kwa dot xls na dot xlsx.
08:28 Faili zilizo kwenye fomati hizi zinaweza kufunguliwa baadaye kwenye programu ya MS Excel.
08:36 Bonyeza mshale wa menyu kunjuzi karibu na ikoni ya Save kisha uchague chaguo la Save As.
08:43 Katika kisanduku cha Save As, bonyeza menyu kunjuzi ya File type chini kulia.
08:50 Chagua fomati ya Excel 2007 hyphen 365 (.xlsx).
08:59 Bonyeza kitufe cha Save kilicho juu kulia mwa kisanduku cha mazungumzo.
09:05 Tukihifadhi faili kwa fomati nyingine yoyote, kisanduku cha Confirm File Format kitaonekana.
09:13 Weka tiki kwenye chaguo la “Ask when not saving in ODF or default format
09:20 Kisha bonyeza kitufe cha Use Excel 2007 hyphen 365 format.
09:28 Tutarejeshwa tena kwenye dirisha la Calc.
09:32 Angalia mabadiliko ya jina la faili kwenye Title bar.
09:37 Spreadsheet pia inaweza kusafirishwa kama PDF.
09:42 Ili kufanya hivyo, bonyeza ikoni ya Export Directly as PDF kwenye Standard toolbar.
09:49 Vinginevyo, tunaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza menyu ya File menu kwenye menu bar. Kisha bonyeza chaguo la Export as PDF.
09:59 Kisanduku cha PDF options kitafunguka.
10:03 Katika kisanduku hiki, tutaona mipangilio mbalimbali ya kubinafsisha chaguo la PDF.
10:10 Acha mipangilio iliyopo kama ilivyo kisha bonyeza kitufe cha Export kilicho chini.
10:17 Chagua mahali ambapo tunataka kuhifadhi faili, kisha bonyeza kitufe cha Save.
10:24 Faili ya pdf itaundwa katika folda hiyo.
10:29 File extension nyingine maarufu inayofunguka katika programu nyingi ni dot csv.
10:36 Hii hutumika mara nyingi kuhifadhi spreadsheet data katika fomati ya faili ya maandishi.
10:43 Hii inapunguza ukubwa wa faili kwa kiasi kikubwa na ni rahisi kubeba.
10:49 Zaidi ya hayo, tunaweza kuhifadhi spreadsheet katika fomati ya dot html, ambayo ni web page format. Hii hufanyika kwa njia ile ile iliyoelezwa hapo juu.
11:03 Katika menyu kunjuzi ya File type, chagua HTML Document (Calc)(.html).
11:10 Chaguo hili hutoa kiendelezi cha dot html kwa spreadsheet.
11:16 Chagua tena eneo lile lile la kuhifadhi faili.
11:21 Kisha bonyeza kitufe cha Save kilicho juu kulia mwa kisanduku cha mazungumzo.
11:27 Kisanduku cha Confirm File Format kitafunguka.
11:31 Weka tiki kwenye chaguo la “Ask when not saving in ODF or default format
11:38 Kisha bonyeza kitufe cha Use HTML Document (Calc) Format.
11:46 Tunaona faili limehifadhiwa kwa kiendelezi cha dot html.
11:52 Fomati hii hutumika tunapotaka kuonyesha spreadsheet yetu kama web page.
11:58 Inaweza kufunguliwa katika web browser yoyote.
12:02 Tufunge spreadsheet hii kwa kubonyeza File menu kisha Close.
12:10 Sasa tutajifunza jinsi ya kufungua spreadsheet iliyopo katika LibreOffice Calc.
12:17 Tufungue spreadsheet Personal Finance Tracker dot ods
12:22 Bonyeza menyu ya Open File upande wa kushoto wa kiolesura cha LibreOffice.
12:28 Kisanduku cha kuchagua faili kitafunguka.
12:32 Nenda kwenye eneo ambako faili letu liliokolewa.
12:36 Sasa katika orodha ya majina ya faili yanayoonekana, chagua Personal Finance Tracker dot ods.
12:44 Kisha bonyeza kitufe cha Open kilicho juu kulia.
12:49 Faili Personal Finance Tracker dot ods linafunguliwa kwenye dirisha la Calc.
12:56 Vivyo hivyo, tunaweza pia kufungua mafaili yenye viendelezi vya dot xls na dot xlsx katika Calc.
13:06 Sasa tuone jinsi ya kurekebisha faili na kuihifadhi kwa jina lile lile.
13:13 Hivyo basi, tuhariri faili kwa kufanya vichwa vya habari kuwa bold na kuongeza ukubwa wa maandishi.
13:20 Kwa kufanya hivyo, bonyeza kwanza cell yenye rejeleo A1.
13:25 Sasa bonyeza ikoni ya Bold katika Standard toolbar. Kichwa cha habari SN kinakuwa bold.
13:34 Bonyeza mshale wa kushuka chini kwenye sehemu ya Font Size katika Standard toolbar.
13:40 Katika menyu kunjuzi, tuchague 14.
13:44 Ukubwa wa maandishi ya kichwa SN unaongezeka kuwa 14.
13:49 Sasa, tuweke font tofauti tunayopenda kutumia.
13:54 Bonyeza mshale wa kushuka chini kwenye sehemu ya Font Name katika Standard toolbar.
14:00 Kutoka kwenye menyu kunjuzi, chagua Arial kama font.
14:05 Vivyo hivyo, hariri vichwa vingine vya habari.
14:10 Sasa tuhifadhi mabadiliko tuliyofanya.
14:14 Kwa kufanya hivyo, bonyeza ikoni ya Save kwenye Standard toolbar.
14:19 Tufunge spreadsheet sasa.
14:22 Bonyeza menyu ya File kwenye menu bar kisha bonyeza chaguo la Close.
14:29 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya ya sauti. Tufanye muhtasari.
14:36 Katika mafunzo haya, tulijifunza:
14:39 Kuhusu LibreOffice Calc.
14:41 Menyu mbalimbali za toolbars ndani ya Calc.
14:45 Jinsi ya kufungua spreadsheet mpya na iliyohifadhiwa.
14:49 Jinsi ya kuhifadhi na kufunga spreadsheet.
14:52 Jinsi ya kuihifadhi kama MS Excel spreadsheet na
14:56 Jinsi ya kuipeleka kama PDF katika Calc.
15:01 Kama kazi ya nyumbani, Fungua spreadsheet mpya kwenye Calc.
15:06 Ihifadhi kwa jina Spreadsheet-Practice.ods
15:11 Andika vichwa vya habari kama “SN”, “Name”, “Department” na “Salary”.
15:18 Piga mstari chini ya vichwa vya habari na vifanye kuwa bold.
15:22 Ongeza font size ya vichwa vya habari hadi 12.
15:26 Hifadhi na funga faili.
15:29 Video kwenye kiungo kifuatacho inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial. Tafadhali ipakue na uitazame.
15:38 Tunaendesha warsha tukitumia spoken tutorials na tunatoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie.
15:48 Una maswali kuhusu Spoken Tutorial hii?
15:52 Tafadhali tembelea tovuti hii
15:55 Chagua dakika na sekunde ambapo una swali
16:00 Eleza swali lako kwa kifupi
16:03 Timu ya mradi wa Spoken Tutorial itahakikisha unapata jibu
16:08 Utahitaji kujisajili kwenye tovuti hii ili kuuliza maswali.
16:13 Jukwaa la Spoken Tutorial ni kwa maswali maalum ya mafunzo haya.
16:19 Tafadhali usichapishe maswali yasiyo husiana au ya jumla. Hii itasaidia kupunguza machafuko.
16:27 Tukiwa na machafuko machache, tunaweza kutumia mijadala hii kama nyenzo ya kufundishia.
16:33 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India.
16:40 Mafunzo haya yalitolewa awali na DesiCrew Solutions Pvt. Ltd. Mwaka 2011

Tuki hitimisha, Ni mimi Hokins Moshi pamoja na timu ya Spoken Tutorial kutoka IIT Bombay. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina