LibreOffice-Suite-Calc-6.3/C2/Basic-Data-manipulation-in-Calc/Swahili

From Script | Spoken-Tutorial
Revision as of 18:05, 14 May 2025 by Ketkinaina (Talk | contribs)

(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search
Time Narration
00:01 Karibu kwenye Mafunzo Simulizi kuhusu Basic Data Manipulation kwenye Calc.
00:07 Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya:
00:11 Kutumia baadhi ya Formula za msingi kwenye Calc
00:15 Kupanga kwa safu na Kuchuja data
00:20 Somo hili limeandikwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS toleo 18.04 na LibreOffice Suite toleo 6.3.5
00:34 Je, formula ni nini?
00:36 Fomula ni mlinganyo unaotumia nambari na vigeu ili kupata jibu.
00:43 Variables ni cell locations zenye data muhimu kwa ajili ya equation.
00:50 Shughuli za Msingi za Hisabati Kwanza, tutajifunza jinsi ya kufanya baadhi ya mahesabu ya msingi ya hisabati katika Calc..
01:00 Hiyo ni kujumlisha, kutoa, kuzidisha na gawanya.
01:07 Fungua faili la Personal Finance Tracker dot ods.
01:12 Hebu tujumlishe gharama ya matumizi yote yaliyotajwa chini ya heading Cost.
01:19 Tutaandika Jumla Kuu moja kwa moja chini ya Mengineyo.
01:25 Kisha bonyeza kwenye cell A8 na uandike namba ya mfuatano kama 7.
01:33 Sasa bonyeza kwenye cell C8 ambapo tunataka kuonyesha jumla ya costs.
01:42 Andika sawa-sawa na SUM na ndani ya mabano weka safu ya safu wima zitakazojumlishwa. Yaani C3 hadi C7
01:55 Sasa bonyeza Enter.
01:58 Angalia kwamba kiasi chote chini ya Cost kimejumlishwa na jumla inaonekana kwenye cell C8.
02:07 Sasa, hebu tujifunze jinsi ya kufanya kutoa kwenye Calc.
02:12 Tuseme tunataka kutoa gharama za House Rent na Electricity Bill.
02:19 Tutaonyesha hii kwenye cell C10.
02:23 Bofya kwenye seli C10 kisha andika yafuatayo – sawa-sawa na C3 kutoa C4.
02:33 Bonyeza Enter. Angalia thamani kwenye cell C10.
02:39 Inaonyesha thamani ya kutoa kati ya C3 na C4.
02:45 Vivyo hivyo, mtu anaweza gawanya na zidisha data katika seli tofauti.
02:52 Bonyeza kwenye cell C11 na andika is equal to C5 asterix C6 kisha bonyeza Enter.
03:04 Jibu la kuzidisha linaonyeshwa katika seli C11.
03:10 Bofya kwenye seli C12 kisha andika sawa-sawa na C3 gawanya C6 na bonyeza kitufe cha Enter.
03:22 Jibu la mgawanyo linaonekana kwenye cell C12.
03:27 Hebu turudishe mabadiliko ya mgawanyiko, kuzidisha na kutoa tuliyoyafanya.
03:35 Ili kufanya hivyo, bonyeza kitufe cha Ctrl+Z mara tatu.
03:41 Operesheni nyingine ya msingi katika spreadsheet ni kupata wastani wa namba. Hebu tuone jinsi ya kufanya hivyo.
03:50 Kwenye cell B9, tuandike heading kama Average.
03:56 Hapa tunataka kuonyesha wastani wa gharama jumla.
04:01 Halafu bonyeza kwenye cell C9.
04:05 Na andika sawa-sawa na Average na ndani ya mabano C3 hadi C7. Bonyeza Enter.
04:16 Tunaona kwamba wastani wa safu ya Cost unaonekana kwenye cell.
04:23 Hebu turejeshe mabadiliko kwa kubonyeza vitufe vya: Ctrl+Z.
04:29 Vivyo hivyo, tunaweza kupata wastani wa vitu kwenye safu ya mlalo pia.
04:36 Tutajifunza kuhusu fomula na vifanyikazi vingine baadaye katika mfululizo huu
04:43 Sasa hebu tujifunze jinsi ya kupanga data kwenye Calc spreadsheet.
04:48 Kupanga kunaweka safu na mstari katika spreadsheet kwa mpangilio unaoeleweka.
04:55 Kupanga kunatusaidia kuchambua na kuona data kwa ufanisi zaidi.
05:02 Hufanya iwe rahisi kutafuta na kupata kitu ndani ya sheet yote.
05:09 Tunaweza kupanga data tukitumia hadi vigezo vitatu, vinavyotumika mfululizo.
05:17 Kupanga kunaweza kutumika kwa sheet yote au sehemu ya cells.
05:23 Kwa kawaida, data hupangwa kulingana na thamani halisi. Kwa mfano: kupanda, kushuka, alfabeti, kushoto kwenda kulia, ya zamani hadi mpya, n.k.
05:39 Tutapanga data chini ya heading Costs kwa mpangilio wa kupanda.
05:45 Sasa, kwa kubonyeza kitufe cha kushoto cha panya, chagua cells C1 hadi C7.
05:52 Hii inachagua safu ya cells tunayotaka kupanga.
05:57 Nenda kwenye Standard toolbar. Hapa tunaweza kuona alama tatu tofauti za sorting.
06:04 Bonyeza ikoni ya Sort Ascending.
06:07 Kisanduku cha mazungumzo cha Sort range kinaonekana.
06:11 Bonyeza kitufe cha Current selection.
06:14 Angalia kuwa nambari kwenye cells zilizochaguliwa sasa zimepangwa kwa mpangilio wa kupanda.
06:21 Bonyeza ikoni ya Sort Descending.
06:24 Kwenye kisanduku cha mazungumzo cha Sort range, bonyeza kitufe cha Current selection.
06:30 Angalia kuwa nambari kwenye cells zilizochaguliwa sasa zimepangwa kwa mpangilio wa kushuka.
06:37 Rudisha mabadiliko haya kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl+Z mara mbili.
06:43 Nambari zote zimerudi kwenye cells zao za awali.
06:48 Ili kupata udhibiti zaidi wa kupanga data, bonyeza ikoni ya Sort.
06:54 Vinginevyo, tunaweza kwenda kwenye menu bar na kubonyeza Data. Kisha bonyeza Sort kutoka kwenye orodha ndogo.
07:05 Kwenye kisanduku cha mazungumzo cha Sort Range, bonyeza tena kitufe cha Current selection.
07:11 Wakati huu, kisanduku kingine cha Sort kinaonekana chenye tab mbili: Sort criteria na Options.
07:19 Tab ya Sort criteria imechaguliwa kwa chaguo-msingi. Chini yake, tunaweza kuona Sort keys tatu.
07:27 Chini ya orodha ya kuchagua kwenye Sort key 1, chagua Cost.
07:32 Kisha bonyeza chaguo la Ascending lililo karibu na hilo.
07:37 Ili kupanga kwa mpangilio wa kushuka, bonyeza chaguo la Descending. Mimi nitachagua chaguo la Ascending.
07:46 Sasa bonyeza kitufe cha OK kilichopo kona ya chini kulia.
07:51 Tunaona kwamba safu ya Cost imepangwa kwa mpangilio wa kupanda.
07:57 Hebu turejeshe mabadiliko haya kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl+Z.
08:02 Safu nyingi pia zinaweza kupangwa kwa mara moja.
08:07 Ili kufanya hivyo, chagua kwanza safu nyingi, kisha tumia chaguzi za sort. Nitakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo.
08:16 Tuseme tunataka kupanga Serial numbers, Items pamoja na Cost.
08:23 Kwa hiyo, chagua kwanza safu zote 3: SN, Items na Cost kama inavyoonyeshwa hapa.
08:31 Sasa nenda kwenye menu bar na bonyeza Data. Kutoka kwenye menyu ndogo, bonyeza Sort.
08:40 Kisanduku cha mazungumzo cha Sort kinafunguka.
08:43 Chini ya tab ya Sort criteria, kwenye menyu ya Sort key 1, chagua Cost.
08:50 Kisha kwenye menyu ya Sort key 2, chagua SN.
08:55 Na kwenye menyu ya Sort key 3, chagua Items.
09:00 Bonyeza Descending kwenye chaguzi mbili za kwanza za sort.
09:05 Bonyeza Ascending kwenye chaguo la tatu la sort.
09:09 Kisha bonyeza kitufe cha OK.
09:13 Angalia mabadiliko. Tunaona kuwa safu zote zimepangwa kulingana na maagizo yaliyowekwa.
09:22 Hebu turejeshe mabadiliko haya.
09:26 Sasa hebu tujifunze jinsi ya kuchuja data kwenye Calc.
09:31 Filter ni orodha ya masharti ambayo kila kipengele kinapaswa kutimiza ili kionekane.
09:39 Nitakuonyesha kipengele hiki.
09:43 Ili kutumia filter, bonyeza kwenye cell yoyote, kwa mfano cell. iliyoandikwa Items
09:52 Bonyeza ikoni ya Auto Filter kwenye Standard toolbar.
09:57 Vinginevyo, unaweza kwenda kwenye menu bar na kubonyeza Data. Kisha bonyeza Auto Filter kutoka kwenye menyu ndogo.
10:08 Tunaona mshale wa kushuka umeonekana kwenye kichwa cha Items.
10:15 Bonyeza mshale huo wa kushuka.
10:18 Kisanduku cha pop-up cha Filter kinafunguka.
10:21 Sasa tuseme tunataka kuonyesha data ya Electricity Bill pekee.
10:27 Kwa hiyo, kwanza toa alama kwenye chaguo la All.
10:32 Kisha weka alama kwenye chaguo la Electricity Bill na bonyeza kitufe cha Ok.
10:39 Ni data ya Electricity Bill pekee inayoonekana kwenye sheet. Vipengele vingine vimechujwa.
10:49 Ili kuona tena data yote, bonyeza mshale wa kushuka kwenye cell Items.
10:57 Weka alama kwenye chaguo la All.
11:00 Hakikisha kuwa vichwa vyote vimechaguliwa kisha bonyeza kitufe cha Ok.
11:05 Sasa tunaweza kuona data yote tuliyokuwa nayo kwenye sheet.
11:12 Kuna filters nyingine katika Calc ambazo tutajifunza kwenye mafunzo yajayo ya mfululizo huu.
11:19 Tuweke na tufunge faili.
11:22 Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya. Hebu tufanye muhtasari.
11:27 Katika mafunzo haya, tulijifunza jinsi ya: Kutumia Formula ya msingi kwenye Calc, Kupanga kwa safu na Kuchuja data
11:38 Kama kazi ya nyumbani:
11:40 Fungua “spreadsheet hyphen practice dot ods” faili.
11:45 Panga safu ya Salary kwa mpangilio wa Ascending
11:49 Chuja safu ya Name na uonyeshe Rahul’s data.
11:54 Rejesha mabadiliko.
11:57 Video kwenye kiungo kifuatacho inatoa muhtasari wa mradi wa Spoken Tutorial. Tafadhali ipakue na uiangalie.
12:05 Timu ya Mradi wa Spoken Tutorial huendesha warsha na kutoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie.
12:15 Tafadhali tuma maswali yako yaliyo na muda kwenye jukwaa hili.
12:19 Mradi wa Spoken Tutorial unafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India.
12:25 Mimi ni msimulizi wako, Hokins Moshi kutoka IIT Bombay; Na Kwa heri. Asante kwa kutazama.

Contributors and Content Editors

Ketkinaina