Difference between revisions of "LibreOffice-Suite-Calc-6.3/C2/Formatting-Data--in-Calc/Swahili"
From Script | Spoken-Tutorial
Ketkinaina (Talk | contribs) (Created page with "{|border=1 |- || ''' Time''' || '''Narration''' |- || 00:01 || Karibu kwenye '''Mafunzo Simulizi''' kuhusu '''Formatting Data in Calc.''' |- || 00:07 || Katika somo hili...") |
Ketkinaina (Talk | contribs) |
||
| Line 42: | Line 42: | ||
|| 01:12 | || 01:12 | ||
|| Ikiwa umebadilisha ukubwa wa dirisha la '''LibreOffice''', baadhi ya ikoni huenda zisionekane. | || Ikiwa umebadilisha ukubwa wa dirisha la '''LibreOffice''', baadhi ya ikoni huenda zisionekane. | ||
| + | |- | ||
| + | || 01:18 | ||
| + | || Katika hali hiyo, bofya ikoni ya mishale miwili mwishoni mwa- zana ili kuona ikoni zilizofichwa. | ||
|- | |- | ||
|| 01:27 | || 01:27 | ||
Latest revision as of 17:58, 14 May 2025
| Time | Narration |
| 00:01 | Karibu kwenye Mafunzo Simulizi kuhusu Formatting Data in Calc. |
| 00:07 | Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya: |
| 00:11 | Kuweka muundo wa mipaka ya seli na Rangi Usuli za seli. |
| 00:16 | Kupanga maandishi ya mistari mingi kwa kutumia Automatic Wrapping. |
| 00:22 | Kuunganisha cells. |
| 00:25 | Kupunguza maandishi ili yaingie ndani ya cell. |
| 00:29 | Mafunzo haya yameandikwa kwa kutumia Ubuntu Linux OS toleo 18.04 na LibreOffice Suite toleo 6.3.5 |
| 00:42 | Kwanza, hebu tujifunze kuhusu kuweka muundo wa cell mipaka ndani ya Calc. |
| 00:47 | Fungua faili letu la Personal Finance Tracker dot ods. |
| 00:52 | Kuweka muundo wa mipaka kunaweza kufanyika kwenye cell moja au kundi la cells. |
| 00:59 | Chagua cells A2 hadi G2 kwa kushikilia kitufe cha kushoto cha kipanya. |
| 01:06 | Kisha nenda kwenye Formatting toolbar na uchague ikoni ya mipaka. |
| 01:12 | Ikiwa umebadilisha ukubwa wa dirisha la LibreOffice, baadhi ya ikoni huenda zisionekane. |
| 01:18 | Katika hali hiyo, bofya ikoni ya mishale miwili mwishoni mwa- zana ili kuona ikoni zilizofichwa. |
| 01:27 | Bofya kwenye ikoni ya mipaka. |
| 01:30 | Sanduku la kushuka linajitokeza likiwa na mitindo mbali-mbali ya Mitindo ya Mipaka. |
| 01:35 | Bofya kwenye yoyote ya mitindo unayotaka kutumia kwenye mipaka. Nitachagua chaguo la mwisho. |
| 01:45 | Sasa bofya mahali popote kwenye spreadsheet ili kutoa uteuzi cells. |
| 01:51 | Tazama kwamba cell mipaka zimepangwa kulingana na mitindo ya Mipaka iliyochaguliwa. |
| 01:58 | Hebu turudishe mabadiliko haya kwa kubofya vitufe vya: Ctrl+Z. |
| 02:03 | Tunaweza pia kufanya jambo hili kwa kutumia sanduku la majadiliano la Format cells. |
| 02:09 | Bonyeza kulia kwenye cells zilizochaguliwa na uchague chaguo la Format Cells. |
| 02:15 | Au bofya vitufe vya Ctrl+1 kwenye kibodi. |
| 02:20 | Kwa njia yoyote, sanduku la majadiliano la Format Cells litafunguliwa. Sasa nenda kwenye tab ya mipaka. |
| 02:29 | Tunaona chaguzi za Line arrangement, Line, Padding na Shadow style. |
| 02:38 | Mtu anaweza kubadilisha yoyote kati ya hizi kulingana na mapendeleo yetu. |
| 02:43 | Katika sehemu ya Line Arrangement, tunaona dirisha dogo la preview lililo na jina: User-defined. |
| 02:51 | Chini ya Pre-sets, nita bofya chaguo la tatu. |
| 02:56 | Unaweza kuona kwamba linajitokeza kwenye dirisha la preview. |
| 03:01 | Nitabadilisha pia Style, Width na Color kutoka sehemu ya Line, kama inavyoonyeshwa. |
| 03:09 | Kutoka kwenye menyu-kunjuzi ya style, nita chagua mistari ya dotted. |
| 03:15 | Nitaweka upana kuwa desimali 2 na kuchagua rangi kuwa Nyekundu. |
| 03:24 | Tazama mabadiliko kwenye dirisha la preview. |
| 03:28 | Sasa, nenda kwenye sehemu ya Padding. |
| 03:32 | Tazama kwamba thamani zote ni sawa. |
| 03:36 | Ikiwa tutajaribu kubadilisha thamani ya padding upande mmoja, zote zitabadilika. |
| 03:44 | Hii ni kwa sababu chaguo la Synchronize limechaguliwa. |
| 03:49 | Ikiwa tunataka kuweka thamani tofauti kwa kila upande, |
| 03:53 | basi chaguo la Synchronize linahitaji kuondolewa tiki. |
| 03:58 | Hebu tuondoe tiki kwenye chaguo la Synchronize. |
| 04:02 | Nitaweka thamani ya padding kwa juu na chini kuwa 1.5 mm. |
| 04:11 | Na Kushoto na Kulia kuwa 1 mm. |
| 04:16 | Unaweza kuchunguza mitindo ya vivuli baadaye kwa uhuru. |
| 04:21 | Bofya kwenye kifungo cha OK kilichopo chini. |
| 04:25 | Sasa bofya mahali popote kwenye spreadsheet ili kuondoa uteuzi cells. |
| 04:30 | Tazama kwamba mitindo ya mipaka tuliyochagua sasa imewekwa kwenye cells zote zilizochaguliwa. |
| 04:37 | Katika mafunzo yetu ya awali, tuliweka moja ya mitindo chaguo-msingi kwenye vichwa vya habari. |
| 04:43 | Sasa hebu tukaweke rangi zingine kwenye vichwa vya habari, tukitumia chaguo la Rangi ya Usuli. |
| 04:50 | Sasa chagua cells A1 hadi G1 kwa kushikilia kifungo cha panya cha kushoto. |
| 04:57 | Kisha nenda kwenye Formatting toolbar na chagua menyu kunjuzi inayofuata kwa ikoni ya Rangi Usuli. |
| 05:05 | Menyu ibukizi ya Rangi ya Usuli inafunguka. |
| 05:09 | Chagua rangi unayotaka kuweka kama rangi ya usuli kwenye seli.Mimi nitabofya rangi ya Chungwa. |
| 05:18 | Tazama mabadiliko. |
| 05:21 | Sasa rangi Usuli kwenye vichwa vya habari imewekwa kuwa Orange. |
| 05:26 | Calc inatoa chaguzi mbalimbali za kupamba mistari mingi ya maandishi. |
| 05:33 | Moja ya hizo ni Automatic Wrapping. |
| 05:36 | Inaruhusu mtumiaji kuandika mistari mingi ya maandishi kwenye cell moja. Hebu tujaribu hii. |
| 05:46 | Bonyeza kulia kwenye cell B9 na chagua chaguo la Format Cells. |
| 05:53 | Kisha nenda kwenye tab ya Alignment. |
| 05:57 | Chini ya sehemu ya Properties, weka tiki kwenye chaguo la Wrap text automatically. Kisha bofya kwenye kifungo cha OK kilichopo chini. |
| 06:09 | Sasa andika maandishi yafuatayo kwenye cell B9. |
| 06:14 | “This is a personal Finance Tracker. It is very useful.” Kisha bonyeza Enter. |
| 06:23 | Tunaona kwamba taarifa nyingi zinajipanga kwa wrap ndani ya cell hiyo hiyo. |
| 06:30 | Fanya uondoaji wa mabadiliko haya kwa kubonyeza vitufe vya: Ctrl+Z. |
| 06:36 | Sasa tutaweza kujifunza jinsi ya kuungana kwa cells katika Calc. |
| 06:41 | Kwanza bofya kwenye cell yenye thamani ya 1 chini ya kichwa habari, SN. |
| 06:47 | Sasa shikilia kitufe cha Shift kwenye kibodi kisha bofya kwenye cell yenye neno Salary. |
| 06:55 | Cells zilizochaguliwa zitakuwa na kivuli. |
| 06:58 | Bofya kwenye ikoni ya Merge and centre cells kwenye Formatting bar. |
| 07:06 | Dirisha la Merge Cells litajitokeza. |
| 07:10 | Hapa kuna chaguzi tatu za kuunganishwa kwa cells zinazoonyeshwa pamoja na muhtasari. Tunaweza kuchagua yoyote kulingana na upendeleo wetu. |
| 07:22 | Nataka kuhamisha maudhui ya cells zote mbili kuwa kwenye cell moja. |
| 07:28 | Hivyo, nitachagua kitufe cha redio cha: “Move the content of hidden cells into the first cell”. |
| 07:36 | Kisha bofya kwenye kitufe cha OK kilichopo chini ya dirisha la mazungumzo. |
| 07:42 | Tazama kuwa cells zilizochaguliwa na maudhui yao zimeunganishwa pamoja. |
| 07:48 | Kwa mbadala, tunaweza kuunganishwa kwa cells kwa kubofya kwenye Format menu kwenye menu bar. |
| 07:55 | Kutoka kwenye menyu ndogo, nenda kwenye Merge Cells na chagua chaguo lolote unalopendelea.Chunguza haya mwenyewe baadaye |
| 08:06 | Fanya uondoaji wa mabadiliko haya kwa kubonyeza vitufe vya: Ctrl+Z. |
| 08:12 | Sasa tutaweza kujifunza jinsi ya kupunguza maandishi ili yafaane ndani ya cell. |
| 08:18 | Ukubwa wa fonti wa data kwenye seli unaweza kurekebishwa kiotomatiki ili kufaa data hiyo kwenye seli.Hebu tujifunze jinsi ya kufanya hivyo. |
| 08:30 | Kwanza andika maandishi yafuatayo kwenye cell B10 This is for the month of June. Kisha bonyeza Enter. |
| 08:41 | Ili kupunguza maandishi, ili yaweze kufaa, bonyeza kulia kwenye seli B10. |
| 08:48 | Kisha chagua chaguo la Format Cells. |
| 08:53 | Dirisha la Format cells litajitokeza. |
| 08:57 | Nenda kwenye tab ya Alignment. |
| 09:00 | Chini ya sehemu ya Properties, bonyeza kisanduku cha kuangalia Shrink to fit cell size. |
| 09:07 | Kisha bonyeza kitufe cha OK kilichopo chini ya dirisha la mazungumzo. |
| 09:13 | Tazama kuwa, maandishi yote ndani ya cell yanapungua na kuendana na cell. |
| 09:20 | Yanaenda kujirekebisha kwa kupunguza saizi ya fonti ili maandishi yaingie ndani ya cell. |
| 09:28 | Fanya uondoaji wa mabadiliko kwa kubonyeza vitufe vya Ctrl+Z pamoja. |
| 09:35 | Kisha hifadhi na funga faili. |
| 09:40 | Hii inatufikisha mwisho wa mafunzo haya, hebu tufanye muhtasari. |
| 09:45 | Katika mafunzo haya, tulijifunza: |
| 09:49 | Kurekebisha cell mipaka na rangi usuli za seli. |
| 09:54 | Kurekebisha mistari mingi ya maandishi kwa kutumia Automatic Wrapping. |
| 09:59 | Kuuunganisha cells na |
| 10:01 | Kupunguza maandishi ili yafae ndani ya cell. |
| 10:06 | Kama kazi ya nyumbani:
Fungua “spreadsheet hyphen practice dot ods” faili. |
| 10:12 | Chagua headings zote. |
| 10:15 | Patia rangi ya rangi usuli ya kijivu kwa vichwa habari. |
| 10:19 | Kwa kutumia “Automatic Wrapping” andika maandishi kwenye cell A10 “This is a Department Spreadsheet”. |
| 10:27 | Punguza maandishi haya ili yafae ndani ya cell A11. |
| 10:33 | Video kwenye kiungo kilichofuata inatoa muhtasari wa Mradi wa Spoken Tutorial. Tafadhali pakua na angalia. |
| 10:41 | Timu ya Mradi wa Spoken Tutorial hufanya semina na kutoa vyeti. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tuandikie. |
| 10:51 | Tafadhali weka maswali yako ya wakati kwenye jukwaa hili. |
| 10:56 | Miradi ya Spoken Tutorial inafadhiliwa na MHRD, Serikali ya India. |
| 11:03 | Mafunzo haya yalitolewa awali na DesiCrew Solutions Pvt. Ltd. mwaka 2011 Mimi ni Hokins Moshi pamoja na timu ya Spoken Tutorial kutoka IIT Bombay, tunahitimisha kwa sasa. Asante kwa kutazama. |